50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 4,139
- 4,124
Wakuu wanabodi
Niende moja kwa moja kwenye hoja
Lengo la msingi la chama cha siasa ni kuingia kutwaa dola. Ima kwa hila au halali. Uchaguzi wa mbinu za halali ima za hila inategemea sana mazingira ya kisiasa ya wakati husika kwenye nchi. Hapa nyumbani kwa iliyokuwa Tanganyika upo ushahidi namna TANU ilifanikisha kutwaa dola kwa njia ambazo ni sahihi kuita ni njia halali za mazungumzo na chaguzi za hapa na pale. Huko Zanzibar, tunafahamu ASP ilivyotumia njia za hila kupindua serikali dhalimu ya Sultani na kutwaa dola. Itoshe kusema mbinu zote hizi huongozwa na hisabati za kisiasa. Ni nini hutokea ikiwa chama cha siasa kinapofanya makosa ya hisabati za kisiasa?
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa miaka karibu 17 sasa kimejinabaisha kuwa ni chama bora, chenye sera na mipango mikakati madhubuti, chenye watu wenye maono mujarabu (wakipenda kujiita wenye akili kubwa) na chenye uthubutu wa kutosha kuikosoa na kuikaripia serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Kishindo cha CHADEMA pale chama hiki kilipokuwa kikiitisha mikutano ama ya kanda ama kitaifa, kiliibua mvumo kwa rika na makundi yote ya Watanzania. Ilifika mahali Watanzania bila kujali imani, itikadi ama asili zao walipata matumaini mapya na siasa zetu wakiamini chama hiki ni mkombozi mpya. Hata viongozi waandamizi wa CHADEMA walitumia sana neno hili la ukombozi wa pili upo njiani kujinasua na CCM.
Makosa ya hisabati za kisiasa za CHADEMA yana historia ndefu. Kwa ufupi, moja ya makosa ya hisabati za kisiasa ya awali ya CHADEMA yalidhihirika wakati wa chaguzi za ndani za chama. Uchaguzi wa BAVICHA Taifa 2014 uliibua makundi ndani ya chama. Zipo taarifa zisizo rasmi kwamba baadhi ya washindi wa uchaguzi huu hawakupewa ushirikiano wa kutosha uongozi wa makao makuu, ilhali baadhi ya washindwa walipewa "recognition" iliyoibua mashaka ndani ya chama. Kama haitoshi, hakuna ushahidi wa kutosha kuonesha namna gani uongozi wa CHADEMA taifa ulishughulikia ipasavyo mpasuko uliojitokeza kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa BAVICHA Taifa 2014.
Kosa lingine la hisabati za kisiasa kwa CHADEMA lilidhihirika baada ya kuruhusu Dr Wilbroad Slaa kuondoka kufuatia ujio wa Mh Lowassa na kundi lake la M4U maarufu "ulipo tupo. CHADEMA kama chama kilichojitanabaisha kuwa na nia ya kutwaa dola, kilifanya kosa kubwa la kisiasa kumwacha Dr Slaa ajitenge na chama. Binafsi ni miongoni mwa wanaoamini kwamba ujio wa Mh Lowassa ndani ya chama hiki haukutokea kwa bahati mbaya. Bali ni suala lililopangwa na kuratibiwa vyema kwa muda mrefu na baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA. Hivyo ni sahihi kuhitimiha kwamba Dr Slaa alishtushwa na ujio wa wageni hawa maana hakuwa amejiandaa ama kuandaliwa mapema kuwapokea. Ikiwa Katibu Mkuu huyu angeandaliwa mapema kuwa Mh Lowassa ataletwa chamani, kisha kupewa hadhi ya ugombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano, upo uwezekano mkubwa kwamba Dr Slaa asingeondoka CHADEMA, na pengine muda huu ninavyoandika, CHADEMA ndio kingekuwa chama dola hapa Tanzania. Hili likuwa ni kosa jingine la hisabati za kisiasa linalokigharimu chama hiki.
