25.04.2013 Ruvu Shooting Vs Simba SC

25.04.2013 Ruvu Shooting Vs Simba SC

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
"Head to head"

25.04.2013 16:00
Ruvu Shooting Vs
Simba SC

23.09.2012
Simba SC 2-1
Ruvu Shooting

15.04.2012
Ruvu Shooting 0-1 Simba SC

19.10.2011
Simba SC 2-0
Ruvu Shooting

09.03.2011
Ruvu Shooting 0-1 Simba SC

15.09.2010
Simba SC 2-1
Ruvu Shooting
===
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara, timu ya Simba leo itakuwa na kibarua kigumu! Ítakaposhuka dimbani kukipiga na Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi kuu ambayo
inatarajiwa kuwa na
ushindani mkubwa
kwani Simba
watakuwa
wakipigania ushindi wa pointi tatu ili kuwa katika orodha ya timu tatu bora...
===
Kocha wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa ametabiri kuwa mchezo dhidi ya Simba utakuwa mgumu na wenye kila aina ya ushindani, ingawa ametamba kushinda.
Simba ambayo imechemka kutetea taji lake la ubingwa wa ligi msimu huu, leo Alhamisi itakuwa kwenye kibarua kigumu kuvaana na Maafande hao, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkwasa alisema jijini Dar es Salaam kuwa vijana wake wamefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo na kuahidi ushindi.
"Tumepata muda mzuri wakujiandaa na mchezo wa Simba. Pia, hali za wachezaji wangu wote ni wazima wa afya."
"Simba ni timu nzuri, nimewaona wakicheza katika mechi tofauti. Wana vijana wenye kasi na uzoefu na ligi."
"Lakini kwetu hilo haliwezi kututisha na kucheza bila malengo ya ushindi." alisema Mkwasa ambaye alijiuzulu kukinoa kikosi cha timu ya Taifaya Wanawake Twiga Stars.
Kocha huyo alieleza kuwa mchezo huo utakuwa mkali na wenye ushindani kutokana na timu zote mbili kuundwa na vijana wenye vipaji vya soka na kasi uwanjani.
Simba inashika nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi 37 wakati Ruvu akiwa na pointi 30 na kukamata nafasi ya saba kwenye msimamo huku kila moja ikiwa na michezo mitatu mkononi.

CHANZO: SD SPORTS
african-lion-male_436_600x450.jpg
 
kama ni taifa jkt wanafungwa ila ingekuwa mabatini wangeisoma simba..
 
===
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara, timu ya Simba leo itakuwa na kibarua kigumu! Ítakaposhuka dimbani kukipiga na Ruvu Shooting
sijaelewa chochote hapo kwenye red,kivipi ni mabingwa watetezi wakati tayari wameshavuliwa huo ubingwa wao na wanaume wa Jangwani?
ebu acheni masiala ya kuandika kauli tata
 
Simba anaweza akamaliza Ligi akiwa wa 5.
 
wakuu hakuna JF member kwenye jukwaa la sport alioko Taifa kuangalia game?
mbona hakuna updates na jukwaa limepooza sana,au wengi mnasubiri mei mosi?
 
Mechi haipo imehairishwa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom