Abdulrahaman kinana na Nape Nmauye ndani ya ifakara.

Abdulrahaman kinana na Nape Nmauye ndani ya ifakara.

Ziroseventytwo

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
9,447
Reaction score
17,928
Katibu mkuu wa ccm ndg Abrahamani kinana na katibu mwenezi Nape Nnauye wapo hapa ifakara kwenye viwanja vya makari stend. Mkutano wao unarushwa live na radio Pambazuko fm. Wapo hapa wakitokea wilayani ulanga, baada ya kukutana na zomea zomea kwenye mji mdogo pale ruaha juzi. Watu ni wachache sana, wanawake ni % kubwa... Kwa sasa anazungumza Nape...
 
kagueni gari zote za msafara wake kuhakikisha hakuna meno ya tembo kutoka katika maeneo ya Mofu,Kibaoni,Idete,Chita,Udzungwa, na mapori ya huko karibu hata na Selous.Kinana hakubaliki, LINDA TEMBO WETU KWA VIZAZI VYETU
 
Kinana anakaribishwa sasa, na mwenyekiti wa ccm mkoa...kidumu chama cha mapinduziiiii!. Anapayuka kinana! Kuna wanachama 162 wapya wa ccm, wanawakilishwa na wenzao 12 kuchukua kadi...mkutano unaendelea. Kiukweli mkutano umepooza sana.
 
kagueni gari zote za msafara wake kuhakikisha hakuna meno ya tembo kutoka katika maeneo ya Mofu,Kibaoni,Idete,Chita,Udzungwa, na mapori ya huko karibu hata na Selous.Kinana hakubaliki, LINDA TEMBO WETU KWA VIZAZI VYETU

hahahahahah mkuu umeuwa hh!
 
Wembe uleule wakiongea pumba piga mawe majangiri hayo
 
kazi ya kurikoti live inawenyewe jamani! wasikose kupitia kwa bibi kalembwani!
 
Akiongea na radio pambazuko, Nape Nnauye amewataka watu wa kilombero hususani wakazi wa ifakara kuendelea kuiunga mkono ccm, kwani inatekeleza ahadi walizotoa mwaka 2010, kwani daraja la mto k'mbero ilikuwa 1 ya ahadi ya rais kikwete. Daraja tayari limeanza ujenzi wa awali.Mkutano umemalizika na hamna cha maana zaidi ya propaganda za kukichafua CDM.
 
ww muongo bhana. Wanatokea ulanga mara jana ruaha. wapi na wapi
 
Yaliyotokea Ifakara jana jioni yamenishangaza baada ya hotuba ya Kinana kwenye mkutano wa hadhara, wananchi wengi sana walokuwa na kadi za Chadema na kidogo Cuf walikuwa wanarusha hovyo kadi hizo na kushinikiza kupewa za CCM.

Picha naleta soon
 
Siasa za majukwaani zinategemea zaidi jinsi mtu alivyoamka siku hiyo. Cha ajabu na chama kingine kikifika hapo baada ya siku chache mambo kama hayo yatatokea. Tuwekee picha tukusaidie kuamini!
 
Siasa za majukwaani zinategemea zaidi jinsi mtu alivyoamka siku hiyo. Cha ajabu na chama kingine kikifika hapo baada ya siku chache mambo kama hayo yatatokea. Tuwekee picha tukusaidie kuamini!

Hana haja ya picha mie nimehudhuria mkutsno kidogo niwatukane makafiri hawa, eti wanatupa kadi za chama changu hadharani,sijui wamerogwa nini na magamba...nyambafu zao
 
Nadhani si bure magamba wamewaroga watu hawa, maana walikuwa wanakimbia kurudisha kadi za CDM kama vile zinawasumbua mikononi mwao....
 
Hana haja ya picha mie nimehudhuria mkutsno kidogo niwatukane makafiri hawa, eti wanatupa kadi za chama changu hadharani,sijui wamerogwa nini na magamba...nyambafu zao

Mbona tumemwona yule dogo ambaye wamempa laki tano na kupiga nae picha na bendera ya chadema huku Kinana akitabasamu kama zuzu!
 
Back
Top Bottom