Abdulrahman Kinana: Who is he?

Abdulrahman Kinana: Who is he?

Kinana ana husika na mradi wa kuwapatia uraia wa Tanzania wakimbizi wote wa kisomali walioko Chogo mkoani Tanga.Wakimbizi wa Kikongo,Burundi na Rwanda walikataliwa na kulazimishwa kurejeshwa makwao.

mkuu siunajua zimwi likujualo.......
 
14.JPG


Abdulrahman Kinana amekuwa kama Mwanasiasa wa kutegemewa sana katika duru za siasa za CCM.

Katika vipindi tofauti vya miaka ya Uchaguzi amekuwa akipewa kazi ya kuwa Campaign Manager wa CCM. Kazi hii mara nyingi inahitaji uratibu wa hali ya juu na kubuni mikakati makini itakayopelekea ushindi kwa chama husika.

uwt-dar-2.jpg


Lakini karibu katika chaguzi 3 au 4 ambazo yeye amekuwa Manager, sijaona akipewa cheo fulani Serikalini baada ya Ushindi. Hili pia ni suala la kujiuliza ni kwa nini hapewi? Hana uwezo au hataki?

xx95.jpg


Kwa lugha ya vijana wa mjini Kinana amekuwa kama ni MASTER MIND wa CCM na hivyo katika Siasa za Tanzania.

NECKikao.jpg


Katika kampeni zinazoendelea sasa hivi Kinana amekuwa Campaign Manager pia, na amekuwa mara kwa mara akitoa maelezo mbele ya vyombo vya habari huku akionekana ni mtu mwenye kujiamini kupitiliza na ambaye hana papara za aina yoyote . . . . hii imenifanya niwe curious kidogo kutaka kujua kwa undani . . . . Abdulrahman Kinana Ni Nani Hasa?

sefunajk.jpg


Wenye details za historia yake na nini anafanya na role yake katika siasa za CCM ni nini tunaomba watujuze.

images


Naomba Kuwakilisha!
 
Abdulrahman Kinana amekuwa kama Mwanasiasa wa kutegemewa sana katika duru za siasa za CCM.

Katika vipindi tofauti vya miaka ya Uchaguzi amekuwa akipewa kazi ya kuwa Campaign Manager wa CCM. Kazi hii mara nyingi inahitaji uratibu wa hali ya juu na kubuni mikakati makini itakayopelekea ushindi kwa chama husika.

Lakini karibu katika chaguzi 3 au 4 ambazo yeye amekuwa Manager, sijaona akipewa cheo fulani Serikalini baada ya Ushindi. Hili pia ni suala la kujiuliza ni kwa nini hapewi? Hana uwezo au hataki?

Kwa lugha ya vijana wa mjini Kinana amekuwa kama ni MASTER MIND wa CCM na hivyo katika Siasa za Tanzania.

Katika kampeni zinazoendelea sasa hivi Kinana amekuwa Campaign Manager pia, na amekuwa mara kwa mara akitoa maelezo mbele ya vyombo vya habari huku akionekana ni mtu mwenye kujiamini kupitiliza na ambaye hana papara na lolote . . . . hii imenifanya niwe curious kidogo kutaka kujua kwa undani . . . . Abdulrahman Kinana Ni Nani Hasa?

Wenye details za historia yake na nini anafanya na role yake katika siasa za CCM ni nini tunaomba watujuze.

Naomba Kuwakilisha!
Those are qualities of soldiers who can cross mount Everest with only a knife and piece of bread!! Sijui mengine, ila kama kweli anajiamini na ametulia, ndio maana amepewa kazi ya kuwa craft man wa siasa za uchaguzi
 
Those are qualities of soldiers who can cross mount Everest with only a knife and piece of bread!! Sijui mengine, ila kama kweli anajiamini na ametulia, ndio maana amepewa kazi ya kuwa craft man wa siasa za uchaguzi

Mmmh! Yawezekana ikawa ni hivyo tu?

Na historia yake ya U-Soldier ikoje?
 
Kwa ufupi alikuwa na nafasi za juu Serikalini enzi hizo mpaka watu walipoanza kumzushia mambo ya uraia, ndipo hapo akapotea kwenye medani ya siasa za uongozi na kuibuka akiwa anatumika tu kwenye chaguzi!
 
