A shameful battle field

Rationalizer

Member
Jul 12, 2013
46
19
KUSHINDWA VITA.
Mh. Paul Makonda ameshashindwa vita. Sio kosa lake kwa sababu ukienda vitani aidha kuna kupiga au kupigwa ndio maana kuna msemo " Backfire" ambayo inakuja kama KARMA ama LAANA au A COMPLETE DEFEAT na lazima ukubali matokeo na wapenzi wako wakubali kubaki kuwa wafariji wako na sio kukupa moyo eti, utayashinda yote kwa yeye akutiae nguvu kwani haiwezekani tena. Serikali imesema na sio Mh. Makonda akiwa mmoja wapo na sio Paul Makonda kasema ndiyo ilikuwa kigezo cha ushindi wa vita.

MAKOSA YA KIUFUNDI ALIYOYAFANYA MH. MAKONDA

1.0 LACK OF SITUATION ANALYSIS
Hakuna ubishi kwamba binadamu yeyote aliyefanikiwa kimaisha lazima awe amepitia milima na mabonde mengi. Kama ilivyo kwa Mh. Makonda, alipaswa kukumbuka alitokea wapi, yuko wapi na anaelekea wapi na hili halitegemei sheria, maandiko matakatifu wala kanuni zilizotungwa na kuhifadhiwa kimaandishi, isipokuwa utashi binafsi na ushauri wa kweli wa marafiki, ndugu na wanaofanya naye kazi ndio ilikuwa ngao yake ya kutekeleza majukumu akiamini kwamba kila analolitenda liko kisheria, limeamuliwa na wengi kwa kufuata mifumo sahihi ili kupunguza kasi ya kupingwa kama inavyoonekana sasa.

2.0 ALIKUWA KISIASA ZAIDI
Alitaka wateule wengine kama Kamanda Sirro, wakuu wa mikoa mingine, manaibu na mawaziri wao pamoja na makatibu wakuu waonekane wazembe wakati yeye akijijengea umaarufu, ili Mh. Rais amuone, amuamini na ampe majukumu zaidi ya aliyonayo ila kiuhalisia isingewezekana.

3.0 HAKUJUA VITA ALIYOTAKA KUPIGANA
Kuijua vita inahusisha kujiuliza maswali mengi pamoja na yafuatayo, Ni aina gani ya vita? , Ina maadui gani na uwezo wao kifedha na pia uwezo wao kiakili ni upi? Zaidi ya fedha na akili, maadui wana silaha gani za ziada? Je maadui wanayo political back-up be it national or international?

Je kuna uzoefu wa kupambana na vita kama hii aidha nchini na au kimataifa? Je kama uzoefu upo, mbinu zipi zilitumika? Ushindi ulipatikana or it just ended as a lost war in the shameful battle field? Rasilimali watu, fedha na muda gani zitahitajika? Je technologia gani ya mawasiliano au ya mitambo/nyenzo za kivita zitumie hasa kwa kuzingatia technologia wanayotumia maadui?

Vita vitakapopigwana, madhara gani yategemewe? Na je ni kina nani wataathirika na kwa kiwango gani? Maadui wakiamua ku-counter attack, watatumia mbinu gani na mbinu zao zitakuwa na madhara gani? Anyway, so many questions to ask ila itoshe tu kujiuliza kwamba Mh. Paul Makonda amejiuliza maswali haya na mengine mengi? Mh. Makonda naamini utasoma hapa, je umegundua udhaufu wako hapa au utaishia kuniona mbaya kwa maoni yangu?

4.0 KUSHINDWA KUJITETEA
Mashambulizi yalivyozidi, Mh. Makonda alisahau nguvu ya dola aliyoitumia kwa cheo chake kuendesha vita na badala yake, akaanza kulalamika kuna mpango wa kutumiwa majini, mara kuonekana misikitini akiombewa na kanisani akilia machozi. Hapa ndipo what the scientist call " A Verifiable Indicator" of a no more strength to keep fighting but rather defending oneself.

SILAHA PEKEE
1.0 WANANCHI
Utashi wa watanzania waamue wamsamehe au waendelee kumshupalia japo kuna mgawanyiko hapa, wapo wanaomtetea na wanaomkosoa na inatokana na jinsi jamii ilivyoguswa na tuhuma zinazomkabili Mh. Paul Makonda ikilinganishwa na jinsi walivyomchukulia kabla hajatuhimiwa na uzito wa hadhi aliyonayo sasa. Kunyamaza kimya bila kujibizana na kina Gwajima ineemsaidia kupunguza msongo wa mawazo pamoja na mijadala mitandaoni pamoja na magazetini lakini sasa it is too late kwani kiuhalisia wakosoaji ni wengi kuliko wanaotetea.

