A free HIV/AIDS generation ... begins with you

Junior. Cux

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2011
Posts
5,319
Reaction score
3,798
Nimeona tukumbushane mambo muhimu kidogo katika jumapili ya leo. Taifa bila virusi vya ukimwi inawezekana, jitahidi kufanya haya:
  • Tumia kinga kila mara unapokutana kimwili. huwezi kumjua muathirika kwa kumuangali, wala usimuamini mtu kwa macho kwa vile kasema yuko vizuri, matumizi ya kinga yanaweza okoa maisha yako kwa kiasi kikubwa.
  • Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu. baadhi ya watu hawafurahii tendo wakitumia kinga either kwa michubuko au maumivu, ni vema ukatafuta mpenzi mmoja muaminifu mtakaeweza kushiriki nae.
  • Acha kujamiiana. kama hujapata hata mmoja mwaminifu basi ni vizuri ukasubiri na kuacha kushiriki tendo mpaka pale utakapofanikiwa kumpata.

Sio mbaya tukaelezea changamoto mbalimbali tunazokutana nazo katika jitihada za kujikinga na ugonjwa huu na jinsi gani tunaweza kukabiliana nazo, ushauri wako leo unaweza kuwaokoa mamilioni ya watu siku za mbeleni.

sharing is caring....
 
Mtoa mada umeniangusha sana..
Ila umezungumzia suala muhimu mno !
Ningefurahi kama ungetuamsha pia kwamba..
JAMBO LA MSINGI LA KWANZA NI KUJITAMBUA KWA KUPIMA HIV..
BAADA YA KUIJUA AFYA YAKO NDIO UENDELEE NA HATUA NYENGINE..
unakua na mpenzi mwaminifu lakini ushaathirika hujijui,ni sawa na sifuri..
mnatumia kondom kumbe nyote wagonjwa,ni afadhali mngewahi ARV kuliko kukimbilia kondom..
Unapojijua afya yako utawaokoa na wengine..
 

Asante kwa kukumbushia, hapo pa muhimu zaidi...
 
Jitahidi kuweka kinga karibu hata stimu zikishapanda iwe rahisi kuikumbuka..

Baadhi ya watu wanapata maambukizi ilhali kinga wanazo mifukoni lakini genye zikipanda wanasahau kutumia
 
Jitahidi kuweka kinga karibu hata stimu zikishapanda iwe rahisi kuikumbuka..

Baadhi ya watu wanapata maambukizi ilhali kinga wanazo mifukoni lakini genye zikipanda wanasahau kutumia

Sure kabisa... na ionekane kawaida mtu kutembea na kinga kwenye wallet/pochi, maana ukionekana umebeba baadhi wanakufikiria sio.
 
Linda wengine...Usisambaze ukimwi makusudi
 
Kidumu chama cha michepuko....

Tukumbuke kutumia kinga jamani....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…