Hapo kuna walakini sio siri, navyojua hio concept ya bits iwe 32/64 inatokana na kitu kinaitwa data bus zilizopo katika mfumo wa computer. Kazi ya data bus ni kusafirisha taarifa (data) kutoka katika eneo moja kwenda jingine ndani ya computer aidha toka kwenye Ram kwenda kwa Cpu n.k. Bus ni mkondo unaobeba hizo data.
Data ni taarifa yoyote isio rasmi yaweza kuwa tarakimu,herufi ama alama za kiuandishi. Hizi data huwa na vipimo maalum kitaalamu navyo tulianzia bits, bytes, kilobytes, megabytes, gigabytes na sasa naona tumekwishafikia terabytes katika matumizi yetu ya kawaida.
Tukija kwenye swala la mtoa mada, wanaposema 32bits ama 64bits ina maana kwamba kompyuta husika ina mkondo unaowezesha kusafirisha kiwango cha taarifa yenye ujazo wa 32bits vivyo hivyo huwa kwa 64bits. Ukitazama haraka utaona kwamba 64bits ni mara mbili ya ile 32bits hivyo 64bits inakuwa bora zaidi.
Applications zake katika matumizi ya kompyuta ni kwamba kunakuwaga na softwares ambazo ili kuweza kuzitumia zinahitaji teknolojia ya usafirishaji wa taarifa uwe kwa kiwango cha 32bits na zile zinazodai 64bits. Hivyo nzuri ni kuwa na komyuta yenye kiwango cha 64bits maana itakupa nafasi ya kutumia hata softwares zitazohitaji kiwango cha chini ambacho ni 32bits kwa sasa!