Abdulwahid Sykes kutoka Burma, Dockworkers Union hadi TANU

Hawatajwi? Mbona wewe umewataja?

Kwa taarifa yako kuna mashujaa wa ukweli (unsung heroes) hata wasiofahamika. Nadhani unajua msemo wa Avumae Papa Baharini. Kwahio cha maana kila anayejua / anayemfahamu shujaa wake sio vibaya akamtaja, otherwise tutahitaji robo tatu ya historia ikitaja watu (ambayo sio mbaya) ila in summary nadhani matokeo ni muhimu zaidi na kutajana iwe subset
 
Hawatajwi ?, Mbona wewe umewataja ?

Kwa taarifa yako kuna mashujaa wa ukweli (unsung heroes) hata wasiofahamika...., Nadhani unajua msemo wa Avumae Papa Baharini.... Kwahio cha maana kila anayejua / anayemfahamu shujaa wake sio vibaya akamtaja, otherwise tutahitaji robo tatu ya historia ikitaja watu (ambayo sio mbaya) ila in summary nadhani matokeo ni muhimu zaidi na kutajana iwe subset
Key...
Kwangu mimi imesadifu kuwa wazee wangu ndiyo mashujaa wa wote kwa kuwa walipigania uhuru wa Tanganyika.

Hii ndiyo sababu kuu ya mimi kuandika historia yao ambayo haikuwa imehifadhiwa.

Ninao wajomba zangu na baba zangu ambao katika siku zilizopita hapa mjini Dar es Salaam walivuma kwa sifa kadhaa kama kucheza Gossage Cup na kukichukua kikombe.

Ninao ambao walikuwa hodari katika muziki na rekodi zao za santuri zilirekodiwa na Hugh Tracey, Mzungu kutoka Rhodesia zikatolewa santuri na Gallotone Johannesburg.

Lakini hawa hawakunivutia kama hawa waliounda AA 1929, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika1933, Dockworkers Union 1948, TANU 1954 na Tanganyika Railways African Union.

Hata hivyo hii haiwakatazi wengine kuandika vitabu vya mashujaa wao.
Mimi nina jumla ya vitabu 10 nimeandika hadi sasa vya historia ya hawa wazee wangu.

Wengine nimeweza kuwatia katika Dictionary of African Biography (DAB), Oxford Univeristy Pressm New York (2011) (Volume 6) na yote haya ni yenye faida kwetu kama taifa na kwa vizazi vijavyo.

1622122969378.png

Hiyo picha ni Gossage Team Winners 1949 kuna wazee wangu watatu katika timu hiyo.

1622123072421.png

Salum Abdallah huyu ni babu yangu muasisi wa TANU Tabora, Western Province 1954 na Rais Muasisi wa TRAU 1955 ana historia kubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Vipi nitaacha kuandika historia ya hawa wazalendo?
 
Mpaka tunyooke tumuelewe sykes 😂😂😂

Ova
Mrangi,
Ukifanikiwa kumfuta Abdul Sykes katika historia ya TANU unakuwa umefanikiwa kufuta historia yote ya harakati za kupigania uhuru kuanzia 1929 na kupita 1961 baada ya uhuru.

Huwezi kumleta Julius Nyerere, Hamza Mwpachu na Chief Kidaha Makwaia katika harakati ikiwa hunae Abdul Sykes.

Hutoweza hata kumleta baba yake Kleist Sykes kama huna Abdul Sykes.

Hutoweza kuwaleta watu mashuhuri wa Dar es Salaam kama Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, Bantu Group kwa kuwataja wachache ikiwa huna Abdul Sykes.

Hutoweza kujua mchango wa Earle Seaton katika uhuru wa Tanganyika ikiwa umemtambuka Abdul Sykes.

Ndiyo maana nilipoandika historia ya maisha yake hata historia ya Nyerere ikabadilika pakubwa mno.

Watu wengi walishtushwa na yale waliyosoma ndani ya kitabu.

Chuo Cha CCM Kivukoni walijaribu wakidhani wanaweza kufuta historia nzima ya jamii ambayo ina watoto walioona na waliosikia ya wazee wao.

Ndiyo hii leo zaidi ya miaka 20 toka kitabu kitoke mjadala haujasimama na kila baada ya miaka 4 kitabu kinachapwa upya.
 
Key...
Kwangu mimi imesadifu kuwa wazee wangu ndiyo mashujaa wa wote kwa kuwa walipigania uhuru wa Tanganyika.
Hii ndiyo sababu kuu ya mimi kuandika historia yao ambayo haikuwa imehifadhiwa.
Naam na mimi nikakukumbusha kwamba avumae Papa Baharini kumbe na wengine wapo..., kwahio huenda wazee wako wana bahati wamepata msemaji wewe (kuna wengine ambao walipigania uhuru hawana msemaje) kwahio huenda hawa wote sio kwamba kwa sababu ya Chuki bali ndio the way of the world Tunaposema Mfalme fulani alishinda vita sio kwamba yeye ndio alipiga maadui wote na kuwamaliza (huenda hata hakugusa jambia wala bunduki)...

Hivyo basi ni wajibu wa kila mwanahistoria (anayejua jambo ) kuliweka sawa vile alijuavyo kwa ku-balance pande zote bila kuweka chumvi /biassness (sababu huenda hata hizo sinema za Vietnam Wars zingetengenzwa Hanoi na sio Hollywood) huenda zingekuwa na mtizamo tofauti.

Tatizo walilo nalo wengi kwako unaonekana kwamba una biasness katika maandiko yako..., jambo ambalo ni la kusikitisha sababu kama uliweza kuongea na wengi wa wahusika ungekuwa hauko Bias ungeacha rasilimali ya maana sana, Yaani yote uliyokuwa unaambiwa na wazee wako ungeweza kuyachuja na kuuliza huko na kule critically kuhakikisha kwamba haujalishwa matango pori (after all hawa wazee wetu sometimes kwa wajukuu / watoto wao wanaweza pindisha ukweli)

Tunahitaji mashujaa wengi zaidi (ili wawe role models wa watu wetu) sio kwamba tukiongeza wengine wengine watapungua bali tusishushe mashujaa wengine ili tuwakuze wengine wote wana nafasi katika taifa...
 
Key,
Nakuhurumia kidogo.

Wewe ndiyo leo unaingia katika mjadala huu.

Hujui kuwa mjadala huu hapa uko zaidi ya miaka 10 na unarudia hoja na kuuliza maswali ambayo wenzio wameniuliza na nimewajibu miaka 10 iliyopita.

Kubwa ni kuwa wazee wangu walifutwa katika historia na kukawa na historia ambayo siyo.

Sasa mimi nimeandika historia ya wazee wangu na halazimishwi mtu kuniamini anaweza akabaki na historia ya Chuo Cha CCM Kivukoni.

Ajabu niionayo ni pale anapokuja mtu kutaka ati anifunze namna ya kuandika historia ambayo yeye haijui.

Kama wapo mashujaa mnaowajua ambao mimi sijawaeleza michango yao andikeni historia zao kama nilivyofanya mimi.

Kwani mlikuwa mnajua kuwa Nyerere alitiwa katika uongozi wa TAA mwaka 1953 na Abdul Sykes?

Mimi si ndiye niliyekuelezeni na nikakutajieni hata kadi yake ya TANU kuwa ni no 3 no. 2 ya mdogo wake Ally na no. 7 mdogo wake wa mwisho Abbas?

Andikeni historia za mashujaa wengine waliosahaulika.
 
Back
Top Bottom