Kama haitoshi, ujio wa Mh Lowassa na timu yake ulipokelewa kwa namna tofauti na wanachama wa CHADEMA. Ilifika wakati kukawa na tetesi za uwepo wa CHADEMA asili na CHADEMA academia. Hapa tunapata kosa jingine la msingi sana. Lipi? Hakuna ushahidi wa kutosha unaothibitisha kwamba viongozi waandamizi wa chama taifa walifanya jitihada za makusudi kuunganisha wanachama wake wageni na wale wa zamani. Ni wazi ipo sintofahamu ya nani hasa ni mfaidika nambari moja na ujenzi wa CHADEMA huko mashinani. Ni hawa wanachama wapya waliokuja na Mh Lowassa ama ni wale wa wanachama wa imani waliojengwa na uongozi wa Dr Slaa? Kosa la msingi hapa ni kushindwa kwa uongozi wa CHADEMA taifa kuja na mkakati wa kuwaweka sawa wanachama wake ili wasahau makosa yaliyopita, na kuganga yajayo. Kwa mfano, chama kilipaswa kuwa na mikakati ya kuwajenga upya wanachama wake kuhusu mwelekeo wa siasa za chama baada ya ujio wa Mh Lowassa, lakini mpaka sasa hakuna kitu kama hicho. Kiasi kwamba wanachama hawaelewi ni nini msimamo wa chama kuhusu kuisimamia serikali, na ni zipi agenda za kukisemea chama.
Kosa jingine hisabati za kisiasa la chama hiki ni kule kung'ang'ania mbinu iliyotumika kuidhiti CCM iliyokuwa ikiongozwa na Jakaya Kikwete, kwamba serikali inakandamiza demokrasia na kwamba serikali inafuja rasilimali za taifa na kwamba kila mradi wa serikali umegubikwa na rushwa. Maajabu kabisa. Kama nilivyoandika hapo juu, mbinu na mipango mikakati ya kisiasa inategemea zaidi hali ya kisiasa ya nchi. Hali ya siasa ya nchi inakuwa influenced na kiongozi anayetawala wakati huo. Kwa mfano, hoja tajwa zilizotumika kumdhibiti Mh Jakaya Kikwete na serikali yake, haziwezi kufua dafu kwa utawala huu wa Mh Magufuli. Kuhusu Mh Magufuli, utawala wake unagusa maisha ya kila siku kwa kila Mtanzania, utawala wa Magufuli unagusa na kubadilisha mahusiano kati ya mtu na mtu hapa nchini.
Mathalani, uhusiano wa raia na askari polisi ama uhusiano wa raia na watumishi wa umma umebadilika sana hivi sasa. Pia, utawala huu wa Magufuli namna taasisi za kijamii na mifumo inayoziongoza imebadilika sana. Upo ushahidi wa kutosha kuhusu namna taasisi za elimu zinavyojiongoza, idara za afya, mahakama, magereza na hata mifumo ya kibenki na masoko umebadilika sana. Vile vile, ijapokuwa ni mapema kuhitimisha, lakini zipo ishara kadhaa zinazoonesha kwamba jamii yetu inaanza kubadilika. Walau kwa kiasi kikubwa Watanzania wanaanza kuwa 'honest" na yale wanayoyasema na kutenda. Ujanja ujanja unaanza kutoweka taratibu. Sasa kwenye utawala huu wa Magufuli, huwezi kuiyumbusha serikali, taasisi zake ama asasi za kiraia, ama vikundi vya kijamii ama mtu mmoja mmoja kwa hoja nyepesi nyepesi za kisiasa. Hivyo, CHADEMA wanaendelea kufanya kosa kubwa sana kwenye hisabati za kisiasa kwa kuendelea kutumia mbinu zile zile za "name and shame" kwenye utawala huu. Maana umbua umbua haina nafasi tena.
