A new favorable post for Harrison Mwakyembe!

A new favorable post for Harrison Mwakyembe!

reandle

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
11,166
Reaction score
8,159
Nitangulie tu kusema kwamba mimi si Shabiki wa Mwakyembe. Na hata humu jamvini nimepata kumponda si mara moja wala mara mbili! Hata hivyo, nitakuwa mnafiki niliyekubuhu nitakaposhindwa kutamka hadharani kwamba huyu ndie kiongozi pekee tangu awamu ya Ally Hassani Mwinyi hadi sasa ambae ameweza kunigusa kiutendaji!!

Frankly speaking, namuona Mwakyembe kwamba ndie kiongozi pekee hadi sasa ambae amelitambua kwa mapana yake tatizo kuu la nchi hii na kuamua kulivalia njuga!!

Matatizo makuu ndani ya jamhuri yetu ni mawili......UFISADI NA UWAJIBIKAJI! Wapo viongozi wanaochukia ufisadi, lakini kwa bahati mbaya wanashindwa kuwa WAWAJIBIKAJI hata linapokuja suala lile lile wanalolichukia....UFISADI!! Kwamba, ufisadi unafanyika ndani ya mamlaka yako, lakini unashindwa kuchukua hatua na badala yake unabaki kulalama na ama labda kufoka! Frankly speaking, ni heri uwe na kiongozi fisadi lakini muwajibikaji kuliko kuwa na kiongozi asiye fisadi na sio mwajibikaji! Hapa ndipo unapokutana na ukweli ule kwamba bado Lowassa ni kipenzi cha watanzania wengu hadi leo licha ya tuhuma za ufisadi ambazo zimekuwa zikimwandama for years now!! Nachukia ufisadi, lakini ukinilazimisha nitoe hukumu ama kwa kiongozi fisadi au kwa kiongozi asiye mwajibikaji; basi huenda rungu langu likamshukia asiye mwajibikaji endapo condition itakuwa ni kushusha rungu husika kwa mmoja wao tu!

As of now, Harrison Mwakyembe ame-prove si tu kwamba ni Mwajibikaji mzuri bali pia ni mtu ANAYECHUKIA UFISADI!! Naomba hapa tutofautishe ingawaje ukiangalia kwa jicho la wepesi unaweza usione tofauti! Kuna mtu kutokuwa fisadi na kuna mtu kuchukia ufisadi!! Wala sina hakika kwamba Mwakyembe sio Fisadi bali lililo dhahiri kwangu ni kwamba Mwakyembe ANACHUKIA UFISADI!! Kutokua fisadi na kutochukua hatua dhidi ya mafisadi ni kutochukia ufisadi! Hakika, nchi yetu hapa ilipofikia katu haina haja na mtu kama huyo!! Nchi hii inahitaji mtu kama Mwakyembe ambae at least anaonesha kwa vitendo kwamba anachukia ufisadi!! Laiti leo hii panaitishwa uchaguzi mkuu na hivyo mie kupiga kura kwa kuangalia national interest, basi sina shaka kwamba kura hiyo nitaipeleka kwa Mwakyembe vinginevyo nitakuwa nimeangalia personal interest!

Kutokana na hayo hapo juu, nashawishika kuamini kwamba Harrison Mwakyembe anahitaji post nyingine zaidi ya hii aliyonayo hivi sasa! Hii ni muhimu kwavile ufisadi ndani ya nchi hii upo kila mahala! It's very unfortunately, kutokana na nafasi aliyonayo Mwakyembe basi analazimika kushughulikia ufisadi kwenye eneo lake la kazi tu kwani kwingineko hana mamlaka nako! Hivyo basi, natamani pangekuwapo Wizara mpya itakayofanana na jina sawa na Wizara ya Kupambana na Kuzuia Rushwa! TAKUKURU, iwe ni just one of the Agency/Authority/Department ya hii Wizara! Likewise, Department of Director of Public Prosecution nayo iwe splited up na kuwe na section itakayo-deal na masuala ya corruption tu! Section hii nayo, iwe chini ya wizara mpya!

The rationale of my advice?!
Miongoni mwa taaisisi tatizo ndani ya nchi hii ni TAKUKURU na Idara ya Mwendesha Mashitaka ya Umma(DPP)! Hizi taasisi ni tatizo na ni good corruption accelerators huku viongozi wake wakiwa wanatupiana lawama wenyewe kwa wenyewe!! Ni kawaida kabisa kusikia bosi wa TAKUKURU akisema DPP anachelewesha kesi za ufisadi huku DPP nae akilalamika TAKUKURU kuchelewesha uchunguzi!! Wote hawa wanabebwa na kitu kimoja; nacho ni kuwa chini ya viongozi(wa Wizara) WASIOCHUKIA UFISADI! Nashawishika kuamini kwamba watu kama hawa (Feleshi/DPP na Hosea) wanapaswa kuwa chini ya mtu anayechukia ufisadi na mwenye spirit ya uwajibikaji!

Honestly speaking, naamini kwa nafasi kama hii au nyingine yoyote (even being head of state) kama hii basi inaweza kutoa mwanya kwa Harrison Mwakyembe kupashughurikia kila pahala!
 
Mkuu pole sana inaonekana umekurupuka kutoka usingizini; Ni kweli hata mie binafsi namkubali sana Dr. Mwakyembe kwa utendaji wake wa kazi, lakini natofautiana na wewe kimtizamo mabadiliko katika nchi hii hayawezi letwa na Dr. Mwakyembe mwenyewe, tatizo ni mfumo mzima umeoza, unanuka na umekumbatia ufisadi. Suppose Dr. Mwakyembe anakuwa rais kwenye uchaguzi ujao, watakao unda serikali yake si ndo hao hao mafisadi ana pambana nao? Jiulize issue ya Dr. Mwakyembe na ATC imeishia wapi, ndo ujue jinsi mafisadi walivyo na nguvu zaidi ya Dr.Mwakyembe.
 
Ccm hawawezi kumpitisha kuwania uras kwa sababu zifuatazo
1.Wana-ccm wanampitisha mtua aliyekubalika ndani ya balaza na si anaekubalika na wanatanzania wengi.

2.Huwa wanamchagua mtu atakeyelinda interest zao binafsi na si za nchi,

3.Mtu mwenye kundi(mtandao) kubwa ndani ya ccm ndio anayepitishwa.
Kutokana na sababu hizo hapo me naona chama akiwezi kumpitisha kuwania.
 
SIJAKURUPUKA.......hayo ya mfumo tushaandika sana, tena sana lakini hata huo mfumo bado unahitaji committed personnels to keep it in track!!
 
Ccm hawawezi kumpitisha kuwania uras kwa sababu zifuatazo
1.Wana-ccm wanampitisha mtua aliyekubalika ndani ya balaza na si anaekubalika na wanatanzania wengi.

2.Huwa wanamchagua mtu atakeyelinda interest zao binafsi na si za nchi,

3.Mtu mwenye kundi(mtandao) kubwa ndani ya ccm ndio anayepitishwa.
Kutokana na sababu hizo hapo me naona chama akiwezi kumpitisha kuwania.

.........

Nakubaliana nawe kuhusu hoja zote huku mbili za kwanza zikiwa ni tatizo wakati hoja yako ya mwisho ni jambo la kawaida....in politics, u must have strong a supporters base otherwise u're done while u're still under water! Tatizo ni aina ya hao suporters....are they for national interests or otherwise!
 
mkuu NasDaz umeongea sawa. dk. mwakyembe mi naamin akipata nafas hzo au akiweza kuwa rais atatusaidia sana kusogea mbele kwa kasi kubwa. lasivo tutakuwa tunaenda kwa mwendo wa harijojo. wakuu, ufisad na kutowajibika ndo vitu vikuu vinavyo turudisha nyuma. mengine ni visingizio tu
 
ccm wasipompitisha yeye au mtu wa aina yake kugombea watapoteza urais. wasipoupoteza urais basi watakuwa wameamua nchi ipoteze miaka 5 au 10. watakuwa watakuwa wameamua kutu-lostisha
 
You're very right....jamaa yaani anaonesha dhati ya nafsi kwamba anachukizwa na ufisadi na ukosefu wa kuwajibika....haya matatizo ni makubwa sana nchini mwetu!
 
Ccm hawawezi kumpitisha kuwania uras kwa sababu zifuatazo
1.Wana-ccm wanampitisha mtua aliyekubalika ndani ya balaza na si anaekubalika na wanatanzania wengi.
2.Huwa wanamchagua mtu atakeyelinda interest zao binafsi na si za nchi,

3.Mtu mwenye kundi(mtandao) kubwa ndani ya ccm ndio anayepitishwa.
Kutokana na sababu hizo hapo me naona chama akiwezi kumpitisha kuwania.

maandamano tu yataondoa mzizi wa fitna
 
Good analysis nami pia sipingani nawe kwa yale yote anayo yafanya ndugu Mwakyembe. Anacho kifanya kwa sasa ni hatua ya pili lakini hatua ya kwanza hakuwatendea haki watanzania ambao leo tuna msifia ya kuwa ni mtu ambaye ameonyesha uthubutu wa kuwawajibisha wazembe kwenye serikali hii ya wajanja. Tatizo analojaribu kulishughulikia sasa hivi alikuwa na nafasi ya kulikata kichwa dubwashika hili lakini alichagua mapenzi kwa CHAMA na SERIKALI iliyoko madarakani kwenye sakata la RICHMOND.Alificha ukweli wa kiini cha UFISADI na uzembe katika suala la UWAJIBIKAJI iweje leo tumuone kuwa ni shujaa??????? Anacho kifanya sasa hivi ni Revenge of skeleton -kulipiza kisasi- (igizo maarufu) hasa baada ya kumtenda toka kwa genge la mafisadi na wanamtandao. Kwa macho yawadanganyika anastahili sifa lakini watanzania wanao angalia mambo kwa mtazamo mkubwa huwezi kuwashawishi kwasuala unalo ongelea hasa mtu anapopewa nafasi ya kutimiza wajibu wake kwa umma wa taifa lakini akachagua mapenzi kwa chama na serikali na kuliacha Taifa lake. So sifa mpeni lakini ukweli utabaki palepale-AMESHINDWA KUONYESHA UZALENDO ULIO TUKUKA KWA TAIFA LAKE-
 
well spoken nasDaz!! kudoz. japo maoni kidogo kama ifuatavyo na kwa kukunukuu:-

"Kwamba, ufisadi unafanyika ndani ya mamlaka yako, lakini unashindwa kuchukua hatua na badala yake unabaki kulalama na ama labda kufoka!"

JK na Pinda ni mfano wa viongozi wa aina hii; pacifiers! hata body language yao huwa haionyeshi kama ni mtu amechukia jambo na anataka kuchukua hatua madhubuti kama alivyokuwa Ben mkapa!! tabia ambayo huwa inawaacha mafisadi wakijipa moyo kwamba kwamba "its business as usual;" Mkulu wa kaya hana neno; si umemuona bwana??!!!

"Frankly speaking, ni heri uwe na kiongozi fisadi lakini muwajibikaji kuliko kuwa na kiongozi asiye fisadi na sio mwajibikaji!

ClearlyEd Lowasa fits this description! Ed ameandamwa sana na tuhuma zisizothibitishwa za ufisadi lakini anabaki kuwa kiongozi mwenye ujasiri wa kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia; Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe;

"Kuna mtu kutokuwa fisadi na kuna mtu kuchukia ufisadi!! Wala sina hakika kwamba Mwakyembe sio Fisadi bali lililo dhahiri kwangu ni kwamba Mwakyembe ANACHUKIA UFISADI!!"

Harison hawezi kuchukia ufisadi kisha akawa fisadi; kwa sababu kuwa fisadi kisha akachukia ufisadi ni positions mbili zinazokinzana na kwa hiyo dr. Mwakyembe asingekuwa na moral authority ya kusimama kifua mbele kupambana na madudu ambayo anajua serikali nzima inayajua lakini hawawezi kuyakemea kwa sababu they are also embedded; fuatilia vizuri rekodi ya utumishi wa umma ya Dr. Harrison utamfahamu vizuri na kumtendea haki;

"Kutokana na hayo hapo juu, nashawishika kuamini kwamba Harrison Mwakyembe anahitaji post nyingine zaidi ya hii aliyonayo hivi sasa! Hii ni muhimu kwavile ufisadi ndani ya nchi hii upo kila mahala!"

Dr. Harisson katika mfumo wa utawala bora kamili anastahili awe Rais wa jamhuri au pungufu ya hapo basi awe Waziri mkuu mtendaji (Coordination and Supervision); kwa bahati mbaya wale wanaonufaika na mfumo uliopo wa kifisadi na hujuma ya mali ya umma (Machiavelian conformists) hawako tayari kumuona mtu mzalendo kama Dr Mwakyembe akifika hapo juu! kwa sababu atabomoa mitandao yao ya uhujumu; wako tayari wamtoe roho ili waendelee na ufisadi wao.
 
Mimi nadhani huyu jamaa akiongezewa majukumu atakua niutralised kwa kua ufisadi umezagaa kila mahali kwenye hii serikali ya sisiemmm. Wacha apambane na bandari na eneo hilo dogo. Tukimtakia madaraka zaidi tunaweza kumwingiza matatani na wapenda madaraka kwenye chama chake tukampoteza. Tatizo ni the whole system.
 
kaka umenene lakini tatizo siyo watu,

tatizo ni misingi tuliyoiweka kikatiba,

tunahitaji katiba itakayolazimisha uwajibikaji wa kila mtu ikiwa ni pamoja na wananchi

naamini akina mwakyembe tupo wengi sana

tupiganie katiba yenye mifumo bora ya kuwajibisha tusitegemee uwezo wa mtu binafsi, watu wanapita tu.
 
nitangulie tu kusema kwamba mimi si shabiki wa mwakyembe. Na hata humu jamvini nimepata kumponda si mara moja wala mara mbili! Hata hivyo, nitakuwa mnafiki niliyekubuhu nitakaposhindwa kutamka hadharani kwamba huyu ndie kiongozi pekee tangu awamu ya ally hassani mwinyi hadi sasa ambae ameweza kunigusa kiutendaji!!

Frankly speaking, namuona mwakyembe kwamba ndie kiongozi pekee hadi sasa ambae amelitambua kwa mapana yake tatizo kuu la nchi hii na kuamua kulivalia njuga!!

Matatizo makuu ndani ya jamhuri yetu ni mawili......ufisadi na uwajibikaji! Wapo viongozi wanaochukia ufisadi, lakini kwa bahati mbaya wanashindwa kuwa wawajibikaji hata linapokuja suala lile lile wanalolichukia....ufisadi!! Kwamba, ufisadi unafanyika ndani ya mamlaka yako, lakini unashindwa kuchukua hatua na badala yake unabaki kulalama na ama labda kufoka! Frankly speaking, ni heri uwe na kiongozi fisadi lakini muwajibikaji kuliko kuwa na kiongozi asiye fisadi na sio mwajibikaji! Hapa ndipo unapokutana na ukweli ule kwamba bado lowassa ni kipenzi cha watanzania wengu hadi leo licha ya tuhuma za ufisadi ambazo zimekuwa zikimwandama for years now!! Nachukia ufisadi, lakini ukinilazimisha nitoe hukumu ama kwa kiongozi fisadi au kwa kiongozi asiye mwajibikaji; basi huenda rungu langu likamshukia asiye mwajibikaji endapo condition itakuwa ni kushusha rungu husika kwa mmoja wao tu!

As of now, harrison mwakyembe ame-prove si tu kwamba ni mwajibikaji mzuri bali pia ni mtu anayechukia ufisadi!! Naomba hapa tutofautishe ingawaje ukiangalia kwa jicho la wepesi unaweza usione tofauti! Kuna mtu kutokuwa fisadi na kuna mtu kuchukia ufisadi!! Wala sina hakika kwamba mwakyembe sio fisadi bali lililo dhahiri kwangu ni kwamba mwakyembe anachukia ufisadi!! Kutokua fisadi na kutochukua hatua dhidi ya mafisadi ni kutochukia ufisadi! Hakika, nchi yetu hapa ilipofikia katu haina haja na mtu kama huyo!! Nchi hii inahitaji mtu kama mwakyembe ambae at least anaonesha kwa vitendo kwamba anachukia ufisadi!! Laiti leo hii panaitishwa uchaguzi mkuu na hivyo mie kupiga kura kwa kuangalia national interest, basi sina shaka kwamba kura hiyo nitaipeleka kwa mwakyembe vinginevyo nitakuwa nimeangalia personal interest!

Kutokana na hayo hapo juu, nashawishika kuamini kwamba harrison mwakyembe anahitaji post nyingine zaidi ya hii aliyonayo hivi sasa! Hii ni muhimu kwavile ufisadi ndani ya nchi hii upo kila mahala! It's very unfortunately, kutokana na nafasi aliyonayo mwakyembe basi analazimika kushughulikia ufisadi kwenye eneo lake la kazi tu kwani kwingineko hana mamlaka nako! Hivyo basi, natamani pangekuwapo wizara mpya itakayofanana na jina sawa na wizara ya kupambana na kuzuia rushwa! Takukuru, iwe ni just one of the agency/authority/department ya hii wizara! Likewise, department of director of public prosecution nayo iwe splited up na kuwe na section itakayo-deal na masuala ya corruption tu! Section hii nayo, iwe chini ya wizara mpya!

The rationale of my advice?!
Miongoni mwa taaisisi tatizo ndani ya nchi hii ni takukuru na idara ya mwendesha mashitaka ya umma(dpp)! Hizi taasisi ni tatizo na ni good corruption accelerators huku viongozi wake wakiwa wanatupiana lawama wenyewe kwa wenyewe!! Ni kawaida kabisa kusikia bosi wa takukuru akisema dpp anachelewesha kesi za ufisadi huku dpp nae akilalamika takukuru kuchelewesha uchunguzi!! Wote hawa wanabebwa na kitu kimoja; nacho ni kuwa chini ya viongozi(wa wizara) wasiochukia ufisadi! Nashawishika kuamini kwamba watu kama hawa (feleshi/dpp na hosea) wanapaswa kuwa chini ya mtu anayechukia ufisadi na mwenye spirit ya uwajibikaji!

Honestly speaking, naamini kwa nafasi kama hii au nyingine yoyote (even being head of state) kama hii basi inaweza kutoa mwanya kwa harrison mwakyembe kupashughurikia kila pahala!

noted with concern.
 
Good analysis nami pia sipingani nawe kwa yale yote anayo yafanya ndugu Mwakyembe. Anacho kifanya kwa sasa ni hatua ya pili lakini hatua ya kwanza hakuwatendea haki watanzania ambao leo tuna msifia ya kuwa ni mtu ambaye ameonyesha uthubutu wa kuwawajibisha wazembe kwenye serikali hii ya wajanja. Tatizo analojaribu kulishughulikia sasa hivi alikuwa na nafasi ya kulikata kichwa dubwashika hili lakini alichagua mapenzi kwa CHAMA na SERIKALI iliyoko madarakani kwenye sakata la RICHMOND.Alificha ukweli wa kiini cha UFISADI na uzembe katika suala la UWAJIBIKAJI iweje leo tumuone kuwa ni shujaa??????? Anacho kifanya sasa hivi ni Revenge of skeleton -kulipiza kisasi- (igizo maarufu) hasa baada ya kumtenda toka kwa genge la mafisadi na wanamtandao. Kwa macho yawadanganyika anastahili sifa lakini watanzania wanao angalia mambo kwa mtazamo mkubwaI huwezi kuwashawishi kwasuala unalo ongelea hasa mtu anapopewa nafasi ya kutimiza wajibu wake kwa umma wa taifa lakini akachagua mapenzi kwa chama na serikali na kuliacha Taifa lake. So sifa mpeni lakini ukweli utabaki palepale-AMESHINDWA KUONYESHA UZALENDO ULIO TUKUKA KWA TAIFA LAKE-

Fikra kama hizi ndio zinazotufanya tupige marktime kama Taifa. Tunabaki kulialia tu wakati tunatakiwa kufanya kazi na kusonga mbele.
Leo hii hakuna asiyejua kuwa Richmond ni Ufisadi wa wakubwa.......na hivyo ni wajibu wetu kama wananchi kuwaelimisha wananchi ili wahusika wasirudi madarakani.........lakini hamtaki kufanya hiyo kazi mpaka sasa mafisadi wanajisafisha.........na kuonekana eti mafisadi watendaji..........Mwakyembe alikwishafanya kazi yake .......whether umempa 20% or 70%...its not relevant...........mijitu mingine imebakia kulialia ikitaka kusikia na ku-assume JK alihusika ndio itafurahi........mijitu hii siasa za vyama zimewatawala kuliko kuwatumikia wananchi......na hivyo walioko madarakani wasifanye kazi kisa eti kuna mambo hakuyasema kwenye Richmond.........extremely poor mentality
 
well spoken nasDaz!! kudoz. japo maoni kidogo kama ifuatavyo na kwa kukunukuu:-

"Kwamba, ufisadi unafanyika ndani ya mamlaka yako, lakini unashindwa kuchukua hatua na badala yake unabaki kulalama na ama labda kufoka!"

JK na Pinda ni mfano wa viongozi wa aina hii; pacifiers! hata body language yao huwa haionyeshi kama ni mtu amechukia jambo na anataka kuchukua hatua madhubuti kama alivyokuwa Ben mkapa!! tabia ambayo huwa inawaacha mafisadi wakijipa moyo kwamba kwamba "its business as usual;" Mkulu wa kaya hana neno; si umemuona bwana??!!!

"Frankly speaking, ni heri uwe na kiongozi fisadi lakini muwajibikaji kuliko kuwa na kiongozi asiye fisadi na sio mwajibikaji!

ClearlyEd Lowasa fits this description! Ed ameandamwa sana na tuhuma zisizothibitishwa za ufisadi lakini anabaki kuwa kiongozi mwenye ujasiri wa kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia; Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe;

"Kuna mtu kutokuwa fisadi na kuna mtu kuchukia ufisadi!! Wala sina hakika kwamba Mwakyembe sio Fisadi bali lililo dhahiri kwangu ni kwamba Mwakyembe ANACHUKIA UFISADI!!"

Harison hawezi kuchukia ufisadi kisha akawa fisadi; kwa sababu kuwa fisadi kisha akachukia ufisadi ni positions mbili zinazokinzana na kwa hiyo dr. Mwakyembe asingekuwa na moral authority ya kusimama kifua mbele kupambana na madudu ambayo anajua serikali nzima inayajua lakini hawawezi kuyakemea kwa sababu they are also embedded; fuatilia vizuri rekodi ya utumishi wa umma ya Dr. Harrison utamfahamu vizuri na kumtendea haki;

"Kutokana na hayo hapo juu, nashawishika kuamini kwamba Harrison Mwakyembe anahitaji post nyingine zaidi ya hii aliyonayo hivi sasa! Hii ni muhimu kwavile ufisadi ndani ya nchi hii upo kila mahala!"

Dr. Harisson katika mfumo wa utawala bora kamili anastahili awe Rais wa jamhuri au pungufu ya hapo basi awe Waziri mkuu mtendaji (Coordination and Supervision); kwa bahati mbaya wale wanaonufaika na mfumo uliopo wa kifisadi na hujuma ya mali ya umma (Machiavelian conformists) hawako tayari kumuona mtu mzalendo kama Dr Mwakyembe akifika hapo juu! kwa sababu atabomoa mitandao yao ya uhujumu; wako tayari wamtoe roho ili waendelee na ufisadi wao.

Heshima mbele mkuu..........Mwakyembe nafasi anayostahili pungufu yake ni Uwaziri Mkuu.......kama ulivyo-hint hapo juu......watu wakitaka kumfahamu vyema waangalie historia yake........binafsi nilianza kumfahamu vema na uzalendo wake.....wakati wa sakata la kuuza NBC.......watu kama akina Balozi Mpungwe(mastermind wa Ufisadi Tanzania)......Lowassa......hawawezi kuiva na huyu Mwakyembe.........
 
Binafsi nami nilianza kumfahamu wakati alipomwanga manyanga kama mjumbe wa NBC/NMB baada ya kutokubaliana na upuuzi ambao ulikuwa unafanywa na serikali. In fact, hata mimi nakubaliana na wewe kwamba pungufu ya nafasi anayostahili ni Uwaziri Mkuu lakini sikutaka kuitaja hiyo nafasi kwa sababu za wazi kabisa! Nashawishika kuamini kwamba Mwakyembe si mpenda madaraka anayestahili kupewa vyeo vya kama Waziri Mkuu, la hasha! Kuwa PM kwake atakuwa too general wakati kwangu namuona kwamba ndio tiba muafaka ya kupunguza tatizo la ufisadi and ONLY ufisadi. Hiyo ndiyo sababu iliyonifanya nione umuhimu wa kuwa na wizara itakayohusika na ufisadi tu na taasisi zake...hapo ndipo nilipokuja na idea ya Wizara Kuzuia na Kupambana na Rushwa huku ikihakikisha TAKUKURU na part ya DPP wanakuwa chini ya wizara hii. Binafsi naamini tatizo lingine la nchi hii ktk kupambana na rushwa ni TAKUKURU na DPP ambao hawafanyi kazi sawasawa na kwa bahati mbaya hakuna anayewalazimisha wafanye kazi sawasawa.....so, hawa nao wakiwa chini ya mtu anayewatazama kwa jicho la moja kwa moja, then naamini gurudumu litanza kutembea!
 
kaka umenene lakini tatizo siyo watu,

tatizo ni misingi tuliyoiweka kikatiba,

tunahitaji katiba itakayolazimisha uwajibikaji wa kila mtu ikiwa ni pamoja na wananchi

naamini akina mwakyembe tupo wengi sana

tupiganie katiba yenye mifumo bora ya kuwajibisha tusitegemee uwezo wa mtu binafsi, watu wanapita tu.

You're very right....sasa mbona hukuniunga mkono mkono pale wakati napigia debe suala kuwa na Katiba ya Kikatiba?! Anyway, let me talk like this.....ni kweli, katiba ni taizo tena ndio tatizo kubwa msingi!!! Lakini kwa bahati mbaya sana, watu tunazani tukiwa na katiba safi kabisa(of 21st Centuary) then huo utakuwa mwarobaini tosha kabisa! Lakini amini amini nakuambia, katiba yoyote ambayo ndani yake itakuwa na kifungu kinachohubiri Utawala Bora, basi katu katiba hiyo haitaweza kumaliza tatizo la rushwa! Utawala Bora ni tatizo, trust me ingawaje wanasiasa wote including wa upinzani wameingia kwenye mtego huu wa kushabikia utawala bora! The so called Utawala Bora ni kichaka kizuri kwa mafisadi na watu watu wengine wasiofuta sheria. Utawala Bora bora ni kichaka cha watendaji wasiotaka kuwajibika! Na ndio maana viongozi wengi kama sio wote barani Afrika huwezi kuta miongoni mwao anapinga the so called Utawala Bora....hii ni tofauti kabisa na mifumo ambayo mara kwa mara imekuwa ikiletwa na nchi za magharibi! Hawapingi mfumo wa Utawala Bora coz' ni kichaka cha maovu yao! Hapa ndipo tunaposhindwa kuelewa na kuishia kulalama! Watu wanataka leo Lowassa apelekwe Korokoroni kutotkana na kashfa ya Richmond....apelekwe mahakamani kwa ushahidi upi? Utawala Bora hapo unatulazimisha pawepo na ushahidi usio na shaka ndipo apelekwe mahakamani! Na hata ukimpeleka bado ataachiwa tu....labda sana sana atapatwa na hatia la matumizi mabaya ya ofisi na sio ufisadi! Moja ya misingi mikuu kabisa ya Utawala Bora ni Utawala wa Sheria......hili tinalishuhudia Kenya hivi sasa kwamba pamoja na Uhuru na mwenzake kuwa ICC, lakini bado wana haki ya kugombea Urais coz' wale ni watuhumiwa tu....huo ndio Utawala Bora!

So, unapokuja hapa nyumbani....katika nchi ambayo wananchi wake hatuna maadili, so Utawala Bora ni tatizo! Nchi hii wengi ni mafisadi na kilichopo ni kwamba wale ambao hawajafanya ufisadi ni kwavile tu hawajapata nafasi zenye mianya ya ufisadi! Nchi hii ufisadi hauna chama.....wanaonekana CCM ndio mafisadi kwavile tu wao ndio walio kwenye system na wale wanaoonekana wanapinga sana ufisadi ni kwavile tu hawajawa kwenye system! So, hii maana yake ni nini? Mimi mfannyabiashara sina maadili mema.....katibu mkuu wa wizara hana maadili mema....waziri hana maadili mema.....Polisi hana maadili mema....watendaji wa Takukuru hawana maadili mema....Bosi wa TAKUKURU hana maadili mema.....DPP hana maadili mema.....Karani wa Mahakama hana maadili mema....Jaji hana maadili mema.....WAKATI huo huo ili mimi nipelekwe Segerea kwa kosa la kumuhonga Waziri/Katibu Mkuu ni lazima pawe na ushahidi wa kutosha(Utawala wa Sheria....Major Pillar of Good Governance) ambao utapita kwenye channels zote nilizozitaja hapo juu!!!! Unazani nitapatikana na hatia?

So ingawaje nakubaliana na wewe kwamba tatizo ni katiba lakini wala usizani katiba inayohubiriwa na wengi inaweza kutatua tatizo....Katiba inayohubiri Utawala Bora inaweza fanya kazi vizuri kwenye jamii ambayo angalau ina maadili! Jamii ambayo yenyewe tu inafahamu kwamba kutoa ama kuomba rushwa si jambo jema hata kidogo!! Lakini jamii kama yetu inahitaji kushinikizwa kuchukia vitendo hivi......Watanzania si jamii inayostahili kuongozwa kwa Katiba yenye lugha laini na ya kuvutia kama iliyomo kwenye Biblia, kwamba "mwenzako akikupiga kofi shavu la mkono wa kushoto, mgeuzie na shavu la kulia akupige!" Kwenye jamii yetu, ukimgeuzia na shavu la kulia, huko nako atakutandika kofi zito zaidi kuliko lile la awali na ukidondoka chini na kupoteza maisha, Biblia hiyo hiyo inakuruka na kukuambia "Usifanye majaribu kwa Bwana Mungu Wako!"
 
Back
Top Bottom