Kwa waafrika asilimia kubwa tunaishi kwa kusaidiana na pengine hapo ulipofika uliwezeshwa kwa namna moja au nyingine!!!! Na pia hata mzazi wako inawezekana alisaidiwa au aliwezeshwa mpaka wewe kufika hapo hapo ulipofika.
Huwa nashangaa mke au mume kukataa kusaidia ndugu wa mwenza wake au hata marafiki pale ambapo uhitaji unahitajika!!!! Huku uwezo wa kusaidia anao..... Na hapo anasahau pengine baba au mama kawezeshwa sana misaada sana mpaka yeye anafika wakati wa kuweza kusimama mwenyewe.,.,..
Nitawezesha na kusaidia kadri ya uwezo wangu na sitatupa mtu.