3 wanusurika kifo ajali trekta..

3 wanusurika kifo ajali trekta..

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Watu watatu wamenusurika kifo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara baada ya trekta walilokuwa wamepanda kukatika tella na kuanguka.

Tukio hilo limetokea kata ya Namelock Wilayani Kiteto wakati watu hao wakitoka shambani kwenda Kata ya Dongo.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumain Magesa akizungumza na majeruhi hosp ya Wilaya ya Kiteto pamoja na kuwapa pole ametoa wito kwa jamii kutotumia trekta kama chombo cha usafiri.

Maeneo mengi Wilayani Kiteto yanatumia trekta kama chombo cha usafiri kubeba abiria na mizigo hivyo wamiliki na madereva hao wametakiwa kutopakia abiria kwenye tella.
 
Daaaaah pole sana ndugu mlionusurika na ajali hii kwa kweli trekta si chombo cha kusafirishia abiria please tupandandeni magari basi tax na magari mengine ya kusafirishia abiria
 
Daaaaah pole sana ndugu mlionusurika na ajali hii kwa kweli trekta si chombo cha kusafirishia abiria please tupandandeni magari basi tax na magari mengine ya kusafirishia abiria
Tax unapandia wapi Kiteto mzee baba ? Hayo mabus yenyewe yapo ya kuhesabu
 
Back
Top Bottom