Musoma Yetu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2016
- 2,633
- 2,297
Namshukuru sana dereva kwa uzalendo huu anaouonyesha. Nimekupenda kuamua kuwa dereva mzalendo, na kuanza kuwaonyesha njia abiria wako, kuwa huu ni muda wa taifa kwanza ili abiria tufike salama. Lakini nashukuru pia, kwa upinzani kutengeneza barabara nzuri leo dereva kaamua kupita na wale wa ndiyooo!!! Imepita!! Nadhani ni muda mzuri wa wale wa ndiyo, kubadili fkra zao kwani dereva tayari kaonyesha njia. Na nyie wa hapana, endeleeni kufarahia, si dereva ameamua kupita kwenye njia zenu na ndiyo ilikuwa shauku ya siku nyingi kwenu? Hawezi akawambia amepita kwenye njia yenu waziwazi wakati mna macho na masikio mnasikia. Dereva nimekupenda, ni dereva usietaka kuangusha abiria wako na kuharibu tairi za magari yako wakati kuna barabara ilishatengenezwa na inaonekana ipo vizuri.