Aah! nyonda! ee nyonda'angu!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Nikuye naye namiye
Yamtimani yakuye
Niseme namsikiye
Ya penzi lilozamiye
Aa! nyonda, nyonda 'angu!

Ya guso nitamaniye
Baridi 'ako nsikiye
Na busu unipatiye
'lo tamu nisimuliye
Aa! nyonda, nyonda 'angu!

Machoyo yanambie
Mikono nikumbatie
Sikio uling'atie
Na hamu inizidie!
Aa! nyonda, nyonda 'angu

Na jasho linitokeye
Na mate yadondokeye
Miguno elfu miye!
Tetemo ntetemiye!
Aa! nyonda, nyonda 'angu!

Raha unipatiye
Na miye nikupe weye
Wawili tupendaniye
Na joto tupashaniye
Aa! nyonda, nyonda 'angu!

Na mola atupatiye
Watoto atujaliye
Wakue tushuhudiye
Wajukuu atupe siye!
Aa! nyonda, nyonda 'angu!

Na beti nafunga miye
Nishike nikumbatiye
Unipe nikupe weye
Ni miye na wangu miye
Aa! nyonda, nyonda 'angu!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)
 
Vuvuzela Matata hiyo ni swahili ya Kongo au?..kuna maneno yamenimix!..Una bidii si kidogo,kudoz..
 
Hahahahahahah umenichekesha kweli hapo kwenye bold....Vuvuzela imeshanda chati nasikia Jabulani pia inapanda chati taratibu. Ni mtu ambaye hana msimamo akikwambia kitu chake basi usishangae kesho akabadilisha kabisa alichokwambia. Vipi yule alikuahidi hivyo? unamuamini kweli? Achana naye yule Jabulani tu! lol!
 
yani kweli tumepata misemo mipya..mpaka WC ziishe hiyo vuvu&jabu tayari vimejulikana sana na pia kwa maanda zetu nyingine..nimeshamsave mtu kwenye simu Vuvuzela mana anaongea huyo nabaki kusema okay,yeah,mhh na bye!.. job true true BAK!!!
Enjoy hilo shairi man mie kuna maneno bado nayatafakari!!!!
 
Yatafakari tu BJ kama ukitoka kapa basi yakusanye na umtumie Mkjj ili akufafanulie maana ya maneno hayo.
 
yani kweli tumepata misemo mipya..mpaka WC ziishe hiyo vuvu&jabu tayari vimejulikana sana na pia kwa maanda zetu nyingine..nimeshamsave mtu kwenye simu Vuvuzela mana anaongea huyo nabaki kusema okay,yeah,mhh na bye!.. job true true BAK!!!
Enjoy hilo shairi man mie kuna maneno bado nayatafakari!!!!

nimecheka hadi masikio yanauma! yaani ukiwa mahali usije kuisahaku hiyo simu maana mtu anaona inapiga halafu jina linaonesha "Vuvuzela". Halafu bora asiwe ndiyo shosti wako maana akijua!!
 
Lol....I hope hakuna aliyenisave mimi kama hivyo.....

You never know NN hahahah....mtu naweza akakutoa kiutu uzima kumbe huku anasema nilikuwa na vuvuzela linanipigia kelele tu nimemtolea nje lol!
 
Back
Top Bottom