Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,429
Jaribio la mtu mmoja aliyetaka kuuza paka 500 kwenye migahawa tofauti ili watumike kama nyama, limeshindikana baada ya polisi kupata taarifa na kumkamata.
Gazeti la South China Morning Post limeripoti kuwa kwa muda mrefu mtu huyo, aliyejulikana kwa jina moja la Sun, alikuwa akiiba paka na kuiuzia migahawa iliyo karibu na jiji la Jiujiang katika jimbo la Jiangsu.
Polisi walidokezwa kuhusu mwizi huyo wa paka baada ya mtu aliyejulikana kama Yang alipoenda katika mamlaka husika. Paka wa Yang naye alipotea wakati akitibiwa.
Wakati wakimtafuta paka huyo, polisi waligundua sehemu ambayo Sun alikuwa akihifadhi paka kwenye mapango kati ya saba na nane katika kijiji kilichopo karibu ya Jiujiang, ripoti ya polisi inaeleza.
Inasemekana kuwa Sun alikuwa akijiandaa kusafirisha wanyama hao kwa ajili ya kuwauza kabla ya polisi kuwasili na kumkamata.
Baadaye, polisi waligundua nyumba nyingine iliyo karibu na barabara kuu ambako kulikuwa na mamia ya paka waliofungiwa wakisubiri kusafirishwa kwenda kwenye migahawa.
Paka wengi, baadhi wadogo na wengine shume, walikuwa katika hali mbaya kiafya, kwa mujibu wa polisi.
Sun alikuwa akikamata paka hao kwa kutumia ndege mdogo kama chambo. Mwizi huyo wa paka aliiambia polisi kuwa kila paka angeuzwa kwa dola 4.4 sawa na takriban Sh10,000.
Polisi haikueleza kama paka wa Yang, ambaye alitoa taarifa za kupotelewa na mnyama wake, alipatikana.
Chanzo; Mwananchi