Acacia yasema inautambua mkutano kati yake na Rais Magufuli

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, imesema imetambua mazungumzo yaliyofanyika kati ya Rais John Magufuli na Mkurugenzi Mtendaji wa Barrick Gold, John Thornton.

Acacia wamesema wanatambua uwepo wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Tanzania mapema leo kufuatia mkutano kati ya Rais wa Tanzania, Mh. Dk John P. Magufuli na John Thornton, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation.

Acacia wametoa taarifa hiyo leo, saa chache baada ya Rais kufanya mazungumzo na Mkurugenzi huyo wa Barrick.

“Tutatoa taarifa zaidi kadri itakavyofaa na kikao chetu kilichopangwa kufanyika kwa njia ya simu, Alhamisi tarehe 15 Juni saa tatu asubuhi muda wa Uingereza kitafanyika kama ilivyopangwa,” imesema taarifa ya Acacia.
 
Mazungumzo hayafanikiwa kama watabase kwenye ripoti zile mbili bila ya barick kujiridhisha.

Barick watafunga virago,hawana uwezo wa kulipa trilion 300 hata siku moja.

Na sisi ndo tushakodoa macho bila trilion 300 wafunge tu mgodi
 
Bado nao hawaeleki mbona hawakutuambia kama huyo rais anakuja au na pia ni kama sisi mambo ya kushtukizwa,wapi gordon
 
Kuna chama cha siasa na uchimbaji madini kinaomba ripoti ya Mruma...nawauliza hivi...kuna Mtaalamu wa miamba huko chadema?
 
..acacia hawakubaliani na matokeo ya ripoti za Prof.Mruma na Prof.Osoro.

..pia wamesema wamekuwa wakweli siku zote ktk kulipa kodi na mrahaba.

..kama msimamo wa acacia ni huo ni bora serikali ikataifisha mchanga na kuuza.

.. Baada ya hapo tutajua thamani halisi ya mchanga ktk soko na kiwango ambacho tumekuwa tukiibiwa.
 
Back
Top Bottom