Aaron Ramsey's Goal Curse

Raymanu KE

JF-Expert Member
Jan 20, 2022
6,843
12,593
Aaron Ramsey Ni mchezaji wa mpira wa soccer aliyejiunga na timu ya Arsenal mnamo tarehe 10/06/2008 akitokea Cardiff City.
Ni mchezaji aliyedhaniwa kuwa na gundu/ mikosi ya ajabu Sana baada ya watu kugundua kwamba kila anapofunga goli lazima mtu maarufu( celebrity) Duniani afe muda mfupi baada ya yeye kufunga bao.

Ifuatayo Ni list ya baadhi ya watu maarufu ( celebrities) Duniani waliofariki muda mfupi tu baada ya Aaron Ramsey kufunga goli.

1.OSAMA BIN LADEN
Ni aliyekuwa mhalifu hatari zaidi Duniani.
Mnamo 01/05/2011 mchezaji Aaron Ramsey alifunga bao la pekee kwenye mechi Kati ya Arsenal na Manchester United na baadae kidogo jioni ya siku hiyo ndipo mwamba hatari Osama Bin Laden alipokamatwa na maaskari wa Kimarekani na kuuaua.

2.STEVE JOBS
Huyu alikuwa chief Executive Officer wa kampuni ya Apple kipindi hiko.
Alifariki Dunia muda mfupi baada ya Aaron Ramsey kufunga goli kwenye mechi ya Arsenal dhidi ya Tottenham mnamo 05/10/2011

3.MUAMAR GADAFFI
Huyu alikuwa kiongozi katili (dictator) wa nchi ya Libya.
Mnamo 19/10/2011 Aaron Ramsey alifunga bao kwenye mechi ya UEFA champs.League dhidi ya Olympic Marseille ya Ufaransa na siku hiyo hiyo ndipo dictator Muamar Gadaffi alipokumbana na umauti kwa kuuaua.

4.PAUL WALKER
Huyu alikuwa Ni muigizaji ya filamu za Action na alihusika Moja kwa Moja katika movie maarufu za FAST & FURIOUS sehemu ya 1 Hadi 7.
Mnamo 30/11/2013 mchezaji Aaron Ramsey alifunga bao kwenye mechi ya Arsenal dhidi ya timu yake ya awali ya Cardiff City na siku Hiyo ndipo muigizaji Paul Walker alikufa kwa ajali ya barabarani kipindi wanashoot scenes za sehemu ya 8 ya FAST & FURIOUS

5.ROBIN WILLIAMS
He was a comic actor.
Alikumbana na umauti masaa machache baada ya Aaron Ramsey kufunga bao dhidi ya Manchester City mnamo 11/08/2014

6.EDUARDO GALEANO
Ni aliyekuwa mtangazaji na mwandishi wa habari maarufu zaidi kutoka nchini Uruguay.Alifariki mnamo 04/11/2015 siku ambayo Aaron Ramsey alifunga goli kwenye mechi ya Arsenal dhidi ya Burnley

7.DAVID BOWIE
American iconic singer.
Alifariki mnamo 09/01/2016 muda mfupi baada ya Aaron Ramsey kufunga bao dhidi ya Sunderland

8.ALLAN RICKMAN
Aliyekuwa mcheza filamu maarufu Sana Duniani.Huyu alikufa maasa 24 baada ya Aaron Ramsey kufunga bao dhidi ya Liverpool mnamo 13/01/2016 Allan Rickman alifariki mnamo 14/01/2016

9.NANCY REAGAN
Ni aliyekuwa mke wa hayati Ronald Reagan ambaye alikuwa Rais wa Marekani.
Nancy Reagan alifariki masaa machache baada ya Aaron Ramsey kufunga goli kwenye mechi ya Arsenal dhidi ya Tottenham mnamo 05/93/2016

Wapo watu wengine 14 zaidi waliokuwa maarufu zaidi Duniani ambao walifariki Dunia baada ya Aaron Ramsey kufunga goli.
Ikumbukwe kwamba Hawa wote walifariki baada Ramsey kufunga bao ,Yaani Hakuna aliyefariki kabla ya Ramsey kufunga bao.
Kwa hiyo watu wengi waliamini magoli ya Aaron Ramsey yalikuwa na uhusiano wa Moja kwa moja na vifo vya wale macelebrities.

Ila duru zinasema jamaa alipelekwa kanisani akafanyiwa maombi na matambiko mengine gundu zikaacha kumuandama.Kwa hiyo siku hizi akifunga bao hafi mtu yeyote Wala Hakuna ajabu yoyote inayotokea kufuatia ufungaji wake.
 