2.0 UONGOZI WA NCHI
Hakuna njia nyingine zaidi ya aidha kumshauri Mh. Makonda ajiuzulu kwa heshima yake binafsi, familia yake, chama pamoja na serikali ama uteuzi wake utenguliwe ili mamlaka ya uteuzi ijijengee heshima ya utendaji kazi kwa haki hasa ukizingatia kuna waliopatikana na tuhuma kama au zinazofanana kwa kiasi fulani na za Mh. Paul Makonda ambazo madhara ya dhahama zilizowakumba zinaweza kuleta tafsiri ya uonevu pale makando kando ya Mh. Makonda yakipotezewa kiaina.


Nawasilisha
 
Umepembua vizuri sana, yeye alijua Jeshi la Police linaweza kupambana na kila kitu, kumbe kuna vitu ni technic tu, ona sasa mpaka anamwaga chozi kanisani.. What a shame???

Na hili la vyeti Ni moja Tu, watu .wakiamua wanabumbulua mengine mengi Tu. Nyerere hakua mjinga Kung'atuka.

Kunguru Muoga huishi miaka mingi.

Nyani Mzee kakwepa Mishale Mingi.

Mti ukibishana na upepo huvunjika.

Ni heri maji na mkate penye amani kuliko maziwa na asali penye vita

Usimtegemee Mwanadamu. YEREMIA 10:23
 
Mtoa mada anataka kuamnisha Taifa Viongozi wasipigane vita, Mtoa mada ameamnsha Taifa gwajima sio mtu mwenye makosa.....Mtoa mada anatujengea wananchi tuogope vita hata kama hatuna vifaa vya kisasa.....Wakat Eltrea wanapigana na Ethiopia ni wachache na walkuwa na silaha duni lakn waliwadunda vizuri tu....Makonda hajashindwa vita...Mako Vita vyake vinatokana na utendaji wake katika kazi.....wakat mtoa mada wataka mako hawekwe kando....Utajckiaje akiwa Naibu waziri??? Utahama Nchi? Wanaomshambuliwa Mako mitandaon hawafk hata theruth ya Watanzania...Ni kikundi kdg mno cha chadema na wauza unga.....
 
Mange Kimambi kasema Maombi kwa rc ni sawa lkn yaelekezwe kwa nani?. Manake tuna Daud Bashite na Paul Makonda, na ktk maombi lazima utaje jina halisi la mlengwa. Rc taja jina uombewe nalo.
 
Mtoa mada anataka kuamnisha Taifa Viongozi wasipigane vita, Mtoa mada ameamnsha Taifa gwajima sio mtu mwenye makosa.....Mtoa mada anatujengea wananchi tuogope vita hata kama hatuna vifaa vya kisasa.....Wakat Eltrea wanapigana na Ethiopia ni wachache na walkuwa na silaha duni lakn waliwadunda vizuri tu....Makonda hajashindwa vita...Mako Vita vyake vinatokana na utendaji wake katika kazi.....wakat mtoa mada wataka mako hawekwe kando....Utajckiaje akiwa Naibu waziri??? Utahama Nchi? Wanaomshambuliwa Mako mitandaon hawafk hata theruth ya Watanzania...Ni kikundi kdg mno cha chadema na wauza unga.....


upload_2017-3-6_14-18-17.jpeg
 
A shameful loss rather. Huyu jamaa no wonder wanasema alitaga, kwa sababu kila siku anakuja na drama za kumfanya aongelewe zaidi na zaidi.

Na ina maana Sisiemu haimshauri Mh Mtawala atatue hii mambo mapema, au ndio hasikilizi mtu? Au pengine nao wameshaona red flags, so wanamuacha ajifie....? Kiongozi yeyote makini na timamu angeshaona madhara ya hili saga, kisiasa na kiuongozi.
 
Ukimtazama Daudi Albert bashite usoni ni kama ana shida ya ufahamu/ugonjwa wa akili!
tunachotaka hapa ni haki bin haki itendeke taifa ni letu sote na sheria ziwaguse wote wanaokosa bila kujali Waziri, RC au DC. Hakiiii ndiyo itawale bila kujali kabila, jinsia, dini au chochote kile.
 
Rationalizer umenena vyema kiongozi,, thumbs-up!!!! Mwacheni aliye mwishowe atanyamaza!! Alifikri kuwasingizia wenzie ni kazi ndogo? Ona majuto yanavyomkumba!! Sasa hivi ukikafunua ka-Bashite rohoni kanajisemea bora ningejikalia kimya tu haya yakapita!! Sijui katajificha wapi dunia hii!!
 
Back
Top Bottom