3D max na Blender

3D max na Blender

Nitaanza na ukweli mdogo kisha ntamalizia na ukweli mkubwa.

UKWELI MDOGO (Ni ukweli lakini)
3Ds Max (3D Studio Max)

  1. Ni rahisi zaidi kujifunza kuliko Blender. Blender inalalamikiwa kwa interface ambayo si "standard" kwa programu nyingi za 3D, hata hivyo imezidi kuboreshwa sana hivi karibuni. Kwa kifupi 3Ds Max ni rahisi zaidi.
  2. Ina plug-ins nyingi sana na ndiyo programu ya 3D inayodaiwa kuwa na watumiaji wengi kuliko zingine. Hili linasababisha pia iwe na tutorials nyingi sana katika mtandao.
  3. Inauzwa bei ghali sana.

Blender
  1. "Huenda" imekamilika zaidi kuliko 3Ds Max. Blender imetengenezwa ili ijitegemee kadiri iwezekanavyo na ndiyo sababu inafanya vitu vingi kuliko Max. Inafanya ufinyangaji (sculpting) kitu ambacho 3Ds Max haifanyi. Ina fluid simulation, nadhani Max haina ama ni dhaifu hapa. Inafanya compositing (node-based kama Nuke ama Fusion), Max haifanyi.
  2. Ina watengenezaji wengi (developers) hivyo inafanyiwa maboresho ya mara kwa mara na sitoshangaa itakapofikia kuwa ndiyo programu bora kuliko zote. Hatujui lini lakini.
  3. Ni bure, haiuzwi.

UKWELI MKUBWA ZAIDI

  1. 3D animation kwa ujumla ni taaluma inayohitaji muda, nguvu na moyo ili kuweza kujifunza na kuifanya.... well, inategemea unataka ufikie kiwango gani. Hii ina maana programu ni nyenzo tu ila 3D animation ni sanaa... kuijua programu si tiketi pekee ya kumfanya mtu afanye kazi nzuri.
  2. Hata kama mtu atasema 3Ds Max ni bora kuliko Blender ama Maya ni bora kuliko Lightwave 3D ama Cinema 4D.. si kweli kiviiile. Programu zote ambazo ni professional level zina uwezo mkubwa, ndiyo maana zote zina historia ya kutumika katika projects kubwa Hollywood na sehemu zingine duniani.
  3. Programu za 3D kwa kawaida zinahitaji kusaidiana na zingine kama Photoshop, Nuke, After Effects, Fusion, Combustion, Maya Composite, Mocha, Syntheyes (au 3D tracker yoyote), RealFlow n.k. ili kukamilisha baadhi ya kazi. Utalazimika kujifunza programu zingine pia (baadhi), CHANGAMSHA BONGO.
  4. Summary....Programu ni nyenzo tu, UBORA WA KAZI NI SANAA ya mtu mwenyewe.

Kila la heri.
 
Back
Top Bottom