Acacia yapunguza wafanyakazi tena

Acacia yapunguza wafanyakazi tena

wogakuria

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2018
Posts
743
Reaction score
1,224
Acacia yapunguza wafanyakazi tena
pic+acasia.jpg

Kwa ufupi
Hili ni punguzo la pili tangu Serikali ilipozuia usafirishaji wa makinikia Machi 2017.
By Samuel Tindwa, Mwananchi. stindwa@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, imepunguza wafanyakazi, kwa kile ilichokiita mabadiliko ya kiutawala.

Pia imetaja sababu nyingine za kupunguza wafanyakazi kuwa ni katika mpango wa kupunguza gharama wakati huu ambapo serikali imezuia usafirishwaji wa mchanga wa madini.

Hii ni mara ya pili kwa Acacia kupunguza wafanyakazi tangu Serikali ilipozuia usafirishaji wa makinikia.

Serikali ilizuia Acacia kusafirisha makinikia, Machi mwaka jana baada ya agizo la Rais John Magufuli kutaka kuhakikisha serikali inapata mapato ya kutosha katika shughuli za uchimbaji wa madini.

Zuio hilo ambalo mpaka sasa bado halijaondolewa, limesababisha mapato ya kampuni hiyo mwaka 2017 kupungua kwa asilimia 29 ukilinganisha na 2016.

Akizungumza na Mwananchi leo Septemba 5, Mkurugenzi wa Acacia, Assa Mwaipopo amesema tangazo la punguzo la wafanyakazi ni la kweli.

“Tangazo ni la kweli, ninashangaa tu umepataje habari hizo wakati liliwekwa kwa ajili ya watu wa ndani tu,” amesema.

Alipoulizwa kuhusu idadi ya wafanyakazi watakaopunguzwa, Mwaipopo hakutaka kufafanua.

Hata hivyo tangazo hilo limefafanua kuwa upunguzaji huo utafuata taratibu za sheria za kazi na majadiliano baina ya wafanyakazi na uongozi.
 
Sio lazima ichimbwe dhahabu. Wafanyakazi wakatafute kazi kwenye viwanda vingine vya extractive. Kuna watu wako wanachimba Limestones, Graphite hata mchanga. Yote hayo ni madini...
 
All in all watu wote walio kuwa kwenye Engineering field mgodini wame pata bonge la experience
 
Dar es Salaam. Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, imepunguza wafanyakazi, kwa kile ilichokiita mabadiliko ya kiutawala.

Pia imetaja sababu nyingine za kupunguza wafanyakazi kuwa ni katika mpango wa kupunguza gharama wakati huu ambapo serikali imezuia usafirishwaji wa mchanga wa madini.
Hii ni mara ya pili kwa Acacia kupunguza wafanyakazi tangu Serikali ilipozuia usafirishaji wa makinikia.

Serikali ilizuia Acacia kusafirisha makinikia, Machi mwaka jana baada ya agizo la Rais John Magufuli kutaka kuhakikisha serikali inapata mapato ya kutosha katika shughuli za uchimbaji wa madini.

Zuio hilo ambalo mpaka sasa bado halijaondolewa, limesababisha mapato ya kampuni hiyo mwaka 2017 kupungua kwa asilimia 29 ukilinganisha na 2016.

Akizungumza na Mwananchi leo Septemba 5, Mkurugenzi wa Acacia, Assa Mwaipopo amesema tangazo la punguzo la wafanyakazi ni la kweli.

“Tangazo ni la kweli, ninashangaa tu umepataje habari hizo wakati liliwekwa kwa ajili ya watu wa ndani tu,” amesema.

Alipoulizwa kuhusu idadi ya wafanyakazi watakaopunguzwa, Mwaipopo hakutaka kufafanua.
Hata hivyo tangazo hilo limefafanua kuwa upunguzaji huo utafuata taratibu za sheria za kazi na majadiliano baina ya wafanyakazi na uongozi.

Chanzo: Mwananchi
 
Hawa jamaa wako katika hatua ya mwisho ya kufunga shughuli zao hapa Tanzania wameshatupiga vya kutosha na wataendelea kutupiga hata wakiwa wameshaindoka. CCM na wabunge wake ndiyo wametuingiza chaka hili.
 
Sasa kwanini umeiweka tetesi ili hali habari ni ya kweli kwa mujibu wa maelezo?
 
Acacia yapunguza wafanyakazi tena
pic+acasia.jpg

Kwa ufupi
Hili ni punguzo la pili tangu Serikali ilipozuia usafirishaji wa makinikia Machi 2017.
By Samuel Tindwa, Mwananchi. stindwa@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, imepunguza wafanyakazi, kwa kile ilichokiita mabadiliko ya kiutawala.
Pia imetaja sababu nyingine za kupunguza wafanyakazi kuwa ni katika mpango wa kupunguza gharama wakati huu ambapo serikali imezuia usafirishwaji wa mchanga wa madini.
Hii ni mara ya pili kwa Acacia kupunguza wafanyakazi tangu Serikali ilipozuia usafirishaji wa makinikia.
Serikali ilizuia Acacia kusafirisha makinikia, Machi mwaka jana baada ya agizo la Rais John Magufuli kutaka kuhakikisha serikali inapata mapato ya kutosha katika shughuli za uchimbaji wa madini.
Zuio hilo ambalo mpaka sasa bado halijaondolewa, limesababisha mapato ya kampuni hiyo mwaka 2017 kupungua kwa asilimia 29 ukilinganisha na 2016.
Akizungumza na Mwananchi leo Septemba 5, Mkurugenzi wa Acacia, Assa Mwaipopo amesema tangazo la punguzo la wafanyakazi ni la kweli.
“Tangazo ni la kweli, ninashangaa tu umepataje habari hizo wakati liliwekwa kwa ajili ya watu wa ndani tu,” amesema.
Alipoulizwa kuhusu idadi ya wafanyakazi watakaopunguzwa, Mwaipopo hakutaka kufafanua.
Hata hivyo tangazo hilo limefafanua kuwa upunguzaji huo utafuata taratibu za sheria za kazi na majadiliano baina ya wafanyakazi na uongozi.

by Taboola
Sponsored Links

You May Like
Play this game for 1 minute and see why everyone is addictedDelta Wars

10 Most Intelligent Animals In The WorldThe-Best-Top
Kumbe bado katazo la kusafirisha makinikia linafanya kazi,vipi zile container za makinikia bado zipo bandarini au????
 
Back
Top Bottom