2025-2030 tunahitaji Mkapa mwingine

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Baada ya kifo cha rais wetu wa awamu ya tatu Ndugu Benjamin William Mkapa, ndipo watanzania walio wengi mbumbumbu kama mimi tumeweza kuelewa haya maneno ya kujenga nchi ni kujenga taasisi.

Lakini ni wazi kujenga nchi ni sawa na kilimo shambani, kuna hatua ya kulima na kupanda, kuna hatua ya kupalilia na kuweka mbolea na kuna hatua ya kuvuna na kula na katika maisha ya ukulima huwezi kupenda kuvuna na kula ukafanikiwa, kilimo pia hakifanikiwi kwa kulima na kupanda tu.

Nikitazama kuanzia awamu ya Tatu naifananisha tanzania na maisha ya mkulima.

Awamu ya Tatu walijikita katika kutengeneza taasisi hawa ni sawa na kusema waliandaa mashamba. tunaambiwa taasisi kama TRA, TANROADS n.k ziliundwa kipindi hicho ingawa yawezekana kipindi hicho hazikutoa matunda sana ni kwa sababu ukiandaa shamba hauvuni siku hiyo.

Awamu ya nne ukiitazama ni kama ilikuwa inafanya palizi na kuwekea mbolea. katika kipindi hicho sekita binafsi zilistawi sana. Kama ni biashara unaweza kusema awamu ya nne kilikuwa kipindi cha promosheni, yaani kipindi kama unachosikia makampuni ya simu yakisema kutuma miamala ni bure, kipindi unachosikia ukinywa soda unaweza kujishindia gari, lengo kwa hatua hii huwa ni kuwavutia watumiaji wengi zaidi ili wakishapatikana sasa ndio unaanza kuwatoza na kupata faida. Awamu ya nne mazingira ya kufanya biashara kwa watu binafsi yalikuwa mepesi sana na mzunguko wa pesa kwa wananchi ulikuwa mkubwa.

Awamu ya tano imekuja kwa staili ya mwenye shamba sasa anataka kuvuna na hapa ni pamoja na kukusanya kodi na kuhakikisha pesa inayokusanywa inafanya shughuli za kimaendeleo.

Sasa baada ya awamu hii ni wazi tunahitaji kuandaa mashamba mapya, tutanue wigo wa taasisi na ili tufanye hayo tunahitaji mtu mwenye kariba kama ya raisi wa awamu ya Tatu.

2025 tunamhitaji mkapa mwingine.
 
Weka kura yako kwa Tundu Lissu mwezi Oktoba nchi iendelee kuendeshwa kama taasisi na si show ya mtu mmoja!
Hivi huyu zaidi ya uropokaji na kujisifu kujifanya kiranja wa sheria ana nini alichofanyia taifa hili?

Ni mshamba fulani tu hivi asiyejitambua
 
Weka kura yako kwa Tundu Lissu mwezi Oktoba nchi iendelee kuendeshwa kama taasisi na si show ya mtu mmoja!
Hakuna kiumbe duniani aliye kigeugeu zaidi ya binadamu. Tayari umesahau wakati wa awamu ya 3 jinsi mlivyokuwa mnakejeli uongozi wake. Mmesahau jinsi mlivyokuwa mnamuandama yeye pamoja na mawaziri wake waandamizi [Daniel Yona, Bazir Mramba, Wilson Masilingi, nk.]
 
Hivi huyu zaidi ya uropokaji na kujisifu kujifanya kiranja wa sheria ana nini alichofanyia taifa hili?

Ni mshamba fulani tu hivi asiyejitambua
Kabla ya kuuliza kuna nini Lissu amelifanyia taifa! Jiulize wewe umelifanyia nini taifa?
 
Tujikumbushe mifumo imara ya kuendesha nchi ya kagoda, deep green, net group soln, escrow, Dawn's, epa nk nk nk.

Umenena vizuri 2025 -30 apatikane yule anayeonewa huruma ya kutengwa na kupigwapigwa ili aweza kupalili na kuitilia mbolea mifumo hii pendwa na mabunyenye ya ndani ya nchi/Local bunyenyezi.

Hukukosea JPM kaiharibu na kuififisha kama si kuiua hii mifumo ya kuendesha nchi.
 
Back
Top Bottom