Acacia Options to Pay U$300m

aisee wazungu wanahangaika balaa!
kila siku press release!
Hii ni dalili ya mfa maji.
magufuli amewashika pabaya sana!
yule mkalimani nasikia aliwekwa kando wazungu wasijetambua walichokuwa wanaelezwa watanganyika !!
 
PM aliwahi kukurupuka na kusema eti kuna kampuni itajenga mtambo kuchenjua Chunya.....pale pale nikamdharau PM wetu ambae awamu hii ni kama hayupo anazidiwa nguvu....na RC mmoja na pia anazidiwa info toka juu na RC mmoja!!
 
Mara mgawano wa 50 fifty mara migodi inafungwa! Mara mitambo italetwa? Hivi hiyo dhahabu imebakia kiasi gani?
 
Nani kakwambia ugunguw hiyo thread?? Unaboa wewe unayewashwawashwa
 
Mkuu Chige, hii thread yangu, ilitokana na thread yako
Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa ...
kuna smelter ndogo za hadi ya tani 30 tuu kama ile ya Stillwater Mining ya nchini Marekani inayogharimu dola milioni 300 tuu!.

Paskali
 
chige nashukuru sana kwa ufafanuzi mkuu.
Tuliingia kwenye haya majadiliano tukiwa tayari tumeshaamua tunataka mwisho uweje hata kama hauna uhalisia.

Ndio maana mkubwa alipoambiwa mazungumzo mazito, akaendelea kulazimisha waendelee na haya ndio matokeo yake sasa.

Inabidi siasa, mihemko na ushabiki uwekwe pembeni. Utaratibu wa kupitia sheria na mikataba ya madini ifanykushirikisha wadau wenye sifa. Kama hatuwezi, bora hata tulipe pesa ya consultancy.
 
Pascal Mayalla hapo wamesema wanalipa ila kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa chini ya hiyo kampuni mpya na kuzingatia terms watakazokubaliana. Hapo kwenye hizo terms za ulipwaji wa hizo USD 300 M bado napo kuna kitendawili.
 
Pascal Mayalla hapo wamesema wanalipa ila kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa chini ya hiyo kampuni mpya na kuzingatia terms watakazokubaliana. Hapo kwenye hizo terms za ulipwaji wa hizo USD 300 M bado napo kuna kitendawili.
Mkuu Samaritan, lugha ni tatizo, ndio aana hata mtoa mada hii ameshindwa kutafsiri, walichosema ni kwanza wamekubali, lakini kwenye kulipa hizo milioni 300, they don't have the capacity to pay upfront, jamaa akasema ili hizo pesa zipatikane, kwanza ni lazima zile conteiners zitoke, ziuzwe, wadungulize ndipo walipe. Hivyo suala sio kulipa bali ni terms of payments na amounts, ila zitalipwa.

Tatizo langu hapa ni hawa jamaa tunawadai kutokana na kutuibia kwenye mchanga, sisi tumepiga mahesabu ya makisio ya tunachowadai, hesabu zimekuja ni trilioni 450. Acacia akatugomea kata kata kuwa hakuna kitu kama hicho. Baba mtu Barrick, kaingilia kati, tumekubali kukaa nao mezani kujadiliana. Jee msingi wa majadiliano ni nini?, nilidhani ni Add to dictionary kwanza kuhusu hizi trilioni 450, kisha tuzungumze namna ya kuthibitisha kuwa tulikuwa tunaibiwa kwa kuuchenjua mchanga uliopo, na tatu ni kuzuia kuibiwa kwa kuchenjua wenyewe, halafu haya mengine yote ni ziada.

Watu wamekaa siku 80, wametupa walichokubalia, hakuna hata hoja moja katika yale ya msingi, bali kubwa ni ahadi ya fedha za zawadi ya dola milioni 300 ambazo sii sehemu ya deni, wala deni halijazungumzwa chochote, hakuna chochote kuhusu uchenjuaji, wala kutaka kuthibitisha deni, wala kutambua tunaibiwaje.

Tafsiri yangu kuhusu hiki kishika uchumba ni hongo tuu kwa jina zuri la good faith, ili turuhusu mchanga uondoke, bila kujua kilichomo!.

Time will tell.

Paskali
 
Mkuu mchanga kuondoka kwa muda huu lazima uondoke. Kuhusu kuibiwa si kama ilivyokuwa kabla ya makubaliano na itakuwa kwa kupenda kwetu au kujiibia wenyewe. Sasa hivi kwenye mchanga wao chao ni dhahabu tu madini mengine ni yetu hivyo kujua yamo lazima tuyapime na tuyafuate huko wanakotoa dhahabu na sisi kutoa ya kwetu. Pia dhahabu ya ndani ya mchanga imo kwenye hesabu ya mgaona malipo mengine. Muhimu ni kuwapo kwa watanzania waaminifu wa kusimamia michakato yote. Kwenye muhutasari wa Prof Kabudi haya maelezo yamo je hukuyasikia? Au umeyasikia isipokuwa hujayatia maanani na kuona kama ni porojo tu. Ungeyatia maanani mashaka yako yangelenga humo.
 
aisee wazungu wanahangaika balaa!
kila siku press release!
Hii ni dalili ya mfa maji.
magufuli amewashika pabaya sana!
Acha kuweweseka soma kwanza
Mnatuumiza vichwa hatuwezi kupanga bajeti hivi .
Kutoka NOAH@ hadi m300$ sasa mnatuletea hii habari eti m125$ baada ya VAT
😕 😕 😕
 

 
Unanjaa kiasi hiki kumbe?
 
Acha kuweweseka soma kwanza
Mnatuumiza vichwa hatuwezi kupanga bajeti hivi .
Kutoka NOAH@ hadi m300$ sasa mnatuletea hii habari eti m125$ baada ya VAT
😕 😕 😕
 
Unanjaa kiasi hiki kumbe?

Ha ha haaaaa
Na wewe umefurahia kuniquote eeeh

Jione sasa unafikiria njaa kama vile unanifahamu.. fikiria utakavyo.. ukweli umepenya. Nipo hapa nasaga mawe nipike ugali kwa unga wake.

Mnasikitisha na msipobadilika mnalo.
 
Tooobaaa yaani tumeshushwa kutoka 450 trillion?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…