A monkey Cant be judge in its own forest

A monkey Cant be judge in its own forest

Mtu wa Asali

Senior Member
Joined
May 9, 2022
Posts
149
Reaction score
292
Ni dhahiri kwamba, mchawi wa mdororo wa uchumi kwa awamu ya tano uliasisiwa na msimamizi mkuu wa shughuli za Serikali, tulikuwa na nchi yenye kukuza deni la taifa kuliko uchumi wenyewe kama msimamizi wa shughuli za serikali alikosa mbinu za kukusanya kodi awamu ya tano kwa awamu ya sita mbinu hizi anazipata wapi kama awamu ya tano alishindwa kuna lipi kwa msimamizi wa shughuli za serikali kwa awamu ya sita.

Hatuwezi kuwa sehemu ya watu walioshindwa mara mbili waswahili wana msemo mtu mzima hadanganywi mara mbili awamu ya tano uwezo wa ukusanyaji wa kodi uliporomoka na deni la taifa liliongezeka kwa 22% tukiwa na msimamizi wa shughuli za serikali huyu huyu Serikali hiyo pia iliendelea kumwagilia na kupalilia ukuaji wa deni la Taifa.


Alishiriki kuficha madeni kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kupitia ofisi ya msimamizi mkuu wa shughuli za serikali ndiye muhusika mkuu wa kusimamia uhifadhi wa mifuko ya taifa iweje akae kimya Kutotambua madeni haya kwenye Deni la Taifa jambo linaloiweka mifuko ya hifadhi ya taifa kuwa hatarini. Kuletwa sheria za mafao ilikuwa ni janja ya kutochangia au kutoa mafao kwa wastaafu pale pesa zinapohitajika. Hadi leo kunasababisha wastaafu wengi kuhangaika bila kulipwa mafao yao kwa muda mrefu. Rais samia usikubali kuwa mnyonge msimamizi wa shughuli za serikali ni kichwa cha nyoka akibebi mtungi.

Aliyeondoka Tanroad ni mtendaji mkuu kwa namna TANROADS na watu waliokuwa Wafanyakazi wa TANROADS walivyohusika na miradi mbalimbali nchini, kwanini msimamizi mkuu wa shughuli za serikali asifanye uchunguzi maalumu wa Genge la TANROADS? Haiwezekani mtu mwenye wadhifa kama huu katika nchi kuwa kibiriti fitina.

Unasikia eti PCCB itachunguza eti Polisi itachunguza its childish, kwamba mtu unasubiri kuambiwa kufanyia kazi ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali? Ripoti ya CAG imeonyesha katika awamu ya tano kulikuwa na ubadhirifu mkubwa wa matumizi ya fedha za Umma.

Majibu yote ya matumizi ya serikali ya awamu ya tano yanajibiwa na msimamizi mkuu wa shughuli za serikali. Kwanini amekaa kimya. Ripoti ya mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali ametuonyesha wazi jinsi awamu ya tano ilivyoshindwa kufanya kazi. Collective responsibility za serikali ni majukumu ya msimamizi wa shughuli za serikali.

Tuombe Rais kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kujenga mifumo madhubuti ya Uwajibikaji na kuimarisha Taasisi za Uwajibikaji. Bila Taasisi Imara Nchi yetu haitaweza kupiga hatua kubwa za Maendeleo.
 
Aya ya mwisho ndio imebeba kila kitu....bahati mbaya sana wapingaji wa hilo wameshabuni mbinu kali sana ambayo inafanya kazi ya uchawa. Utasikia Mama kafanya hivi na vile,...mara maandamano ya kumpongeza mama...hii yote ni kuua ile mifumo ili abaki mtu na chawa waendelee kunyonya nchi. SHAME ON US ALL!
 
Back
Top Bottom