King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 64,122
- 98,520
Wabunge ndio wanajipangia wajilipe sh ngapi.
Wabunge ndio wanajipangia wajilipe sh ngapi.
Si kweli kwamba wameridhika na wanachopewa isipokuwa hawa ni watumishi wa umma wenye mshahara kiduchu hivyo Hali ngumu ya Maisha wafanye nini!? Hawana pa kusema! Ajabu posho za serikali zimewekwa kwa viwango vya mahali na mishahara, sasa hiki ni kiwango cha wapi!? Wengi wao ni walimu. Shuleni watoto hawana walimu!
Kuna mkakati unaendelea wa kustandadize mishahara na maslahi ya watumishi wa serikali na agencies zake zote. Naamini hili likifanikishwa mambo yatakuwa mazuri. But kwa sasa hali ilivyo si haki kabisa.
Sasa si uwaambie waache kuandikisha wapiga kura na wao wakaandike katiba.
Hapo ninapoandika taarifa hii,niko kwenye foleni ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.Mkoa ni Dodoma wilaya ya Dodoma mjini kata ya Kikuyu Kaskazini.
Tukiwa tunasubiri zamu yetu ya kujiandikisha,kuna mdau amenidokeza hawa jamaa wanaoandikisha wapiga kura, wanalipwa sh 15,000 kwa siku na maboss wao wanalipwa sh 20,000 kwa siku!
Ninachojiuliza,inakuwaje mtanzania mmoja alipwe sh 300,000 kwa siku akiwa pale mjengoni akituandikia katiba, alafu mtanzania mwingine alipwe sh 15,000 kwa siku kwa kazi ya kuandikisha wapiga kura wakati serikali ni moja?
Kama taarifa hii ni ya kweli,basi tabaka la walionacho na wasionacho litazidi kuongezeka kasi siku hadi siku.
Sasa si uwaambie waache kuandikisha wapiga kura na wao wakaandike katiba.
Haya yote wakuu yanaenda kumalizika OCT. 2015. Wait and see
ninakuona unavyosahihisha kiswahili nikajua unakitu upstairs kumbe ninakoseaSasa si uwaambie waache kuandikisha wapiga kura na wao wakaandike katiba.
Yatamalizika vp?
Tusifanye makosa tuwaweke madarakani viongozi wenye imani na sisi walalahoi. Wasiwasi wangu kama atatokea miongoni mwa watangaza nia mwenye sifa hiyo.