Kosa jingine la hisabati za kisiasa wanalofanya CHADEMA wakati huu ni kususia hizi chaguzi za marudio. Mbaya zaidi, kundi la CHADEMA mitandaoni wanaungana na viongozi waandamizi wa CHADEMA bila kuhoji. Aibu sana kwa vijana wasomi wa chama hiki kuunga mkono pendekezo hili mfu la viongozi wakuu wa CHADEMA. Kimsingi, chaguzi hizi zinafanyika kwa sababu ni takwa ni kikatiba inapotea eneo fulani, ama jimbo ama kata haina mwakilishi. Sasa viongozi wakuu wa CHADEMA wanaposusia mahitaji ya kikatiba ni hatari sana. Mbaya zaidi, viongozi wakuu wa chama hiki hawafanyi jitihada zozote za makusudi, zenye mvumo kijamii ili kusukuma mabadiliko ya sheria ya uchaguzi. Badala yake wanasusa. Viongozi wanaosusia hitaji la kikatiba badala ya kupigania maboresho ya kikatiba wanaendelea kuthibitisha kwamba hawatoshi kuaminiwa kukabidhiwa dola.
Haya ni baadhi tu ya makosa ya msingi ya kihisabati za kisiasa ambayo CHADEMA wanafanya kila uchao. Humu sijagusia makosa ya kisiasa kwenye matumizi ya ruzuku za chama. Hili nitajadili wakati mwingine. Yapo makosa ya kihasabati za kisiasa kuhusu nafasi za viti maalumu vya udiwani ama ubunge. Yapo makosa kwenye teuzi mbali mbali za ndani ya chama ambazo baadhi ya wana CHADEMA wenyewe wameripoti humu, rejea "Vijana wa CHADEMA Tarime na utumwa ndani ya chama". Yapo makosa lukuki ya hisabati za kisiasa ambayo kwa weledi wa wana CHADEMA wakiwamo akina @Tundu Lissu @John Mnyika @Tumaini Makene wangeweza kuyasemea kukinusuru chama. Maana kuisema vibaya CCM hakuifanyi CHADEMA iwe madhubuti.
Mwisho, ikiwapendeza wana CHADEMA na wapenda demokrasia hapa Tanzania na wachambuzi wa siasa za Tanzania akina @Pascal Mayalla @Nguruvi3 @Lizaboni muendelee kuwaekeza CHADEMA kwamba ili chama kiwe madhubuti, kiweze kushika dola lazima kiwe na uvumilivu. Kiwavumilie wanasiasa wenye maono kama akina Kitila Mkumbo Zitto Kabwe @Samso Mwimgamba na wenzao wa calibre hiyo. Ima chama kikishindwa kuwavumilia wanasiasa wa namna hii, chama kiunde utaratibu mzuri wa kuhakikisha vijana wa namna hii hawaondoki chamani. Yaani chama kiwe na reserve list ya wanasiasa. Chama Cha Mapinduzi kinafanikiwa kuwa reserve list kwa vile chama hiki kikongwe kinao utaratibu wa kutekeleza haya. Maana yake ni kwamba hata kama CCM haina resources za kuwatunza wanasiasa wake, bado kinao mfumo makini wa kuwavutia wanachama mahiri. Ndio maana CCM ni chama pekee kilichokuwa tegemeo la kweli la Watanzania.
Baada ya machache haya, itoshe kusema kwamba, Ikiwa CHADEMA haitokubali kubadilika na kuendana na siasa mamboleo, chama hiki kitaendelea kuugulia maumivu ya makosa ya kihisabati za kisiasa huku wakiendelea kuilaumu CCM. Fursa ya CCM kuua upinzani ni fursa ambayo CHADEMA wanaitaka sana ili kuifuta CCM kwenye medani ya siasa za Tanzania. Binafsi sishtuki wala sishangai kuona chama dola (CCM) ikiendelea kutumia makosa ya CHADEMA kujiimarisha.
Niwatakie nyote mapumziko mema ya msimu wa sikukuu za Chrismas na mwaka mpya.