Abbas Tarimba,diwani wa kata ya Hananasif anavyo wapumbaza raia wake!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abbas Tarimba,diwani wa kata ya Hananasif anavyo wapumbaza raia wake!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchajikobe, Mar 30, 2010.

 1. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Habari za saa hizi wakulu,,hapa kuna jambo ambalo nimeona bora niliweke ili liweze julikana na kupatiwa ufumbuzi kama kuna uwezekano,Diwani wa kata ya Hananasif Mh.Abbas Tarimba(former president of young africa)miaka ya hivi karibuni alizua utata mkubwa sana baada ya kuruhusu viwanja vya michezo vya shule ya msingi Hananasif kujengwa jengo la shule ya sekondari.Utata huo ulizuka kutokana na kuwa kuna majengo mawili ambayo yalisimamishwa na rais mstaafu Al-haji Ali Hassan Mwinyi kuwa majengo hayo yalijengwa ktk eneo la shule,chakushangaza ni kwamba hapo yalipo majengo hayo pangetosha kabisa kujengwa hiyo shule,lakini amelazimisha ijengwe kwenye viwanja hivyo vya michezo.Suala ambalo lilionyesha wazi kuwa alifanya hivyo kwa ajili ya maslahi binafsi ili afanye biashara ktk ujenzi huo,coz anaduka lake la hardware.Sasa kinacho fanya nishangae ni kwamba juzi kwenye kiwanja hicho ambacho kimebaki kidogo kuliko maelezo,huyu mheshimiwa ameandaa mashindano ya soka akiyaita Tarimba cup ktk kiwanja ambacho hakina uwezo wa kuhodhi wachezaji 22,huku akiwapumbaza raia kwa kuweka zawadi ya donge nono la milion moja kwa bingwa,na elfu hamsini kwa kila mshiriki huku akisisitiza ccm inahamasisha michezo.My take,huyu jamaa anafanya hivi kutokana na ukweli kuwa uchaguzi umekaribia,na wananchi wameshadanganywa na hela wamesahau kilio chao.Je,yale majengo yaliyosimamishwa wana mpango nayo gani ?Mchango wenu tafadhali!!
   
Loading...