Aachiwa baada ya kutishia kuua - Keko

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Mmiliki wa bar kubwa maarufu mitaa ya keko Roberti Mushi, usiku wa Jumapili mida ya saa sita alimjeruji dereva kijana aitwae Ngotikwe Ramadhani kwa kumpiga na mdomo wa bastola baada ya kuzipiga tatu hewani.

Roberti mushi ni mpangaji wa fremu zinazomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi akieleza kwa masikitiko makubwa mwenyeji wa eneo hilo alisema huyu jamaa ameachiwa kwa sababu anafahamiana na maaskari wa kituo cha polisi Chang'ombe kwasababu wamekua wakienda kwake usiku na kupewa pesa ila bar hiyo iwe inakesha usiku kucha kinyume na sheria ya kufunga saa sita.

Mtonyaji wangu aliniambia Roberti Mushi zamani alikuaga jambazi jambo ambalo linampa kiburi.

Usiku wa Jumapili huo baada ya tukio alikamatwa ila alitoka Jumatatu Mchana na silaha yake ipo mikononi mwa polisi, wakiongea kwa masikitiko makubwa wananchi wamelaani kitendo hicho cha polisi kumuachia Robert kwasababu ndio tabia yake kutishia watu silaha.

Niliombe Jeshi la Polisi kutenda haki kwenye kesi hiyo na zote zinazowafikia, huu utawala wa kusaidia wanyonge.

Zubedayo_mchuzi mzee wa umbali mrefu.

RB no: cha/rb/10197/2016

Jalada lipo chini ya askari hawa
OC-cid
D/CPL Andilile
D/C FARIDA
 
Back
Top Bottom