40 mbaroni kwa kuuza ardhi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
40 mbaroni kwa kuuza ardhi


na Julieth Mkireri, Pwani


amka2.gif
JESHI la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa zaidi ya 40 wanaodaiwa kuhusika katika zoezi zima la kuvamia na kugawana ardhi kinyume cha sheria wilayani Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Polisi mkoani hapa Absalom Mwakyoma alisema baadhi ya watuhumiwa hao tayari wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma na wengine kesi zao zinafanyiwa uchunguzi ili sheria ichukue mkondo wake.
Mwakyoma alisema watu hao wamekuwa wakivamia ardhi ambazo tayari zina wamiliki halali huku wao wakidai kuwa mashamba hayo ni pori kisha wanakusanyana na kugawana kinyume cha sheria tena kwa bei nafuu.
Aidha alisema wahusika wakuu wa zoezi hilo la kujigawia maeneo ni pamoja na wenyeviti wa mitaa na vijiji na viongozi wengine wa serikali za mitaa jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu wa kumiliki ardhi.
“Kinachonikera mimi ni mtu au kundi la watu kutochunguza kwanza ardhi wanayotaka kugawana inamilikiwa na nani…badala yake wao wanavamia tu na kuitana kugawana kiholela bila utaratibu wowote wa kupata ardhi hizo,” alisema Mwakyoma.
Maeneo ambayo yamevamiwa na watuhumiwa hao ni Mapinga, Kerege na Vigwaza wilayani Bagamoyo. Mengine ni Kitomondo, Visiga Mbwawa na Miswe wilayani Kibaha, ambapo watuhumiwa wanadaiwa kutokea jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Bunju, Kigamboni na Kibamba, Kimara na Mbezi.
Hivi karibuni serikali ilikemea suala hilo na kuwataka watu wanaojihusisha na uvamizi wa ardhi za watu kufuata sheria na taratibu za kumiliki ardhi na sio kuvamia kiholela.
 
Mwanzo mzuri wa kujisafisha kwa jeshi la polisi............................................
 
Back
Top Bottom