Tuanze kwanza kwa kutuambia sasa hivi anachezea timu gani... Au umeokota mtandaoni tu
 
1.OSAMA BIN LADEN
Ni aliyekuwa mhalifu hatari zaidi Duniani.
Mnamo 01/05/2011 mchezaji Aaron Ramsey alifunga bao la pekee kwenye mechi Kati ya Arsenal na Manchester United na baadae kidogo jioni ya siku hiyo ndipo mwamba hatari Osama Bin Laden alipokamatwa na maaskari wa Kimarekani na kuuaua
Huu ujinga mnaopandikizwa na kuaminishwa na Marekani na washirika wao sijui utawafikisha wapi katika kujikomboa kifikra.

Unasema Bin Laden mtu hatari zaidi duniani. Alikufanyia hatari gani wewe kama Mtanzania au Mwafrika wa Vingunguti?

Iraq, Libya, Syria na sasa Rusia, Korea Kaskazin na hata Iran wote hao ni hatari sana duniani kisa wanahatarisha maslahi ya wapuuzi flani.

Hiyo ilikuwa mbinu ya Bin Laden kupambana na alilenga adui zake. Kwa hiyo kwenye vita ni kuzidiana mbinu. Ukijipendekeza kwa adui zake wewe pia ni adui kama ilivyo tu kwa Marekani ukiunga mkono adui zake anatumia silaha yake ya jadi ya vikwazo na misaada.
 
Nimekuelewa ila umeandika kwa hisia Kali Sana,pole Kama nimekuzingua
 
Hapana mkuu, hata kidogo na wala mm sio muumini wa mfumo wa kimagharibi wala jihadi. Najaribu tu kuangalia katika mtizamo wangu. Pole nawe pale nilipokukwaza ikiwa imetokea hivyo.
 
Huu ujinga mnaopandikizwa na kuaminishwa na Marekani na washirika wao sijui utawafikisha wapi katika kujikomboa kifikra.

Unasema Bin Laden mtu hatari zaidi duniani. Alikufanyia hatari gani wewe kama Mtanzania au Mwafrika wa Vingunguti?

Iraq, Libya, Syria na sasa Rusia, Korea Kaskazin na hata Iran wote hao ni hatari sana duniani kisa wanahatarisha maslahi ya wapuuzi flani.

Hiyo ilikuwa mbinu ya Bin Laden kupambana na alilenga adui zake. Kwa hiyo kwenye vita ni kuzidiana mbinu. Ukijipendekeza kwa adui zake wewe pia ni adui kama ilivyo tu kwa Marekani ukiunga mkono adui zake anatumia silaha yake ya jadi ya vikwazo na misaada.
Yaani huyu jamaa ni pimbi kweli....ety muammar Gaddafi katili na dictator. Shenzi kabisa
 
Osama bin laden aliwahi kushambulia Tanzania watu wengi walifariki
Huu ujinga mnaopandikizwa na kuaminishwa na Marekani na washirika wao sijui utawafikisha wapi katika kujikomboa kifikra.

Unasema Bin Laden mtu hatari zaidi duniani. Alikufanyia hatari gani wewe kama Mtanzania au Mwafrika wa Vingunguti?

Iraq, Libya, Syria na sasa Rusia, Korea Kaskazin na hata Iran wote hao ni hatari sana duniani kisa wanahatarisha maslahi ya wapuuzi flani.

Hiyo ilikuwa mbinu ya Bin Laden kupambana na alilenga adui zake. Kwa hiyo kwenye vita ni kuzidiana mbinu. Ukijipendekeza kwa adui zake wewe pia ni adui kama ilivyo tu kwa Marekani ukiunga mkono adui zake anatumia silaha yake ya jadi ya vikwazo na misaada.
 
Kwahiyo ndio kusema ramsey amefunga magoli tisa tu tangu aanze kucheza mpira na kustaafu?
 
Huu ujinga mnaopandikizwa na kuaminishwa na Marekani na washirika wao sijui utawafikisha wapi katika kujikomboa kifikra.

Unasema Bin Laden mtu hatari zaidi duniani. Alikufanyia hatari gani wewe kama Mtanzania au Mwafrika wa Vingunguti?

Iraq, Libya, Syria na sasa Rusia, Korea Kaskazin na hata Iran wote hao ni hatari sana duniani kisa wanahatarisha maslahi ya wapuuzi flani.

Hiyo ilikuwa mbinu ya Bin Laden kupambana na alilenga adui zake. Kwa hiyo kwenye vita ni kuzidiana mbinu. Ukijipendekeza kwa adui zake wewe pia ni adui kama ilivyo tu kwa Marekani ukiunga mkono adui zake anatumia silaha yake ya jadi ya vikwazo na misaada.
Osama aliua ndugu zetu Dar na Nairobi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom