Tetesi: Account za CHADEMA kufungiwa !

Mkuu huna uwezo wa kuongea na CDF umshauri aokoe nchi?
 

Hilo nilipoona kapema sana .
Tone tone hata dumu mana lengo la CCM na serikali yake ni kuua upinzani wa kweli . Wanataka upinzani jaa.
Mifumo ya serikali na mifumo ya kinyonyaji inakuambia aliyefanya kazi asile kwa maana Kuwa wanataka kuzalisha watumwa kwanza watu wanaopokea amri zao .
Wao wanalimbikiza mali mpaka kizazi cha tano. Sijui hao wanawekewa mali wamefanya kazi saa ngapi!
na Any way Shetani ana roho Mbaya sana.
Ukipata Shida anakupotosha ili uende kwa waganga na kuona mwenyezi Mungu amekusahau na ukifanikiwa anakupotosha pia ili umsahau Mwenyezi Mungu .

Ndivyo serikali ya Chama cha Mashetani ilivyo . Mkiingia kwenye Uchaguzi wanavuruga vyama ,wanaowapiga ,wanawaua na kupora uchaguzi . Msipoingia wanavuruga vyama mwanawapiga ,wanawaua na kusema njoni tushiriki uchaguzi vinginevyo ninyi ni wahaini .


Nikimsikia Mwenyekiti wa ACT akujitapa Kuwa wao wataendelea kushiriki kwa sababu watu wao wengi walishumizwa na kuuawa tangu mwaka 1995 . Yaani Anasahau kabisa kuwa mkakati wa Tanganyika ya Sasa inalenga viongozi wa vyama na sio wanachama. Nimemdharau sana yule Mwenyekiti wa ACT kushangilia wanachama wake kuuawa. Kwa sasa serikali na vyombo vya dola ukihamasisha vurugu wanaanza na mhamasishaji kwanza .

Lakini pia anasahau Kuwa Tanganyika na Zanzibar ni tofauti sana .Watanganyika ni watu wa imani tofauti kuna imani nyingine hawaamini katika kuua binadamu bila kosa . Ndio maana hata Uhuru wa Tanganyika ulipatikana kwa amani baada ya misuguano mingi ya kudai uhuru. ACT Haitakuja kuitawala Zanzibar Milele bila Chadema kuingia Madarakani . Na pia Haitakuja kutawala Tanganyika milele CCM ikiwepo Madarakani .Itabaki kuwa ni msaada wa CCM kuendelea kutawala kwa sababu ya kucheza ngoma za CCM.

Kwenye suala la tone tone na fedha za Chadema kuzuiwa nadhani litakua gumu labda tu chadema wameelezea ule mfumo wao wa kuacha kutumia mahakama kudai haki zao . Michango ya wazi sio kosa katika jamii. Kuna harusi zinachangia mpaka miliini mia tano kwa miezi mitatu tu . Kuna misiba inachangiwa moja bili moja kwa siku tatu .

Michango ile ni ya wazi na inafanywa kwa wazi na inatoka ndani ya nchi sio nje . Waarabu wameingiza matrilioni ya kujisaidia CCM kuendesha ugaidi wao lakini hatuoni hatua ilichukuliwa sembuse tone tone .
Mungu wa haki atasimama . Wakati wa ukombozi ni sasa .
Hata hao wa hazina siku sio nyingi watamfuata Balali .
Fedha na dhahabu yote ni mali ya Mungu na Chadema imesimama na Mungu kuvunja na kubomoa utawala wa kishetani Tanganyika .
 
Master britanicca unawashauri nini viongozi wa Chadema, katika muktadha huo wachukue hatua zipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…