Huyu jamaa amekuwa mkimya kupita kiasi.Hivi alivyogombea ubunge Arusha Mjini alishinda au alishindwa? na Hivi alisomaga nini Harvard?
 
Very Interesting . . . . nimeikuta hii hapa:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/12529-abdul-rahman-kinana.html

Ingawa haijibu kiu ya kupata details zaidi . . . .

Wanomuelewa mh KINANA wanasema kwa kweli ile ndio machine iliyobaki kwenye CCM.

Yeye ndio master mind wa mipango mengi ndani ya Chama na ndio maana Ujumbe wake ndani ya CC na NEC ni wa bila kupata upinzani.

Kwenye Serikali Hii ya Mafisadi yeye ni mshauri wa Mipango mingi hususani ile ya inayohusu masuala ya Kiprotocol na Usalama , wanasema yeye ni INT wa nguvu sana.

Inaelezwa pia kwa kipindi kirefu sasa amekuwa ni MJUMBE MUALIKWA wa BARAZA la mawaziri. Kwa sasa inaonekana ni kama muhimili wa mambo fulani ndani ya chama na serikali.

ULAJI wake anaupata zaidi kwenye biashara zake na ni mjumbe wa BODI nyingi tuuuuu.

Kumbuka kuwa anapata STAHIKI kama za mawaziri baadhi ya wakati.

Jamaaa inasemekana si mtu wa KUKURUPUKA na mipango yake mingi huenda na kukamilika kwa UFANISI zaidi.
 
This was 2008 - And still 2010 Kinana is still a "Subject Matter"!
 
He is very professional ... katika utendaji wake wa kazi! Nilibahatika kufanya nae kazi sehemu fulani, na nili-appreciate kichwa chake!

Yeye ni mwanachama mwenye heshima sana ndani ya CCM, na mara nyingi hutumiwa kusuluhisha mipasuko ndani ya chama (Mbeya alishafika!).

Kwenye biashara, kila unapomkuta Sir Andy Chande basi nae Kinana yupo! hawa ni washikaji sana kibiashara, na mara nyingi wako kwenye Bodi za serikali pamoja!

Eeeh, what a lethal combination! A real soldier and a real business man who can anything at his disposal!!!!!
 
Ukiona kimya hivyo, basi jua ni smart kama watu wanavyosema. Haachi finger wala foot prints sehemu yoyote anayogusa au kukanyaga. Naamini kabisa ni mtu mwenye kutumia akili na master wa soft skills. Vinginevyo asingeweza kupewa kazi ya kushikana mikono na kila mtu ili chama kipate ushindi.

Yeye ni askari wa aina yake. Wengi wakifika rank kama yake jeshini arrogance inatangua hatua kadhaa mbele yao wanapoteza mvuto.

I like those sort of qualities the guy has developed, ukiachilia ya ufanya biashara na yule mfanyabiashara maarufu TZ.
 
Du hii nayo kutoka hapa:

https://www.jamiiforums.com/habari-...-lakini-shehena-la-meno-ya-tembo-silijui.html

Kinana acharuka, asema ametumika kama pilipili kwenye kachumbari !! - Tanzania Daima.

KADA maarufu na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema hahusiki na usafirishaji wa meno ya tembo nje ya nchi, ikiwa ni siku moja tu tangu gazeti moja la wiki, lichapishe habari iliyomuelezea kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyosafirisha meno hayo.

Hata hivyo, kada huyo amekiri kuwa mmiliki wa Kampuni ya uwakala wa meli ya Sharaf Shipping Agency, iliyohusika kusafirisha makontena yaliyokuwa na nyara hizo za serikali, kabla ya kukamatwa nchini China yakiwa safarini kupelekekwa Hong Kong.

Gazeti hilo lilimtaja Kinana kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kwa kuwa na hisa 7,500 kati ya 10,000 katika kampuni hiyo, huku hisa nyingine 2,500 zikiwa zinamilikiwa na mshirika mwenzake, Rahma Hussein. Thamani ya hisa hizo ni sh 1,000 kila moja.

Kinana alitoa ufafanuzi huo katika mahojiano maalum na Tanzania Daima.

"Nimeisoma habari hiyo na kwa bahati mbaya sioni anayenilaumu wala kitu ninacholaumiwa nacho. Kwamba nina hisa katika kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf ni kweli.

"Lakini mimi sina nafasi yoyote ya kiutendaji na wala sishughuliki na uendeshaji wa kampuni hiyo. Kwa kweli sikujua na wala sikuhusika kwa namna yoyote ile na usafirishaji wa makontena hayo na mengine yoyote," alisema Kinana.

Alisema anachojua yeye ni kwamba, maofisa wa kampuni hiyo waliuliza na kuambiwa kuwa shehena iliyokuwa katika makontena hayo ni plastiki zilizotumika.

Alifafanua kuwa, wenye wajibu na mamlaka ya kukagua shehena zote zinazosafirishwa nje ya nchi ni mamlaka za serikali na si kampuni ya uwakala wa meli.

Alisisitiza kuwa, hana mamlaka kwa mujibu wa sheria kukagua mali inayosafirishwa japokuwa anaweza kuuliza bidhaa iliyopo katika makontena hayo.

"Ni dhahiri kabisa kwamba, habari hii imeandikwa na jina langu kutumika katika malengo ambayo siyajui. Nahisi kama jina langu limetumika kama pilipili katika kachumbari ili kunogesha habari.

"Kwa bahati mbaya pilipili imezidi katika kachumbari. Kama lengo lilikuwa kupasha habari, basi umma umedanganywa," alisema Kinana.

Kwa mujibu wa habari hiyo, sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali liliibuliwa kwa mara ya kwanza na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, katika Bunge lililopita la bajeti.

Ilidaiwa kuwa, nyaraka hizo zilionyesha kuwa, kilichokuwa ndani ya makontena hayo ni plastiki zilizodurufishwa na baada ya ukaguzi kufanyika, iligundulika kuwa, kilichokuwemo ni pembe za ndovu.

Habari ya gazeti hilo hata hivyo, ilimnukuu ofisa mwandamizi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, akieleza wazi kuwa kazi ya kukagua kilichomo kwenye kontena linalosafirishwa si ya wakala wa meli kwani, wenye mamlaka na idhini ya kufanya hivyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2009/2010, Kilango alisema utafiti wake umeonyesha kuwa, makontena hayo yalipitia bandari ya Dar es Salaam na nyaraka zinaonyesha ndani kulikuwa na plastiki.

Kilango alisema nchi zinazoongoza kwa kupokea nyara kutoka Tanzania ni Philipines, China, Singapore na Hong Kong.

Kaaaaaazi kweli kweli !
 
Ukiona kimya hivyo,basi jua ni smart kama watu wanavyosema. Haachi finger wala foot prints sehemu yoyote anayogusa au kukanyaga. Naamini kabisa ni mtu mwenye kutumia akili na master wa soft skills. Vinginevyo asingeweza kupewa kazi ya kushikana mikono na kila mtu ili chama kipate ushindi. Yeye ni askari wa aina yake.Wengi wakifika rank kama yake jeshini arrogance inatangua hatua kadhaa mbele yao wanapoteza mvuto.

I like those sort of qualities the guy has developed, ukiachilia ya ufanya biashara na yule mfanyabiashara maarufu TZ.

Unafahamu chochote kuhusu historia yake Jeshini? Nadhani ni Kanali Mstaafu!
 
Abdul Rahman Kinana is king maker,CCM logic board, smart shroud, the guy who can square angles and sharpen corners ,a soldier of fortune. In short is an invisible man behind the scene, Emergency backup and rescue Spiderman cum Superman every time CCM send SOS (save our souls).
 
KINANA A.K.A mfanyabiashara haramu za nyara za Taifa
 
Hivi huyu bwana ana cheo gani katika timu ya kampeni ya CCM ya sasa?
 
Anakumbukwa zaidi kwa "usimamizi" wa kura za CCM. Hii ni kazi ambayo mwanzoni ilifanywa zaidi na Malecela na baadaye Kinana akajifunza kwake namna ya "kusimamia" hizo kura. Hata huko kupewa Uspika wa Bunge la Afrika Mashariki mie nadhani ilikuwa shukrani kwa "usimamizi mzuri wa kura" hapo nyuma.

Na wakati huu naona hawataweza kumtegemea Malecela. "Kazi" itasimamiwa na Kinana tena.
 
Back
Top Bottom