Kama nilivyoona vilikuwa ni viungo vya maiti halisi za vichanga na watu wazima wale watu hawafai kuishi duniani......
.........
Ilifika muda wa ibada nikachukuliwa kwenda huko underground floor, kulikuwa kunatisha mno nikakaa sehemu ya wageni kwa juu kidogo kabla ya holini
Hall lilikuwa kubwa lililopakwa rangi nyeusi na taa zilikuwa nyekundu sana zenye mwanga mkali, madhabahu MSALABA wake uliangalia chini na kulikuwa na jeneza lililofunikwa kutambaa chekundu
Ukumbi ulikuwa na watu wasiopungua hamsini hivi wote wakiwa uchi wa mnyama,ulianza mziki wa heavy metals wenye sauti za ajabu mno kama zile za kuzimu
nina swali hapa......
1.msalaba uliangalia chini kivip?kwamba uligeuzwa chini juu au??
2.watu hao walikua jinsia zote 2?
3.kulkua na wageni wangap labda?kwa makadirio!
I see we mshana jr kiboko. Haya mambo ni kweli au chai?
MSALABA uligeuzwa chini juu
Watu walikuwa jinsia zote
Mgeni nilikuwa pekeyangu nikichungwa na mwenyeji mmoja
Nidanganye ili iweje sasa? Kwenye mada nyingi tu niliongelea kuwa niliwahi kusali kanisa la waabuduo shetani lakini sijawahi kuweka habari kamili in details kama hivi...natumia ID halisi sina sababu ya kuongopa
Na hii story kwangu sio valid tena kwakuwa haya mambo yalitokea miaka almost 18 iliyopita
Temple tour na safari ya kwenda kuhudhuria ibada ya waabuduo shetani
Chuo chetu kila Jumapili kilikuwa kinapokea wageni wengi sana kutoka maeneo tofauti ya South Africa... Wengi walikuja temple kwa ajili ya ibada za chanting, meditation, masomo ya Buddhism lakini pia temple tour
Mimi nilikuwa mmoja wa ma tour guide, kazi ambayo niliipenda sana
Siku moja Jumapili mchana tukiwa karibia kabisa kumaliza shughuli za temple walikuja wazungu wanne wakiwa kwenye mavazi meusi full kuanzia miwani mpaka viatu
Wenzangu walikataa kuwahudumia lakini mimi nikakubali hivyo nikawachukua temple tour, wakawa watu wa maswali mengi sana kiasi kwamba tour iliisha karibia saa kumi na moja jioni
Baada ya tour ile ambayo waliipenda sana wakanipa ofa ya kwenda kwenye synagogue lao lililoko mji wa New Castle, mwendo wa zaidi ya masaa matatu toka chuoni, na kwamba nao wangependa mno nione ibada zao na usiku ule kulikuwa na ibada kubwa
Mpaka leo sijui ninini kilinifanya nikubali kwenda, tena kwa kutoroka kwakuwa nisingeruhusiwa katu na uongozi wa chuo
Nilicheza michezo yangu baada ya dinner na saa moja kasoro nilikuwa njiani kwenda New Castle na wale jamaa kwenye Cadillac jeusi tii, kuhudhuria ibada nisiyojua
Tukafika mwendo wa saa tatu usiku hivi nakumbuka huko njiani tulichepuka na kuingia rough road ya msitu na mashamba kwa zaidi ya nususaaa hivi
Kama kuna siku nilifika kuzimu basi ilikuwa siku hii, mbele yetu kulikuwa na jengo refu jeusi tii likisimama gizani ndani kulikuwa na taa za rangi zilizofifia
Jengo lilikuwa refu la grorofa tatu
Aisee kumbe ni mda mrefu ilitokea. Hivo vichanga walikua wanafanya nini. Pia naskia ibada zao hugeuza msalaba kwanini hawaweki uangalie juu. Na je mtu akitamka jina la Yesu inakuaje?
Sasa na wewe ulivyokuwa kwenye hiyo temple ulikuwa uchi wa mnyama au ulikuwa umevaa mavazi gani na ni mavazi gani mnatakiwa mvae!?
Usithubutu hutoki mzima, wanageuza msalaba kama ishara ya mpinga kristo
Mkuu nimejikuta navutiwa na uzi wako maana napenda kusoma sana hizi mambo. The word is full of secrets you can not understand them all. Learn them slowly. Hivi ndivo DAN BROWN anasema. Nimejikuta nasoma vitabu vya jamaa sana kama vile DA VINCI CODE. FORTRESS. ANGELS AND DEMONS N.K
sasa mkuu umeshaandika kitabu chochote kuhusu hili unaloliongelea?
Kama hutojali naomba uniPM plz
mshana jr hujamjibu Diva Beyonce swali lake apo.......anauliza vichanga huwa wa kazi gan??Usithubutu hutoki mzima, wanageuza msalaba kama ishara ya mpinga kristo
Mimi nilikuwa mwalikwa nilikaa juu kama kwenye balcony hivi nikiangalia kwa chini kilichokua kinaendelea
Hahhahaaaaa no never ni total celibacy life(maisha kamili ya useja)