2020 Uchumi wetu Tunauzika Rasmi

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,440
Ikiwa 2019 uchumi wetu umeshuka mpaka 4.1 kutoka 7.1 na hakuna njia au mkakati wowote wa Serikali wa makusudi wa kujikwamua ktk hali hii, basi ni wazi kwamba 2020 kuna hatari ya uchumi kushuka mpaka kufikia 1.1 au ikwa ni 0 kabisa

Miradi yote inayofanywa na Serkali kwa sasa inahitaji pesa na hakuna hata mradi mmoja mkubwa ambao una sura ya kuzalisha hivi karibuni. Mfano ni mradi wa Stiglas, huu utakamilika baada ya miaka 13 na Kama kutatokea upungufu wa pesa katika ujenzi wa mradi huu, unaweza kwenda hadi miaka 20.

Mradi wa SGR ili ukamilike Zinahitajika pesa nyingi ambazo Serikali haina, tunategemea misaada na mikopo ya kibiashara kutoka kwa Mabeberu. Wakigoma huu mradi hautakamilika kwa wakati, lakini pia hata ukikamilika bado mchango wake ktk uchumi ni mdogo sana kwa sababu huu mradi umekaa kihuduma zaidi.kote inakopita hii reli tayari kuna Barabara nzuri za lami na hakuna shida ya usafiri kabisa, hakukuwa na sababu yoyote ya kuanzisha mradi huu mkubwa ambao utatufilisi, badala yake Kama ni suala la kusafirisha mizigo kwa garama nafuu, tungeweza tukaiboresha Reli ya Kati ili kunusuru Chumi wetu.

Mradi wa ndege, huu kila mtu anajua ni mradi ambao Watanzania wanatakiwa wauhudumie Kama mgonjwa, kwa sababu ukiangalia ripoti ya CAG inajieleza kwamba unajiendesha kwa hasara.

Ukiangalia kwa ujumla biashara nyingi kwa sasa zinadidimia na nyingi kufungwa kabisa kutokana na kukosa walaji Sekta ya ujenzi ambayo ilikuwa inakwenda kwa kasi sasa hivi iko hoi, hakuna mwenye uwezo wa kujenga tena. Hata wale waliojenga hawana wateja wa kupanga, hotel nyingi ziko hoi gest hazina wateja kabisa, mfano hai ni huu msimu wa sikukuu, miaka 5 iliyopita msimu Kama huu huwa ni high season kwa wafanyabiashara, lakini Mwaka huu ni Kama Msiba. Hakuna shamra shamra Zozote, wanunuzi hakuna kabisa.hii ni dalili tosha kwamba Wananchi hawa pesa na matumaini yametoweka kabisa.

Hali hii ikiendelea namna hii, Ina maana Mapato ya TRA kwa mwaka 2020 yatapungua sana, mbaya zaidi hawa Mabeberu wa IMF na World Bank wanatuandama sana, wamefikia mahali sasa wanawatisha mpaka wawekezaji wapya kwamba Ati Tanzania siyo sehemu salama ya kuwekeza! Kwa maana hiyo tusitegemee wawekezaji wapya.

Korosho nayo ndiyo hivyo, inazidi kuozea maghalani.inatia uchungu. Raisi anajitahidi kutafuta japo Soko la mahindi Zimbabwe lakini kwa bahati mbaya sana tumeshachelewa, kwa sababu bei ya mahindi kwa sasa iko juu east Afrika kwa hiyo hatuwezi kuuza mahindi Zimbabwe kwa bei wanayoitaka. Mbaazi ndiyo kabisa hakuna mnunuzi. Yule mnunuzi aliyekuwa ananunua amegoma kwa sababu Serikali ilimdharau mpaka ikaamua kumpima mkojo, Na yeye akaamua kususa. Sasa wakulima wamebaki wanaduwaa hawajui la kufanya. Hakuna juhudi za kuwatafuta wanunuzi wapya.inauma sana!

Watanzania Tujiandae 2020 hali itakuwa mbaya kuwahi kutokea. Na bahati mbaya zaidi ni Mwaka wa uchaguzi, kwa hiyo Nchi itakuwa ktk hali ya uhitaji mkubwa wa pesa kwa ajili ya uchaguzi na pa kuzipata ni kwa hawa hawa wafanyabiashara wachache waliobaki wenye Roho Ngumu.au Wavumilivu.

Watanzania tutafanya Muujiza gani kuepuka hali hii? Hasa ukizingatia Zile mbwembwe za kwenye majukwaa kwamba 2020 tutakuwa na uchumi wa Kati kwa Sababu tulipata Gesi nyingi sana! Sasa iko wapi? Au imeibiwa? Kwanini Watanzania hawaambiwi ukweli na hii ni Nchi Yao ?!
 
Unaweza kutupa ushahidi wa uchumi kushuka kutoka 7.1% mpaka 4.1%
 
Hata mradi wa stiglaz goji nao hauna faida yoyote in short run had uwe rashed kutekelezwa ndio maana mkataba wake ni siri it means ni kuna harufu mbaya humo.Ukisoma bajeti ya nishati kuna miradi mingi ya maporomoko ya maji inayoweza ipa nchi megawat zaidi ya 5000 na ina gharama nafuu na pili inaweza kukamilika ndani ya mda mfupi kuliko kuhangaika na stiglaz na kuharibu hifadhi
 
Were sinuous umeandika mini mamas hujui uchumi hats sentiment vinginevyo no propaganda least wasiojua. Sinuous kaka unaelewa kit unachoongelea.
 
