Aangua kilio cha huruma kwa kukosa ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aangua kilio cha huruma kwa kukosa ajira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 1, 2012.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]KIJANA mmoja [jina kapuni] alijikuta akiangusha kilio cha huzuni mara baada ya kutakiwa kuondoka katika ofisi alipofanya Interview ya kumuingiza katika ajira[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Kijana huyo alimwaga kilio chake hicho katika ofisi za wizara nyeti nchini wakati alipopewa majibu yake na kuonekana hatohitajika ofisini hapo kwa sababu ya kutofanya vizuri mitihani yake kwa mara ya pili

  Kijana huyo alifukuzwa katika ofisi hizo baada ya kuomba mara kadhaa asaidiwe na hakusikilizwa na aliendelea kuwa katika ofisi hizo huku akiangua kilio kikubwa kwa kushindwa mitihani hiyo ya kudahiliwa.

  Mtandao huu ulishuhudia viongozi kutoka wizara hiyo ikimtaka aondoke na kuacha kelele hizo kwani mitihani ndiyo iliyomfanya akose ajira wizarani hapo.

  Kijana huyo alikuwa ni mmoja wa waliochaguliwa kufanya Interviw na alifanikiwa kufaulu awamu ya kwanza na kwa taratibu zilizowekwa na wizara hiyo awamu ya pili ni kupewa mtihani utakaokuongoza kupangiwa idara ama kitengo kulingana na ufaulu wako na kuhakiki ama kweli ulihitimu elimu ambayo umewasilisha vyeti vyako ofisini hapo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyopata mtandao huu, kijana huyo akiwemo na wenzake wawili walishindwa mitihani hiyo na uongozi kuwapa nafasi kwa mara nyingine na kuonekana kushindwa tena mtihani huo kwa mara nyingine ambao ulidaiwa haukubadilishwa chochote.

  Hivyo kutokana na majibu hayo hakuweza kupata ajira kutoka hapo na alitakiwa aende nyumbani na kuambiwa hana nafasi kupata ajira hapo na kuanza kuangua kilio cha hapa na pale na viongozi kulazimika kumtaka aondoke nje ya ofisi hizo.

  Hata hivyo kwa mujibu wa wenzake waliobahatika kuingizwa katika ajira, walidai mwenzao huyo alikuwa akifikiria deni ambalo alikopa ili kutoa hongo ili apate ajira katika wizara hiyo na matokeo yake amekosa nafasi hiyo.

  "Inauma sana jamaa alipigania sana kutafuta ajira japo wengine tumetoa zaidi ya hiyo lakini haina machungu sana kwa sababu tumepata tulichokihitaji, sio riziki" walisema wafanyakazi hao.

  Imedaiwa kuwa kijana huyo alikopa kwa mtu kiasi cha shilingi laki tano na alitoa hapo ili aweze kupata ajira, kati ya hao watatu waliorudia mmoja alibahatika kupata ajira kwa kufaulu mtihani huo.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,436
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  bongo?
   
 3. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mhuuuuuuuu! Kafulila huyo.
   
 4. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wamrudishie mkwanja wake,au kiendacho kwa mganga.
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Wangemfanyia kabisa huo mtihani.
   
 6. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  I was just about to do the same: underline that part and ask what else was to be done.
  His childish attitude ndio imenishangaza even more!
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Habari inakosa utamu wa uwazi!

  Jina la kijana .....KAPUNI!
  Jina la Wizara.....KAPUNI!

  Hey meeen, talk openly!
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Halafu hilo kapu huwa halijai?
  Yaani majina ya watu na wizara yanashindiliwa humo humo.
  Heri hata angeweka tuu vina kama Ehud Brack
   
Loading...