Acacia Yatutangaza Vibaya Duniani, Yadai Tanzania Kuna " risks to the safety and security of people"!, Mwekezaji Gani Ata Invest Kwenye Such Risks?!.

Madini hayaozi, waondoke. Sasa tunahitaji uwekezaji kwenye techno, educ
Karomije type no wonder Mkapa analialia eti viongozi goigoi waliokosa misimamo hawaendelezi waliyoyakuta bali wanabomoa kwa sababu wewe kihwani ni empty tin ni rahisi kusema waondoke
 
Mtu alishasema hashauliki...yeye ni jiwe. Lissu kashauri umeona kilichompata.....
Huo uzalendo wako kaupeleke mbugani
 

wao wanasema hivyo kwa vile imewakuta siku ya nyani ambapo miti yote inateleza.

Mbona wawekezaji wa kutoka Ujerumani, Korea Kusini, Neatherlands, United Kingdom na kwingine wanamiminika Dodoma?

Mbona balozi wetu Dr Slaa juzi kashuka na wawekezaji kuwaleta pale TIC?

Waache tuone wataishia wapi na kutapatapa wao.

Yaani leo hii wanaonyesha hawatambui kuwepo sheria ya Utakatishaji fedha na Deo Mwanyika walikuwa nae si wangemuuliza?
 
Acacia na Barrick wao wametuibia na kula mali yetu kwa miaka 10 mfululizo wakishirikiana na watanzania wenzetu waso waaminifu.

Miaka 10 ni mingi sana yatosha.

Watanzania tusiibeze serikali kwa kila jambo, kwenye hili tuiunge mkono serikali.
Naungaje mkono serikali ya watu viburi walioshupaza shingo wanaodhani ubabe unatatuwa matatizo ya dunia serikali ijihakiki na kujisahihisha ubabe unatuadhili sote so far no labda serikali nyingine yenye adabu na wananchi hii ya magumashi they can go to hell
 
napokupendeaga Pascal Mayalla ndio hapa yaani kwakweli unajua kucheza na BRO JIWE si kwamadongo haya unayompiga.. ni balllaaaa yaani akija kukuelewa unamaanisha mmmh bagosha!! onenee yangu misso
 
Takwwimu zinaonyesha waekezaji wameshuka kwa contrast ya asilimia 65% miaka miwili mbele tu tulikuwa tunaongoza wamekuja viongozi wenye phd za kukamulia ndimu kila kitu dubli dubli
 

Sasa wamaanisha serikali inafanya ubabe kwa Acacia?
 
Kwamba hatutoi suluhisho ?! Je kuna haja ya kuhangaika na makamishina kuwapereka mahakamani huku Mawaziri waliosaini mikataba wakiachwa ?!
Mbali na Lissu kuongea ushauri mwingine wa kitaalamu ambao mnatoa kwa Serikali kuhusiana na makinikia ni upi ? Ina maana leo tuwategemee Prof Osoro na Lissu peke yao ? Mbona mwenzenu Pascal Mayalla amejitahidi kutoa ushauri wa kitaalamu na ameonyesha uwezo wa kifikiri na kuchambua yeye peke yake kama msomi. Wewe hapo Odhiambo Cairo ushauri wako binafsi wa kitaalamu kuhusu Makinikia uko wapi ?

AU mpaka Lissu aandike kupitia Mwanahabari Huru ndiyo mpate cha kuchangia ?
Hebu tuache hizi siasa za matukio na tujaribu kuyatazama mambo katika mapana yake. Kama tunapinga basi tulete hoja nzito zenye utafiti wa kutosha na watu tuzione na tuzichambue kwa umakini.


Je nikuulize leo kuna kamishina anaweza akasaini mikataba na wawekezaji bila idhini ya boss ?! Hakuna.
Sasa hata mikataba ya acaccia ilikuwa mpaka boss wa wakati huo akubali. Hivyo kuwafanya watakatifu is not fair .
Tena kukusaidia tu, Mikataba mikubwa yote ni ya Raisi hawa makamishna wanaisaini kwa niaba ya Raisi (On behalf of) au kama Mashahidi tu (Witnesses). Halafu hakuna anayesema CCM ni wasafi, hebu acheni hii Sensationalism na Partisan Politics ambayo inawafunga akili msiweze kufikiri vizuri. Hapa hoja siyo Magufuli hapa hoja ni nchi.Huyu Raisi ni mpitaji tu ambaye anajaribu kurekebisha baadhi ya mambo sasa kuichukia nchi yako kisa mpitaji ni ukosaji wa uungwana.


Tatizo lenu kubwa ndiyo hili. Hamsomi viti vizuri, mnakurupuka, mnapenda kukosoa ila mkikosolewa mnapiga kelele kweli. Haya sasa wapi nimesema Tundu Lissu hafai, au umeamua kunilisha maneno ?

Leo anatuambia Gas na mafuta siyo yetu!!! Anamlaumu nani?! . Ukizingatia Kikwete alikuwa amebakiza miezi miwili tu. Kwa nini walimruhusu aliburuze bunge huku muda wake ukiwa umeisha ?!
.

Kuhusu swala la gesi na mafuta hawakulalamika CHADEMA tu, hata CCM walilamika kwa mambo mabovu ambayo Jakaya aliifanyia nchi. Hadi Mzee Malecela alisema gesi lazima iwanufaishe wana Mtwara kwanza. Siku ile vurugu ya Mtwara inatokea Jakaya alikuwepi Mtera Iringa, aliwatishia sana viongozi wa CCM ambao walikuwa wanataka gesi isitoke akisema "Lazima atawakata pembe". Mbona unataka kulifanya hili swala kama la mtu binafsi wakati ni swala la kitaifa ?

Tunamlalamikia nani leo ?! Lissu was right
Yes, Tundu Lissu was right. But even people like former Premier Malecela, Dr Slaa, Zitto Kabwe, Mtikila and Mkapa spoke viciously against The Gas Deal. Au unataka kusema huyo Lissu hajawahi kupotosha Umma kwa maksudi ?? AU Unataka nikupe na mifano hai kabisa
 
Takwwimu zinaonyesha waekezaji wameshuka kwa contrast ya asilimia 65% miaka miwili mbele tu tulikuwa tunaongoza wamekuja viongozi wenye phd za kukamulia ndimu kila kitu dubli dubli

NI kawaida hali hio kutokea pale unapowabana wale walokuwa wakifanya shughuli za uwekezaji bila kufuata taratibu na kuiba.

Hivyo hiyo asilimia 65 isikustue sana maana ni lazima taratibu za uwekezaji zifuate na kodi stahiki zilipwe.
 
Mtu alishasema hashauliki...yeye ni jiwe. Lissu kashauri umeona kilichompata.....
Huo uzalendo wako kaupeleke mbugani
Sensationalism over Objectivity:Hii ndiyo shida ya vijana wa kitanzania leo hii.
Magufuli anakosea sana tu na hataacha kukosea lakini hili haliondoi ukweli kwamba Barrick/Accaccia wezi
Hata angeingia Raisi kutoka upinzani huu wizi wa Barrick/Accaccia bado ungekuwepo tu.
NB: Tumia kichwa kufikiria na siyo kufugia nywele peke yake.
 
NI kawaida hali hio kutokea pale unapowabana wale walokuwa wakifanya shughuli za uwekezaji bila kufuata taratibu na kuiba.

Hivyo hiyo asilimia 65 isikustue sana maana ni lazima taratibu za uwekezaji zifuate na kodi stahiki zilipwe.
so unakubali kwamba ulikuwa unadanganya na takwimu zako sasa kubana bana kwa context ya human rights sio kutuletea sera za kirundi rundi unavunja katiba ya nchi hata ya kimataifa wamba mtuhumiwa si mfungwa wala mwenye mamlaka sio mahakama akifuata misingi ya haki za binadamu angegain kuliko anavyopoteza tatizo washauri zake akina makonda gambo na mnyeti ndio wanaona wamepatia
 
kuna uwezekano mkiubwa sana wa watu wa acacia kuendelea kukamatwa na kampuni itaondoka

Kama nao waliingia kwenye mtego huo hawatabaki salama watakamatwa tu.Ifike mahali watz tusitumike kama chambo na wazungu.watu wajifunze kuwa waaminifu na watiifu kwa nchi yao.mbona kwao hawafanti ujinga huo?
 

Nimekudanganya wapi na mimi nimekujibu kuhusu takwimu ulizoleta za asilimia 65?
 
Kama nao waliingia kwenye mtego huo hawatabaki salama watakamatwa tu.Ifike mahali watz tusitumike kama chambo na wazungu.watu wajifunze kujifunze kuwa waaminifu na watiifu kwa nchi yao.mbona kwao hawafanti ujinga huo?

Mimi nawashangaa sana baadhi ya watanzania humu JF ambao wanaoshi kwenye nchi ambazo hakuna upuuzi kama huu wanaofanya Acacia wa kuiba kwa miaka 10 mali ya nchi bila kudhibitiwa.

Nawashangaa sana.
 
Takwwimu zinaonyesha waekezaji wameshuka kwa contrast ya asilimia 65% miaka miwili mbele tu tulikuwa tunaongoza wamekuja viongozi wenye phd za kukamulia ndimu kila kitu dubli dubli
Mkuu lazima tujifunze kuwa wakweli.
Uwekezaji nchini umeshuka sana kwasababu kuna baadhi ya sera za Magufuli kuhusiana na uwekezaji ni mbovu sana. Tena kibaya zaidi ni kwamba zinawathiri hata wawekezaji wa ndani kwetu ambao hawana hata hatia yoyote. Kodi zimekuwa kubwa sana lakini mzunguko wa pesa ni mdogo sana...


