2026: Ikukumbushe

2026: Ikukumbushe

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
467
Reaction score
691
Unapo omba msamaha, ikukumbushe kuwa, waliokukosea katika makosa yao, nao wanastahili kusamehewa; usiwahukumu!

Unapo omba msaada, ikukumbushe pia wanaoshindwa, katika udhaifu wao wanastahili huruma; Usiwadharau!

Unapo omba kusitiriwa, ikukumbushe pia walio kwenye fedheha, katika aibu zao, nao wanastahili staha; usiwacheke!

Kupenda kusamehewa makosa yako bila kusamehe wengine, kupenda kuhurumiwa madhaifu yako bila kuhurumia wengine na kupenda kusitiriwa aibu yako bila kuwasitiri wenginge ni kizuizi kikubwa cha kupokea baraka kutoka kwa Mungu.

2026 nitawasamehe walionikosea, nitawahurumia walio dhaifu na nitazisitiri aibu za wengine wasipate fedheha.

SOMO: Mathayo 18:23-35
 
Napenda sana kusamehe ila uwa sisahau wabaya wangu ni hapo nimeamua kutokusamehe kabisa .

Kama hapa kuna mzee jirani niliivana naye sana mwaka jana yeye na familia yake ila nimesikitika krismqsi na mwaka mpya zimepita pasina hata karibu nyumbani siku za sikukuu na wanajuq fika sina hata wa kumipikia .kiukweli limeniuma na nimeamua kuwakasirikia na kutowasamehe kwa uchoyo wao .

Juma zima hili anapiga kuomba tuonane spokei na kwake sitaenda tena kwa amani ya moyo wangu
 
Back
Top Bottom