Nimenunua T-SMART ya tigo, mpaka sasa nimegundua yafuatayo kwa simu hii:
1. Kasi yake ya internet (ukitumia wi-fi) ni nzuri, video za youtube zinacheza vizuri bila kukwama.
2. Whatsapp inafanya kazi vizuri tu, ila haisapoti document messages (doc, docx, xls, pdf e.t.c.).
3. Unaweza kuimport majina (contacts) toka google account (gmail) na kuyahifadhi kwenye simu yako. Ila kama smartphone yako inahifadhi namba kwa nafasi (mf. 0741 234 567) utalazimika kuhariri kwa kuondoa nafasi hizo (mf. 0741234567) ili uweze kufanya mawasiliano.
4. Ni simu yenye ram ndogo (512 MB), ukiibebesha mzigo mwingi (matumizi makubwa) inakuwa na tabia ya kufreeze.
5. Ina mobile hotspot (unaweza kushare internet na vifaa vingine kama pc au smartphone).
6. Ina uwezo wa remote lock/unlock na find device kama smartphone za kawaida.
7. Ni simu ya line mbili, line ya kwanza (SIM1) lazima iwe ya tigo.
8. Slot ya line ya kwanza (SIM1) ndo yenye uwezo wa H+/4G, line ya pili (SIM2) ina uwezo wa 2G tu.