A Blessing in Disguise? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

A Blessing in Disguise?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kamanzi, Dec 12, 2011.

 1. k

  kamanzi Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Japo wengine kila kukicha hawaachi kupiga kelele kuwa CCM na JK wanainyonya Tanzania mie nacheka mpaka jino la mwisho. YES, najua JK ndiye mmiliki wa Richmond na DOWANS kama Lowassa alivyotueleza; najua pia katika kusherehekea miaka 50 ya umaskini serikali imefuja bilioni zaidi ya 60, na mengine mengi tu.


  Kila nikiangalia hivi najiuliza hivi ni laana au baraka kwamba matukio haya yanaendelea Tanzania. Mimi naamini ni baraka maana CCM na JK wapo madarakani kwa upuuzi wa watanzania waliowapigia kura. Hata kama aliiba kura, aliyefanya actual stealing ni maskini mwenzangu wala sio JK na mkewe Salma.

  My gut feeling inaniambia watanzania watabadilika only if watanyonywa hadi damu ya mwisho vinginevyo ubwabwa tu na tisheti za CCM zitawafanya waipigie CCM. Naomba Mungu JK azidi kudhulumu hasa wale wanaorubuniwa na kofia na tisheti za kijani na manjano ili ifikapo 2015 wageuke na kuona kuwa CCM ni shetani linalotakiwa kutokomezwa tanzania.

  In the meantime, JK kula uvimbiwe. Ufisadi unaofanya ndio utafungua macho wadanganyika siku moja. Kula wala usimbakishie baba kama tulivyokuwa tukicheza zamani.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  taifa ambalo limejenge uadui na Mwenyezi mungu kama letu Mwenyezi Mungu huliachia lipate shida na manunguniko mengi ili hatimaye limjue Muumba............................................na kuacha dhambi
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Kamanzi, hilo la Richmond kumbe umeona ehee...!. Sasa hiyo ndio passport ya EL kuingia Ikulu!. Tena atatumia vifungu vya vitabu vitakatifu kuwa Yeye ndiye yule Mkombozi ulioahidiwa na Mungu baba kufuatia mateso makubwa yaliyosababishwa na mwovu shetani!.

  EL, atawathibitishia Watanzania kuwa CCM siyo mbaya, bali kibaya ni JK na mtandao wake dhalimu!. Naye atatupikia pilau ya mlo wa shibe ya siku moja, pia zaidi ya t-shirt na kofia, yeye ataongeza kanga na mtandio!. Amini nakuambia 2015 tutawapa tena!.

  Mungu ibariki Tanzania!.
   
 4. k

  kamanzi Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Yani Pasco wadanganyika wakiwapa tena CCM, ndo nitaacha kabisa kuwaonea huruma kwa ujinga wao. Huwezi kuchagua wahuni halafu wakifanya uhuni ulalamike kwanini wanaufanya. Kaimani kangu kadogo kalikobaki kanawekwa na theory kwamba watu wakiminywa vya kutosha juwa wanashtuka. Si unaona warusi wamemgomea Putin na matokeo yake ya uchaguzi. Wale wamebanwa mpaka wamechoka. Kama Chinua Achebe alivyosema, 'they have stolen enough for the blind to see", naamini brotherman JK akizidi dhuluma watanzania watapona upofu. Ila Mungu apishe mbali isije kuwa watanzania wanaugonjwa ule wa ESAU kwamba wanauza haki ya uzaliwa wa kwanza kwa MLO mmoja. Kama ndivyo, tumekwisha.
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,626
  Likes Received: 4,729
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakubaliana na wewe kabisa hata mimi naomba gharama ya maisha ipande hata mara elfu kwa kuwa wabongo ni wagumu kujifunza mpaka mambo yawafike ndiyo watatia akili. Kusema kweli kwa jinsi CCM ilivyoifukarisha nchi hii nisingetegemea mtu mwenye akili timamu ambaye si mnufaika wa ufisadi unaofanywa na watawala aiunge mkono CCM. Lakini hadi leo hii kuna watu wanaona CCM kama ni mkombozi wao. Wacha JK na genge lake waendelee kuifisadi nchi kwa kwenda mbele na wadanganyika wazidi kuumia. Umeme unapanda kwa 155% hiyo naona ni ongezeko dogo sana ningependekeza ongezeko la 1000%
   
Loading...