Tafasiri Hisio rasmi
Upendo wa kweli Hauna Mwisho (haumaliziki)
Ilikuwa ni asubuhi yenye harakati nyingi, muda wa saa 2:30 asubuhi, wakati wazee mwenye kuonekana ni muungwana akikaribia miaka 80 alifika ili kuondoa nyuzi kwenye kidole gumba.
Alisema alikuwa na haraka na anataka kuwahi mihadi yake muda wa saa 3:00 asubuhi.
Mimi nikamuchukulia kwa umuhimu mkubwa na nikamuelekeza kuketi kitini, kwa sababu nilijua itamchukua zaidi ya saa moja kabla ya mtu mwingine kuja kuonana naye.
Aliangalia saa yake, nikaona kwa sababu sina shughuri ya kuhudumia mgonjwa mwingine, naweza kutathmini jeraha lake. Nilipo liangalia nikakuta linaendelea vema, hivyo basi nikaongea na mmoja wa madaktari, ili kuchukua vifaa vinavyo itajika kuondoa mshono kisha nikavisha bendeji jeraha lake.
Wakati namuhudumia jeraha lake, Nilimuuliza kama alikuwa na mihadi na daktari mwingine Asubuhi hii, sababu alikuwa na haraka hivyo.
Yule Mzee aliniambia hapana, alikuwa anahitajika kwenda nyumbani ya uuguzi kula kifungua kinywa na mkewe. Nikauliza kuhusu Afya yake.
Akanambia kuwa yuko uko kwa muda sasa na ni mwathirika wa ugonjwa sjukdom (Kusahau).
Tulipokuwa tukiongea, nikamuuliza kama mkewe atajisikia vibaya kama atachelewa japo kidogo.
Akanijibu kuwa mkewe keshamsahau yeye ni nani na wala hawezi kumtambuwa tena, na ni miaka mitano sasa.
Nilishangazwa, nikamwuliza, "Na bado unakwenda kila asubuhi, ingawa yeye hakukumbuki kuwa wewe ni nani? '
Alitabasamu uku akinipigapiga mkono wangu na kusema, Hanitambui tena, lakini mimi bado namtambua yeye nani kwangu.'
Ilinibidi kuzuia machozi yasinitoke kwa msisimko wa mwili na mkono wangu.
Nikawaza, 'Huo ndio upendo ninayo utamani maishani mwangu. Upendo wa kweli si mapenzi ya kimwili au kimahaba.
Upendo wa kweli ni Kukubali hali zote, itakavyokuwa na isivyokuwa.
Pamoja na utani na furaha zote katika barua pepe, Wakati mwingine mtu analeta ujumbe muhimu...
Nami nimeona bora kukutumia ujumbe huu.
Watu wenye furaha si lazima wawe na kila kitu kilicho bora kwenye kila kitu; Wao uona kilicho bora kwa kile kitu walicho nacho.
Natumaini nawe utamtumia yule unaye mjali.
Mimi nishafanya...
'Maisha si kustahamili tu dhoruba,
Bali ni kujua kucheza na mvua.'
Sisi sote tuta zeeka,
kesho yaweza kuwa zamu yetu.