Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,346
- 9,881
Nimekuwa nikimsikia Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi wa ccm Abdallah Bulembo akitoa kauli zenye ukakasi mara nyingi, lakini kauli aliyoitoa juzi inabidi ilaaniwe kwa nguvu zote, na zaidi ifikishwe icc kama kielelezo cha kuchochea uvunjifu wa amani. Amesema ccm inaweza ikafanya mambo yote lakini haiwezi kuikabidhi ukawa ikulu!! Kwanza yeye ni nani kwenye Tanzania hii mpaka atoe kauli kama ile? Na je anachozungumza ni kauli yake binafsi au ni kauli ya chama baada ya maamuzi ya vikao? Tukumbuke kauli kama hizi ndizo zilizoitumbukiza Ivory Coast katika machafuko makubwa baada ya uchaguzi nchini humo miaka kadhaa iliyopita. Mke wa rais na baadhi ya viongozi waandamizi wa nchi hiyo walikuwa wanatoa kauli kuwa rais wa wakati huo hayupo tayari kukabidhi ikulu kwa wapinzani. Sasa hivi wapo jela wakitumikia vifungo vyao kwa kuchochea machafuko. Kitu kingine nashangaa NEC wapo kimya kabisa, hawajatoa onyo wala karipio kwa kauli ya kichochezi iliyotolewa na kiongozi huyo wa ccm. Naomba viongozi wa ukawa wawe wanakusanya vielelezo hivi na kuvihifadhi ili vije vitumike kuwashitaki wale wote watakaoiingiza nchi katika machafuko kama anavyofanya huyu Abdallah Bulembo. Najua icc nao wapo nchini, wafatilie kauli za huyu mwana ccm.