2025 CHADEMA msisuse

Mubby777

JF-Expert Member
Oct 17, 2018
1,638
5,643
Mimi sio mbobez wa siasa ila ninachokiona kwenye Chama changu cha Mapinduzi kinajenga picha ya fukuto kubwa lililoko ndani ya chama

Mbowe kama una mshaur mzur 2025 usisusie uchaguz hata kama katiba mpya haitakuwa imepatikana
Kwanini?

1. Uchaguzi wa 2020 uliacha majeraha mengi ndani ya CCM ila watu walikaa kimya kwa kumuogopa Magufuli 3/4 ya waliogombea sio walioshinda kura za maoni na ukiona mtu kashinda kura za maoni ujue ana ngome kubwa ndani ya jimbo lake So 2025 watu waioshinda kura za maoni 2020 na ngome yao watataka kuonesha umwamba wao huku hawa ambao wamekuwa wabunge kwa huu muda pia wakitaka kuonesha wana nguvu pia hali itakayopelekea chama kugawanyika na sababu raisi aliyepo hawamuogopi basi kugawa kura kuu haitakuwa shida.

2. Team Magu vs team Samia(Kikwete) hapa mgongano ni mkubwa sana na kwa bahati mbaya haijulikani nan ana watu wengi ingawa CCM asili wana nguvu but pia Magu aliwaondoa sana hasa kwenye CC na Kamat kuu na kujaza watu wake mfurugano utaendelea.

3. Uwezo hafifu wa Samia
Kwa sasa chama kimekuwa cha ovyo sana kila mtu anajiropokea anavyojisikia bila woga. Jana nimemsikiliza sijui Mwenyekiti wa Iringa anaropoka huku Ndugai anaropoka huku Nape anapiga vijembe huku Lemutuz yaan kila mmoja sahiz haogop kuropoka.

4. Polepole
CCM wanaweza dharau anachokifanya ila wajue ni kitu kikubwa sana. Mimi naamin yule Bwana ametangulizwa na watu ili kupima msuli wa mama na jinsi mama anavyozid kumpotezea ndo inawapa nguvu walioko nyuma yake wakiamim 2025 hata wanaweza kumpinga bila uoga maana sio chaguo lao. Mama angeweza angechinja kichwa cha pole pole kutoa mfano kwa walioko nyuma yake ili waogope na waheshim mamlaka.

NB: Trust me CCM inagawanyika vipande vipande sana sababu ya uwepo wa mama na pia aliyofanya Magu huko nyuma
2025 Chadema itakusanya viti vingi sana narudia vingi zaid ya sana(Ingawa uraisi hawawez kushinda)

Mbowe na wenzio pls msijitoe uchaguzi wa 2025.
 
Kama Samia hataki kugombea basi aendelee kuwachekea washindani wake eti demokrasia..

Magu keshawazoeza WaTzn kuendeshwa kama punda hapa ni kula kichwa kwa kila anaenyanyua mdomo awe ccm au chadema...
Acha uongo upinzani gani una vilaza?. Magufuri alimteua mwana CUF kuwa Katibu Mkuu wa CCM au umesahau. Kuna mawaziri na manaibu mawaziri wangapi wametokea upinzani?

Juzi hapa baada ya kufanya faulo kwenye uchaguzi wakaenda kuwachukua wanawake kumi na Tisa was upinzani na kuwaweka bungeni na kuahidi kuwalinda kwa gharama yeyote.
 
Acha uongo upinzani gani una vilaza?. Magufuri alimteua mwana CUF kuwa Katibu Mkuu wa CCM au umesahau. Kuna mawaziri na manaibu mawaziri wangapi wametokea upinzani?. Juzi hapa baada ya kufanya faulo kwenye uchaguzi wakaenda kuwachukua wanawake kumi na Tisa was upinzani na kuwaweka bungeni na kuahidi kuwalinda kwa gharama yeyote.

We unaelewa mada kweli au unakurupuka tu? Ulipokuwa shule ndo ulivyokuwa unakurupuka kujibu maswali?
 
