We Bondjamesbond unaishi kwenye sayari ya Mars?
Sio kweli kwamba Nyerere alikuja na unafiki. Nyerere alikuwa siriaz kabisa na kuamishia makao makuu Dom.
Suala la kusuasua kwa serikali kuhamia Dom limeandikwa na kuzungumzwa sana katika vyombo vya habari na bungeni. Kwa sasa hivi hiyo nia haipo kwa sababu za msingi japokuwa watawala hawako tayari kutamka wazi.
Kwa kifupi, nia ya kuhamishia makao makuu ya serikali Dom enzi za JKN ilifungamana na itikadi ya ujamaa (iliyolenga maendeleo vijijini kuliko mijini). Kumbuka itikadi ya ujamaa iliaga dunia na mwasisi wake na hivyo nia ya kuhamia Dom ikatoweka. Zama hizi tumekumbatia itikadi ya 'soko huria' (ubepari) ambayo msisitizo wake ni maendeleo mijini ikiwa ni pamoja na upanuzi wake (urbanization) na kwa mantiki hiyo Dar es Salaam naturally ime-retain hadhi yake ya awali na kuzidi kupanuka kama unavyoiona leo (idadi ya watu, shughuli, vikwanguaanga) japokuwa, kwa bahati mbaya, miundombinu iliyo mingi imebaki kuwa ileile ya enzi za ujamaa - chanzo, kwa mfano, cha msongamano wa magari, mafuriko ya maji machafu na ya mvua wakati wa masika, nk. Kwa hiyo ni suala la kiitikadi za siasa.