Aboud yaua waendesha pikipiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aboud yaua waendesha pikipiki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 5, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATU wawili wamekufa na wengine 49 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es Salam kwenda Morogoro kumgonga mwendesha pikipiki na kupinduka.
  Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa mbili asubuhi eneo la Tamco- Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani mwendesha pikipiki pamoja na abiria wake ambaye ni mtumishi wa halmashauri ya mji wa Kibaha walikufa papo hapo baada ya ajali hiyo.

  Ilidaiwa kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya pikipiki hiyo yenye namba za usajili T 616 BLF aina ya Sky Go iliyokuwa ikiendeshwa na Hamis Dadi kugongwa na basi hilo baada ya kukatisha kutoka barabara kuu kuelekea kwenye ofisi za halmashauri ya mji huo.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Absalom Mwakyoma alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa basi hilo lenye namba za usajili T 588 AYM lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda mkoani Morogoro lilisababisha ajali hiyo wakati likifanya harakati za kuikwepa pikipiki na hatimaye kuigonga kwa nyuma na kusababisha vifo vya dereva na abiria wake.

  Kamanda Mwakyoma alisema majeruhi wote 49 ambao ni abiria wa basi la Aboud walipelekwa katika hospitali ya Tumbi na wengine Muhimbili kwa matibabu ya haraka.

  Aidha alisema pikipiki hiyo ilikuwa imembeba abiria aliyetambuliwa kwa jina la Lucy Mageuza ambaye ni mtumishi wa Halmashauri katika Idara ya Ardhi aliyekuwa akielekea kazini.

  Naye ofisa uhusiano habari na mawasiliano wa Shirika la Elimu Kibaha Gerard Chami alisema kuwa majeruhi hao wanaendelea vizuri ambapo majeruhi watatu wamehamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

  Chami aliwataja majeruhi hao kuwa ni Shela Said (35) mkazi wa Morogoro, Songelaeli Shila (40) mkazi wa Kimara na Maina Kila (35).

  Aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Simon Nchimbi ambaye ni msaidizi wa katibu wa siasa na uenezi wa Kapteni John Chiligati, Rachel Sanga (14) mkazi wa Tabata Nasri Hamza (2) Kinyerezi,Jacline John (17) wa Kilosa.


  Wengine ni Cleopa Mbaga (33) ambaye ni mwanachuo wa chuo cha sokoine (SUA) mkoani Morogoro na Pili Enzi (30) wa Morogoro.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mi ni mtumiaji mzuri wa barabara ya dar-moro,hata jana nilikua safarini kutoka morogoro,kiukweli madereva wa abood huwa wanaenda rough mno,na kampuni hyo ndio inaongoza kwa ajali kwa kampuni zinazotoa huduma ya dar-moro,zipo kashfa nying ambazo mmiliki wa mabasi hayo alishawah kuzfanya,moja wapo ikiwa kuzika maiti kwenye kaburi moja,
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hizi ajari zitatumaliza! poleni sna wafiwa na mungu awapumzishe mahali pema peponi
   
 4. semmy samson

  semmy samson Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Oooooooooh My God Abood ameanza mwaka kwa mkosi...ila pia hizi pikipiki zinakera sana unakuta dereva pikipk hawana ujuzi, halaf ninyi abiria wa pikipiki muwe waangalif na maderva wa pikipik hata kama unaharaka we subir daladala kuliko pikpik maaana unaweza kuwahi mbinguni badala ya unakokwenda.....

  Wana JF tuwe makini Nawapenda sana...

  Pikipiki Hazifai:redfaces::embarrassed:
   
 5. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  wandesha pikipiki wengi ni wale wanaojifunza usiku then asubuhi wanaingia barabarani, wengi wao hawana lesen na wala hawajui sheria za barabarani, umakini unahitajika sana kwa sisi abiria ili kunusuru maisha yetu.
   
 6. M

  MathewMssw Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 7. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  madereva pikipiki ni wazembe kupindukia
   
Loading...