Mimi sio mbobez wa siasa ila ninachokiona kwenye Chama changu cha Mapinduzi kinajenga picha ya fukuto kubwa lililoko ndani ya chama

Mbowe kama una mshaur mzur 2025 usisusie uchaguz hata kama katiba mpya haitakuwa imepatikana...
Chadema tukisusa si ndio vizuri ili mchukue nchi kiulaini?

Huo upendo mkubwa kiasi hicho kqa chadema umetokana na nini?

Too Good to be offered by the unlikely friend
 
Acha uongo upinzani gani una vilaza?. Magufuri alimteua mwana CUF kuwa Katibu Mkuu wa CCM au umesahau. Kuna mawaziri na manaibu mawaziri wangapi wametokea upinzani?. Juzi hapa baada ya kufanya faulo kwenye uchaguzi wakaenda kuwachukua wanawake kumi na Tisa was upinzani na kuwaweka bungeni na kuahidi kuwalinda kwa gharama yeyote.
Kwa hiyo kina Lisu ndio wanaweza kuwa Rais? Lisu na Mwendazake Wana tofauti gani? Nani mgombea wa U Rais huko Upinzani?
 
Acha uongo upinzani gani una vilaza?. Magufuri alimteua mwana CUF kuwa Katibu Mkuu wa CCM au umesahau. Kuna mawaziri na manaibu mawaziri wangapi wametokea upinzani?. Juzi hapa baada ya kufanya faulo kwenye uchaguzi wakaenda kuwachukua wanawake kumi na Tisa was upinzani na kuwaweka bungeni na kuahidi kuwalinda kwa gharama yeyote.
Akili yake haina akili, mjaa LAANA huyo.
 
Kama Samia hataki kugombea basi aendelee kuwachekea washindani wake eti demokrasia..

Magu keshawazoeza WaTzn kuendeshwa kama punda hapa ni kula kichwa kwa kila anaenyanyua mdomo awe ccm au chadema...
Nani kilaza? Umeshampa madaraka ukaona alivyojasili! Mpe urais uone utofauti na ccm unsyoiabudu
 
Mimi sio mbobez wa siasa ila ninachokiona kwenye Chama changu cha Mapinduzi kinajenga picha ya fukuto kubwa lililoko ndani ya chama

Mbowe kama una mshaur mzur 2025 usisusie uchaguz hata kama katiba mpya haitakuwa imepatikana...
MaCCM yakifikaga kwenye uchaguzi yanakuwa pamoja kama Mashetani ya kisende No katiba no Uchaguzi. Wala Mbowe asiingie mkenge
 
Nani kilaza? Umeshampa madaraka ukaona alivyojasili! Mpe urais uone utofauti na ccm unsyoiabudu
Huyo Lisu na Mwendazake kuna tofauti gani? Mda wa kufanyia majaribia Nchi na maisha yetu haupo.Hana sifa za kuwa Rais ila mpinzani na mwanaharakati..

Sio kila anaenyanyua mdomo basi awe Rais ,haipo hiyo.
 
Ni uhayawani kushiriki uchaguzi wa 2025 kwa mazingira yaleyale ya 2020, 2015, 2010, 2005. Unless lengo ni kuambulia viti kidogo vya ubunge na ruzuku kiduchu

Hakuna namna NEC itamtangaza mgombea wa urais nje ya CCM
 
Upole utamgharim mama na Chama 2025

Cdm itashiriki iwapo mazingira sahihi vya ushindani yapo, na sio kushiriki ili kutakatisha ugomvi wa makundi ndani ya CCM. Wao CDM kama chama wanaweza kushiriki kutokana na hizi porojo mnazopiga hapa, lakini sisi wapiga kura tunaojitambua hatutatokea kushiriki chaguzi za kishenzi na kihayawani. Hatuko tayari tena kuona wapiga kura wa upinzani wakiuwawa, kuachwa na vilema vya maisha, ama kubambikiwa kesi, kisha wanasiasa wakae wafanye maridhiano na kupeana vyeo.

Ni bora tubaki salama na kutoshirikiana na viongozi waliopo madarakani bila ridhaa vya umma, huko mbeleni tutatengeneza machafuko ili kuwatoa watawala wasio na ridhaa ya umma.
 
Huyu mama mnamwona mpole ila ndo anawatafuna kimyakimya.The clever woman
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom