Abarikiwe aliyemleta Rais Samia Duniani

Umejitaidi kutoa uchafu wako kichwani. Vp unajisikiaje baada ya uharo wako huo
 
Hakika Rais Samia Suluhu alizaliwa kuja kuikomboa Tanzania katika mikono ya wachumia tumbo na waliokua hawajali haki za wananchi bali kujijali wenyewe lakini yeye ameingia madarakani amefungua soko la ajira mzunguko wa pesa ni mkubwa sana mtaani jana tumeona amezindua mradi mkubwa wa kilimo na lengo ni kuajiliri vijana zaidi ya milioni 3 hakika watanzania tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutupa kiongozi alieleta neema Tanzania
 
Kwa nchi ambayo ina wanachi wenye kujielewa, Samia hana sifa ya kua hata balozi wa nyumba 10. Kwa nchi ya vipofu, ndio matokeo yake haya Samia atasifiwa balaa.
 
China, India na nchi nyingi za Asia hawamjui mungu na wako mbali sana kwenye maendeleo kuliko sisi tunaong'ang'ania Mungu, Mungu Mungu, huyo Mungu kwa nini ameacha nchi zisiomjua ama kumuabudu ziendelee hadi kutaombe msaada kwao wakati yupo? Hana msaada.

Mungu ni hadithi tu za alinacha, Mungu hayupo. Ni kibwengo tu kimeumbwa kwenye akili za binadamu ila kiuhalisia hakipo.
 
Hivi hamuoni umeme unakatika Kila siku, tozo hamzioni Benki, Tigo pesa, Bei ya vyakula kuwa juu Kama unga 2,000, Michele 3,600, maharage 4,000, Deni la Taifa Tilion 100, je mnajielewa kweli. Kila siku kusifia.
Suala la umeme kwa Sasa Hali Ni njema kwa kuwa serikali inaendelea na kazi ya kuimarisha Miundombinu ya umeme pamoja na kutumia vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme Kama vile umeme wa gas, ili hata mvua ikikosekana watanzania Tuendelee kupata umeme wa uhakika bila shida, lakini pia wakati huu ambao mvua zinaendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini imepelekea kupatikana kwa umeme wa uhakika katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo kuwafanya watu Kuendelea na shughuli zao za kiuchumi zinazotegemea umeme.

Suala la Tozo ningependaa kukwambia kuwa Hakuna nchi Duniani Kati ya zile zilizoendelea na kupiga hatua za kiuchumi ambayo ilifika ilipo pasipo nguvu na mioyo ya watu wake katika ujenzi wa mataifa Yao, Ni lazima tuchangie kila mmoja kwa kadri ya kipato chake ili kuijenga nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe,Ndio maana unaona kupitia Tozo serikali yetu ilifanikiwa kujenga vyumba vya madarasa karibu elfu 20 na hivyo kufanya wanafunzi wote kulipoti shuleni kwa wakati mmoja, vituo vya Afya kila Kona ya nchi, utoaji wa Elimu bure Hadi kidato Cha sita,huduma za maji Safi na salama pamoja na ujenzi wa Miundombinu mbalimbali hapa nchini bila kusahau utoaji wa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea

Ndio maana watanzania wanaendelea kumuunga mkono mh Rais na serikali yake kwa kuwa wanaona faida ya kuchangia katika ujenzi na maendeleo ya Taifa letu wenyewe,lakini pia kila mmoja anajiona amechangia katika ustawi wa Taifa letu.

Suala la mikopo napo ningependaa kukwambia kuwa Hakuna nchi isiyo kopa au kuwa na madeni, kikubwa Ni unakopa kwa ajili ya kufanyia Nini? Aina ya mkopo,masharti au riba ya mkopo na muda wa kurejesha mkopo ,Mkopo tunachukua kuendeleza na kukamilisha kwa uharaka miradi yetu ya kimkakati kwa kuzingatia hayo niliyoyaeleza hapa juu ya mkopo,Hata hivyo Tanzania bado Deni letu Ni stahimilivu na ndio maana tunaendelea kukopeshwa na kukopesheka maana mtu hawezi kukukopesha pesa zake Kama anaona huna uwezo wa kulipa na huaminiki.
 
