Abiria 54 watekwa na Meli ya Kijeshi Bahari ya Hindi na kutelekezwa Tanga

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Abiria 54 waliokuwa wakisafiri kwa mashua kutoka Shimoni, Mombasa nchini Kenya kuelekea Kisiwa cha Pemba wanadai kutelekezwa jijini Tanga baada ya kukamatwa na watu waliokuwa kwenye meli kubwa katika Bahari ya Hindi.

Abiria hao waliachwa nje ya jengo la Kikosi cha Majini cha Jeshi la Polisi (Polisi Marine) kilichopo jijini hapa, jana.
Wakizungumza na Mwananchi, walisema ‘walitekwa’ juzi na watu waliokuwa katika meli kubwa ya kijeshi ambayo ilikuwa na askari Waafrika na Wazungu.

“Baada ya kukamilisha ugongaji wa paspoti zetu za kusafiria tulianza safari katika Bandari ya Shimoni, Kenya kuelekea Wete Pemba, lakini wakati tukikaribia kufika Bandari ya Wete ilitufuata meli kubwa ya kijeshi na waliokuwamo melini humo walimwamuru nahodha ateremshe bendera na atii amri yao,” alisema Hamad Said Nassoro (37), mmoja wa abiria aliyekuwa katika mashua hiyo.

Alisema askari hao waliiamuru boti waliyokuwa wakisafiria kugeuza kuelekea Tanga kwa madai kwamba huko walikokuwa wanakwenda hakuna Serikali ni bora wapelekwe Tanga.

“Tukiwa na watoto wetu, tulipokaribia kufika Tanga meli ile kubwa ya kijeshi ilitia nanga na ikaja boti ndogo kutuchukua na kutuweka hapa nje ya Kituo cha Polisi Marine bila kutueleza kama ni wakosaji au vipi,” alilalamika Time Ramadhani Bakari (37).

Time alisema walifikishwa katika jengo hilo la polisi wa majini juzi saa saba mchana na hadi jana hawakuelezwa chochote.

“Hapa tulipo tumelala hapahapa na tuna njaa kali, watoto wanahangaika, tunaiomba Serikali iturejeshe kwetu Pemba kama inaona hatuna makosa na kama tuna makosa ni vyema tufunguliwe mashtaka kuliko tunavyofanyiwa,” alisema Habiba Salim (17).

Abiria hao walisema hawajui hasa kama meli ‘iliyowateka ni ya Tanzania au ya nchi gani kwa sababu ndani yake walikuwemo Waafrika na Wazungu.
Abiria hao walisema wao hufanya shughuli zao Mombasa na kila mwaka unapokaribia mwezi wa Ramadhani hurejea nyumbani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya ibada ya kufunga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe alisema jeshi hilo linafuatilia tukio hilo ili kujua waliowakamata watu hao na ni kwa sababu zipi.

“Niseme tu kwamba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola tunafuatilia suala hili ili kujua kama ukamatwaji wao ulikuwaje na nani walihusika kuwakamata, kisha nitatolea maelezo lakini kwa sasa subirini kwanza,” Kamanda Bukombe aliwaambia wanahabari jana.

Mpaka jana jioni abiria hao walikuwa katika kituo hicho cha polisi wakiwa hawajui iwapo watasafirishwa kurudi Pemba au la. Pia walilalamika kukosa chakula tangu siku waliyotekwa na kwamba, hali za watoto ni mbaya.


Chanzo: Mwananchi
 
Jumuiya ya East Africa ipo tanzania bara tuu zanzibar hampo.Kutoka kenya kwenda zanzibar ni sawa na kwenda urusi.Ndio maana hata bidhaa zenu haziruhusiwi bara
 
kulikuwa hakuna mwenye smartphone ata akapiga kapicha cha uwizi uwizi tuitambue hio meli.
au aliekuwa anatafutwa hakusafiri siku hio
 
Walikuwa wanaongea lugha gani? Je hao askari waliokuwa kwenye meli ya kijeshi ni wa nchi gani Tanzania au nchi tofauti?

Mtoa Maelezo hakuweka bayana aisee!! Haiwezekani mkamatwe bila sababu inawezekana walikuwa na mizigo ya magendo wamebeba.
 
hivi ina maana bahari yetu haina ulinzi mpaka meli za kijeshi za nchi nyingine zinatamba namna hiyo nilitegemea wizara ya ulinzi italitolea ufafanuzi jambo hilo
 
Maigizo Tz hayamalizi, sasa mpaka wanapelekwa hapo kituo cha marine huyo alowapeleka ni mtu asiyejulikana? Wapemba huu mwaka wao Lakini Mwenyezi Mungu atatuvusha salama.
 
Meli ya kijeshi/yoyote haiwezi kuingia Tanzanian waters bila marine/navy control kutambua, eti mpaka ikatia nanga wakapelekwa na boti ndogo wakaachwa polisi. Hao watekaji wanajulikana na meli yao inajulikana, jeshi la maji watakuwa wanafahamu kila kitu na maelekezo ya kuwapeleka pale lazima walishirikiana na Navy, hawa si watekaji, yawezekana ni operation ambayo imebuma na the only solution ni kuwarudisha. Msitegemee taarifa yoyote ya ziada kuhusu, itaisha kimya kimya, huko Pemba mh! kuna jambo na tena si dogo!..hao washakuwa intercepted to disrupt something..update mtapata labda mwezi ujao!
 
Wanajeshi maji wanafanya kazi gani huko jamani, km mambo yenyewe hivi tunaweza kutekwa kijinga sana haiji akilini meri ya watekaji ije kwenye himaya yetu pasipo kufahamu. Poor jeshi maji na polisi maji. Shame on you all!
 
Back
Top Bottom