Wakristo wa kweli wanasikitika kila roho inapopotea, hasa roho ambayo ilikuwa bado haija kiri kuwa YESU NI BWANA. Kwa masikitiko makubwa, napenda kuungana na wote wapenda amani kulaani kitendo hicho, na tunawapa pole wote waliofikwa na msiba. Tunazidi kusisitiza kuwa "HAKUNA NA HAKUTAKUWA NA GHASIA YOYOTE, BAINA YA WAKRISTO WA KWELI, NA WAISLAMU WA KWELI" yote tunayoyaona ni kati ya mashabiki wa Wakristo na mashabiki wa Waislamu, wale ambao maskini hawajui hata makanisa wala miskiti imeelekea wapi???? Poleni sana. Wakristo wote wa kweli Tunaungana katika kulaani machafuko yanayoendelea kote nchini, nasi tutazidi kumlilia Mungu, arejeshe roho za wote wasioijua kweli, pamoja na kuzifunga nguvu za kuzimu ili wote wanao hubiri na kuandaa mauaji na machafuko hayo, washindwe katika jina la YESU.