Lakini mbali na haya yote, hawa wawekezaji wengi wa nje walikuwa wanapiga dili na viongozi wa CCM katika kuvuruga nchi. Mbona hili liko wazi sana ndugu yangu ? Au wewe unaamini kwamba hawa Accaccia/ Barrick walikuwa hawaibi kabisa na mikataba yao??
 
Sababu kuu hatuna wanasheria kwa hali ya sasa , tuna wale wa sawa mkuu. Hali ya nchi yetu ni mbaya sana tuendapo anajuwa Mungu baba tu sie wengine tuendelee kumuomba Mungu baba avifute hivi vikina ndio mzee vife kabisa pamoja na mzee wao wanayemuabudu na kumuogopa.
 

Mkuu Malcom

Nakutegemea sana hapa unyooshe baadhi ya vijana hapa maana tutakesha.

Ningependa ufafanue kidogo kuhusu hilo la baadhi ya sera za mheshimiwa raisi Magufuli kuwaathiri baadhi ya wawekezajikwamba wamaanisha masharti ya uwekezaji au taratibu.

Maana kuna kesi moja nchi fulani ughaibuni kuna wawekezaji walikuwa akipiga tu simu ubalozini na anapewa viza bila kufuata taratibu za uhakiki wa paperworks zao na wakati mwingine bila kupanga foleni.

Hapo unakuta yule balozi au kaimu analazimisha mtoa viza atoe tu bila kufuata taratibu za kufanya "checks".

Matokeo yake tunapata wawekezaji majambazi na watu wengine wa ajabuajabu.

Si vibaya ukifafanua hapo.
 

Mimi siyo mwanasheria wala mfanyabiashara, so please correct me if I am wrong.

Nilishawahi kuambiwa kuwa hakuna kipengele muhimu kwenye mikataba kama eneo linalozungumzia migogoro na hatua za kuvunja mkataba huo. Pande mbili au zaidi zinapoingia kwenye mkataba, na katikati ya muhula kukatokea tatizo, upande wowote unaweza kutoa lalamiko au kutaka kuvunja mkataba.

Hapo kipengele cha majadialiano, mapatano na usuluhishi (negotiation, mediation & arbitration) hutumika. Kama katika kipindi cha mkataba upande mmoja una ushahidi kuwa upande mwingine umedhulumu au kutekeleza uhalifu uliogusa makubaliano ya mkataba huo, wanayo fursa ya aidha kuvunja mkataba na kudai fidia au kusuluhisha kwa kudai fidia na kubadili mkataba. Mara nyingi hili huletwa kwenye meza ya majadiliano na mapatano (amicable resolution) kabla ya kufikishwa mahakama za usuluhishi.

Sasa, ikiwa sisi kama nchi tunao ushahidi kuwa Barrick/Acacia wamevunja makubaliano au kwenda kinyume na mkataba kwa kutakatisha fedha, kukwepa kodi na rushwa, kwa nini tusiutumie ushahidi huu katika majadiliano tukidai fidia? Au kama tumeshindwana mezani kwa nini tusichukue hatua nyingine katika mkataba ya kushitaki mahakamani ilhali ushahidi tunao?

Hata kama dunia inajua kuwa Barrick/Acacia wametuibia sana tatizo linakuja jinsi tunavyokabiliana na hili. We are setting precedence on any other contracts in the mining or extractive industries. Wawekezaji duniani wanaangalia au wataangalia mikataba yetu iliyotangulia na jinsi tumeikabili na maamuzi yao yatategemea na utekelezaji wetu. Sawa inawezekana kwa kukataa usuluhishi kwenye mahakama za kimataifa (international arbitration) tunawapa wakati mgumu Acacia kuuza hisa zao wakimbie, lakini pia tunajiumiza na sisi. Itakuwa vigumu sana kwa mwekezaji wa kimataifa kukubali kuingia mkataba na sisi ikiwa tumekataa international arbitration. Labda bidhaa iwe bei ya madafu kiasi kwamba wanauwezo wa kufyonza hasara yoyote watakayopata.

Kingine, mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi haiingiwi na mtu binafsi, ni serikali ndio inaingia mkataba kwa niaba ya nchi. Kama awamu ya kwanza waliingia mkataba na X, awamu ya pili inapoingia haiwezi kumwambia X kuwa "siutambui mkataba huu kwa kuwa ulisaini na flani wa awamu ya kwanza". Tutafeli sana tukifanya hivyo. Hayo ya nani alikosea tushikane humu humu ndani ya nchi bila kuathiri mikataba nje ya utaratibu wa mikataba hiyo.

Ila kama tunaamua kuyafukia madini hadi pale tutakapokuwa na uwezo wa kuyachimba na kuyafua wenyewe, basi tujiandae kwa hilo na lolote lijalo. Pasi na hayo, tunaweza kujiharibia kwenye uwekezaji wa nje.
 
Well said mkuu, hiki kinachofanyika na sirikali ni kufuel matatizo kuliko kupunguza. Mwenye nguvu mwite power! Tusitafute kiki au misifaaaa, tuone namna bora ya kuanza upya na kuvumu mikataba na katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…