A New Era in Education, From a Pyramid to a Square Structure

A New Era in Education, From a Pyramid to a Square Structure

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,038
👉🏾Zamani, mfumo wa elimu ulikuwa ni piramidi (pembe tatu),
  1. wengi walianza na elimu ya msingi, baadae sababu kama kukosekana kwa msukumo wa elimu,utoro,mazingira,kufeli waliishia darasa la saba au hawakufika,na wengine walikwenda sekondari walioweza kuhimili hizo changamoto.
  2. walimaliza elimu ya sekondari, na wachache zaidi walifikia elimu ya juu. Mfumo huu ulionyesha wazi pengo kubwa kati ya wale waliopata elimu na wale walioshindwa kufikia ngazi za juu.
  3. Mfumo wa elimu wa piramidi unasadifu kuwa idadi ya wanafunzi ilipungua kadri ngazi za elimu zilivyopandwa. Kwa mfano, wengi huanza elimu ya msingi, wachache wanamaliza elimu ya sekondari, na wachache zaidi wanapata elimu ya juu. ilidhihirisha ukosefu wa usawa katika fursa za elimu.
👉🏾Elimu ya nyakati hizi inatofautiana na ile ya zamani. (Mraba au mstatili), Leo hii, jamii inategemea kwamba kila mtoto anayeanza darasa la kwanza atamaliza darasa la saba na kisha kuendelea na elimu ya sekondari na ya juu,hivyo mabadiliko makubwa katika mtindo wa elimu yameonekana,ambapo lengo ni kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata fursa ya kumaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya juu, bila kujali hali ya familia au mazingira ya mtoto.

Tofauti na mfumo wa zamani wa piramidi, ambapo wengi walishindwa kuendelea na elimu kwa sababu ya vikwazo vya kifedha, kijamii au kimazingira. Mfumo huu wa sasa unalenga kuhakikisha kuwa elimu inakuwa ni haki ya kila mtoto, na kwamba hakuna mtoto anayekosa fursa ya kusoma kwa sababu ya hali yake.

Hivyo, jamii sasa inajivunia mabadiliko haya ambapo mfumo wa elimu unakuwa na upana mkubwa, na unatoa nafasi kwa kila mtoto kufika mbali zaidi. Pia inaashiria kuwa elimu imegeuka kuwa chombo cha usawa na maendeleo, ambacho kinahakikisha kuwa kila mtu anapata fursa ya kutimiza uwezo wake kamili.

CHANGAMOTO ZAKE!.

👉🏾Ingawa watu wengi sasa wanapata elimu ya juu, soko la ajira linazidi kuwa na ushindani mkali. lazima jamii itoke nje ya box
👉🏾Mitaala ya elimu katika nyakati hizi imekuwa butu na isiokidhi mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri.
👉🏾Mfumo wa elimu wa sasa umeshindwa kuwaandaa wasomi wenye uwezo wa kung'amua na kupembua changamoto zinazokumba jamii. Mitaala mingi inajikita zaidi katika elimu ya kinadharia, badala ya kutoa ujuzi wa vitendo na mbinu za kutatua matatizo halisi.

MTAZAMO BINAFSI

👉🏾Napendekeza kwamba VETA iwe ni lazima kwa vijana wote baada ya kuhitimu kidato cha sita kwa angalau mwaka mmoja, ambapo baadhi watajiunga na JKT na wengine kujiunga na VETA,itakuwa ni mikakati ya kuzalisha nguvu kazi yenye ujuzi wa vitendo, kukuza viwanda vya ndani, kupanua soko la ajira, na kupunguza idadi ya wasomi wengi wanaomaliza masomo bila ya ujuzi wa kiufundi na kimatendo. Njia hii itawaandaa vijana kwa ajira au kujiajiri na kuchangia katika uchumi wa taifa.

Pia, ni muhimu kuimarisha siasa safi na kuwa na sera bora za uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa, itasaidia katika kuunda mazingira bora ya biashara, kuongeza ajira, na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

In conclusion, a well-rounded education system, combined with practical skills training and sound policies, is key to fostering a skilled workforce, driving economic growth, and ensuring a prosperous future for the nation.
 
umenena vyema ndugu,hasa hapo kwenye veta iwe lazima kwa waliomaliza cha kidato cha nne wakasome ujuzi mwaka mmoja mara tu baada ya mtihani wa kidato cha nne ,Veta nao waongeze wigo wa kozi zao isiwe zile common ili kila mwanafunzi anaeenda Veta akajifunze kile anachohisi ni kipaji chake,baada ya matokeo .Hicho cheti cha veta kwa wale walioishishia kidato cha nne basi kitumike kama equivalent na added advantage kujiunga level Two ya veta,.NACtevet nao pia wasiishie kujiunga na Veta kiutawala bali kivitendo zaidi ,mfano unakuta kozi nyingi zinazotolewa na veta zinaishia Level 2 kwenye vocation Award hazina mwwndelezo wa National technician award NTA hivyo unajikuta mwanafunzi anaona atasomaje kozi ambayo haina ubobezi huko mbele ,ni rai yangu kwa wadau wa elimu kuacha mazoea na kubadili mfumo wa kielimu unaoendana na uhalisia.
 
👏
 
Back
Top Bottom