A talented guy from Kigoma

A talented guy from Kigoma

Talha

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2021
Posts
202
Reaction score
224
Nilikua naangalia Tbc aridhio kuna kijana jina limenitoka kutoka kigoma amenivutia mno kwa vitu anavyovifanya pamoja na mazingira anayoishi ikiwa ni pamoja na nyumba haina umeme lakini ameweza kufanya mambo mazuri cha kwanza ni ameweza kutengeneza mtambo wa kurusha matangazo/radio channel yake kaiita kigoma Fm but ina uwezo wa kurusha matangazo umbali wa mita 100 hivi kwahiyo majirani zake wamekua wanamsikiliza. Pia ameweza kutengeneza pikipiki hii pikipiki lakin nadhani ni kama toy ya kuchezea, na kingine katengeneza jiko la kupikia ambalo unaweza ukaset muda linatumia umeme wa jua.
Kiukweli sio vitu vipya anavyovifanya but hakika ni kijana kama angepata support ya kusomeshwa au kuinuliwa kipaji chake hakika naamini angefika mbali mno.

Kipaji chake ni kikubwa mno maana sio wote tunaweza kufanya hivo,naweza nikasema haijarishi mtu uko na mazingira gani lakini kama Mungu akikupa kitu jua amekupa,sio wote tunaweza kuchora,sio wote tunaweza kuimba,sio wte tunaweza kua wabunifu,sio wote tunaweza kucheza na vipaji vingine, sasa hivi kuna sekeseke la kukosa ajira hasa kwa sisi vijana lakini angalia kitu gani Mungu amekupa cha ziada unaweza ukakionyesha hususani tupo katika kipindi ambacho technology imekua mno tusikae kizembe tutumie fursa adhimu iliyopo.
If you have any talent just grow up with your talent.
 
Kigoma tumebarikiwa sana kwahilo tumshukuru mungu wengi tunavipaji but hatupati nafasi ya kuvionuesha
 
Back
Top Bottom