voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,943
"Ni aibu mbunge anaposimama bungeni na kushangaa..eti ni kwa nini hakuna hata waziri wetu mmoja anayemiliki hata ndege moja nchini?" Je, kwa pato lipi kama sio kuusifia wizi,ufisafi na ubadhirifu wa pesa za walipa kodi wa Tanzania?
Ni kweli, tumekwisha yaona madhara ya wahuni ndani ya siasa na serikali,kupitia ripoti za CAG!
Hivyo ni wakati muafaka kuwakataa kwa vitendo,bila kumung'unya maneno!
Tumeyaona pia majigambo ya walipa visasi kupitia press release na vitabu uchwara vya vibaraka wao!
Ni wakati muafaka wa kuwakataa bila kuwaonea haya hawa mabaradhuli!
Na sasa tunayaishi madhara yao mitaani kwetu, kote nchini. Wananchi mnapaswa kujitetea kulingana na mnachokipitia,mkisubiri wasakatonge wa kisiasa,itakula kwenu milele!
Tumeisha yaona majigambo ya baba za wahuni mpaka kwenye vikao nyeti vya chama chao!
Wakijisifu kwa utamu wa kulamba asali,hadi wanaulizana...ni nani halambi asali kwa sasa?
Na kweli Hadi Ba*la amelambishwa asali na kuikacha ile klabu pendwa ya "visimbuzi" chezea asali wewe!
Na tunayaona madhara ya walamba asali kote mitaani kwetu! Amkeni hiyo 2025 myakatae hayo madhara kupitia vidole vyenu na midomo yenu,kwa kauli na vitendo!
Pamoja na kuitwa "mambuzi" na mgeni mualikwa kutoka Mesopotania! Bado mwenye kistuli wetu, aliwaamuru.."kila Mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake!"
Na kweli wamekula urefu wao na kuumaliza,na mwenyekiti amekuja shtuka pale alipokuta wameingilia hadi karibu na bustani yake,ndio akajitahidi kuwaambia wahuni ...enyi "Stupid"
Ukweli ni kwamba neno stupid,lingesaidia kama lingetamkwa kabla hawajaiba,ila kwa sasa linakosa nguvu, maana wanalifurahia huku wakigongeana glasi za mvinyo wakati wakipongezana baada ya kuiba! (ushahidi ni ripoti ya CAG).
Wale mliopo kwenye fungate la asali kwa sasa,najua mtakalosema ila wananchi nao wanalo lao mioyoni ndani ya vifua vyao.
Tanzania sio mali ya koo fulani teule pekee,bali ilistahili kumnufaisha kila mtanzania kwa sababu hatukuchagua kuitwa watanzania!
Bali ni watanzania kwa sababu hapa ndipo tulipozaliwa kwa maamuzi yake mwenyezi Mungu. Na sio kwa hisani ya wanasiasa wasakatonge!
#Kataawahuni[emoji818][emoji419]
[emoji116]