Abdallah Bulembo: Sitogombea tena Uenyekiti Jumuiya ya Wazazi CCM

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Mwenyekiti Wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo, ametangaza kuwa hatagomea tena nafasi hiyo katika uchaguzi ujao,Kauli hiyo ameitoa Mkoani Dodoma Muda Mfupi uliopita.

=====

Dodoma. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo amesema hatogombea tena nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo.

Bulembo ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi) katika kikao cha baraza hilo mjini Dodoma na kutumia fursa hiyo kuwaaga wajumbe hao na kusema kuwa hoja siyo ubunge alioteuliwa bali ni utamaduni wake aliojiwekea katika maisha yake.

"Hoja hapa siyo ubunge kwamba nitakuwa nakofia mbili huu ni utaratibu wangu niliojiwekea katika maisha siwezi kung'ang'ania madaraka. Nilifanya hivi nilipokuwa naibu Meya Musoma na nilipokuwa kiongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Nchini (TFF), " amesema.

Kutoka na uamuzi huo Bulembo amewaonya wajumbe wenye lengo la kuchukua fomu ili kumrithi kutomfuata wala kumpigia simu awasaidie badala yake amewataka wafuate utaratibu wa jumuiya hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Haya baharia mwenzangu wa nchi kavu William Malecela shavu hilo, ukikosa na hii basi tena, acha tu siasa.
 
Haya baharia mwenzangu wa nchi kavu William Malecela shavu hilo, ukikosa na hii basi tena, acha tu siasa.
Mkuu naona ccm itakuwa inajichimbia handaki yenyewe kwa kupitisha jina LA mtoto kwenda kuongoza jumuiya ya wazazi.hivyo viatu ni vikubwa sana.abaki tu kitengo cha propaganda mitandaoni kwakwe hiyo shughuli anaimudu.
 
Mambo yamebadilika , na elimu yake hiyo ya memkwa hata ujumbe wa nyumba hamsini hapati.
 
Magufuli alishasema Baadhi ya Reforms za Chama Ni Kuwa weka Vijana wasomi kuanzia ngazi ya Kata mpaka Taifa.
 
Back
Top Bottom