Kama wewe unamwamini shetani na kumwabudu Basi wewe endelea na ushetani wako Ila sisi watanzania siku zote tunamwamini Sana Mwenyezi MUNGU na kumtanguliza Mwenyezi MUNGU katika kulilinda Taifa letu, ili liendelee kuwa Tulivu na lenye amani kwa kuwapatia viongozi wetu hekima busara maarifa na njia ya kuongoza Taifa letu katika haki na upendo maana haki huinua Taifa
 
Mbowe ndio mtaalamu wa siasa za Tanzania bila hivyo Genge S wangemsumbua Samia sana.
 
Joined July 28, 2022
Post 4,556
Reaction 1,974

Good Job endelea kukaza buti utapewa teuzi mda si mrefu mama anapita humu
 
Kwa nchi ambayo ina wanachi wenye kujielewa, Samia hana sifa ya kua hata balozi wa nyumba 10. Kwa nchi ya vipofu, ndio matokeo yake haya Samia atasifiwa balaa.
Utakufa na chuki zako kwa Rais wetu Hodari mchapa kazi madhubuti imara mzalendo na Jasiri mama Samia suluhu Hassani ,Rais ambaye anachukuliwa Kama mtetezi na sauti ya Afrika na waafrika,kiongozi mwenye maono na Dira inayoeleweka ,kiongozi aliyejitoa na kujitolea kuwatumikia watanzania wanyonge wasio na sauti kwa upendo na uzalendo
 
Joined July 28, 2022
Post 4,556
Reaction 1,974

Good Job endelea kukaza buti utapewa teuzi mda si mrefu mama anapita humu
Kwani Nani kakwambia kuwa hii Ni barua ya maombi ya uteuzi wangu,au hujasoma nilichokiandika
 
China ama India ama Vietnam ambao hawamjui huyo Mungu unawazidi nini?
 
Umenena ukweli mchungu na Sina cha kuongeza maana umemaliza kila kitu kwa hoja yako iliyoshiba na kujitosheleza
 
Kusema ukweli imekua ni chuki tena. Samia ana maono gani?
 
Kusema ukweli imekua ni chuki tena. Samia ana maono gani?
Tumefika hapa tulipo na kuwa Taifa la kupigiwa mfano kutokana na maono makubwa aliyo nayo mh Rais katika kulipaisha kiuchumi Taifa letu,Ndio maana unaona ameweka mazingira na kusimamia vyema Sera za kiuwekezaji ili kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini, Ni maono ya Rais Samia yaliyopelekea kutoa Elimu bure Hadi kidato Cha sita na kuongeza bajeti ya mikopo ya Elimu ya juu ili kuzalisha wasomi wengi wa fani mbalimbali watakao litumikia Taifa letu katika nyanja mbalimbali
 
Umejitaidi kutoa uchafu wako kichwani. Vp unajisikiaje baada ya uharo wako huo
Jenga hoja ewe mtanzania usiye na adabu Wala hekima katika kuandika kwako,acha kutumia maneno ya ukakasi utafikiri mtu ambaye ulikosa malezi ya wazazi wako katika makuzi yako
 
Tanzania toka lini haijawahi kua taifa la mfano? Toka enzi za Mwalimu Tanzania ni taifa la mfano. Hiyo sio hoja.

Leta hoja nyingine.
 
Aisee umefika mbali sanaa ankolii.

Inatosha sasa, mvua zimeanza nenda kapande njugu mawe zitakusitiri msimu wa kiangazi ,
haya mambo ya uteuzi yamebuma kubali yaishe, move one ankolii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…