Halafu kinachokatisha tamaa zaidi, watu Kama akina Paramasamaki ndio tunawategemea ili tuweze kuondoka hapa tulipokwama, kiukweli wakati mwingine huwa namuonea huruma sana Mkuu wa Nchi hii, Maana yeye huwa anamteua Waziri akiamini atamsadia kumbe anamdidimiza kabisa.
 
Were sinuous umeandika mini mamas hujui uchumi hats sentiment vinginevyo no propaganda least wasiojua. Sinuous kaka unaelewa kit unachoongelea.
Sijasoma uchumi wala sihitaji kusoma uchumi. Mimi ni mkulima wa Mahindi. Lakini najua kusoma na kuandika. Nilisoma Ripoti ya uchumi wetu kupitia IMF. Na wewe pia Kama una ripoti yako iweke humu tuisome maana inaonekana ww ni mtaalamu. Watu wa aina yako ndio mnaopiga makofi wakati mpaka sasa hatuna mnunuzi wa korosho na zinaozea ghalani?
 
Hata mradi wa stiglaz goji nao hauna faida yoyote in short run had uwe rashed kutekelezwa ndio maana mkataba wake ni siri it means ni kuna harufu mbaya humo.Ukisoma bajeti ya nishati kuna miradi mingi ya maporomoko ya maji inayoweza ipa nchi megawat zaidi ya 5000 na ina gharama nafuu na pili inaweza kukamilika ndani ya mda mfupi kuliko kuhangaika na stiglaz na kuharibu hifadhi
Hivi mkuu niulize, ile miti yote itakokatwa inakuwa Mali ya nani?. Ya Serikali au ya mjenzi mwenye mkataba?
 
Walioandikishana mikataba ndio wanajua mm sina jibu kama wewe
Isije ikawa waliitamanii miti. Maana Kama mradi utakwenda kwa miaka 13 tena wakiwa wanakwenda ktk speed ya maxmum bila kukwama popote, naona kuna jambo limejificha ndani ya pazia
 
Tatizo lako hasa wewe nini . Una uchungu na nchi . Au unataka kusema Mbowe ana uchungu na nchi kuliko JPM. Mbona wote hapa JFM mnaandika kama mna PHD ya majibu yote ya maisha.
Kama umeshaona uchumi utakufa so why write? Unataka kusema ndo una majibu au mtu wa kuinua uchumi huo 2020. Acha kuzunguka na weka jina la mgombea wako .
Ikiwa 2019 uchumi wetu umeshuka mpaka 4.1 kutoka 7.1 na hakuna njia au mkakati wowote wa Serikali wa makusudi wa kujikwamua ktk hali hii, basi ni wazi kwamba 2020 kuna hatari ya uchumi kushuka mpaka kufikia 1.1 au ikwa ni 0 kabisa

Miradi yote inayofanywa na Serkali kwa sasa inahitaji pesa na hakuna hata mradi mmoja mkubwa ambao una sura ya kuzalisha hivi karibuni. Mfano ni mradi wa Stiglas, huu utakamilika baada ya miaka 13 na Kama kutatokea upungufu wa pesa katika ujenzi wa mradi huu, unaweza kwenda hadi miaka 20.

Mradi wa SGR ili ukamilike Zinahitajika pesa nyingi ambazo Serikali haina, tunategemea misaada na mikopo ya kibiashara kutoka kwa Mabeberu. Wakigoma huu mradi hautakamilika kwa wakati, lakini pia hata ukikamilika bado mchango wake ktk uchumi ni mdogo sana kwa sababu huu mradi umekaa kihuduma zaidi.kote inakopita hii reli tayari kuna Barabara nzuri za lami na hakuna shida ya usafiri kabisa, hakukuwa na sababu yoyote ya kuanzisha mradi huu mkubwa ambao utatufilisi, badala yake Kama ni suala la kusafirisha mizigo kwa garama nafuu, tungeweza tukaiboresha Reli ya Kati ili kunusuru Chumi wetu.

Mradi wa ndege, huu kila mtu anajua ni mradi ambao Watanzania wanatakiwa wauhudumie Kama mgonjwa, kwa sababu ukiangalia ripoti ya CAG inajieleza kwamba unajiendesha kwa hasara.

Ukiangalia kwa ujumla biashara nyingi kwa sasa zinadidimia na nyingi kufungwa kabisa kutokana na kukosa walaji Sekta ya ujenzi ambayo ilikuwa inakwenda kwa kasi sasa hivi iko hoi, hakuna mwenye uwezo wa kujenga tena. Hata wale waliojenga hawana wateja wa kupanga, hotel nyingi ziko hoi gest hazina wateja kabisa, mfano hai ni huu msimu wa sikukuu, miaka 5 iliyopita msimu Kama huu huwa ni high season kwa wafanyabiashara, lakini Mwaka huu ni Kama Msiba. Hakuna shamra shamra Zozote, wanunuzi hakuna kabisa.hii ni dalili tosha kwamba Wananchi hawa pesa na matumaini yametoweka kabisa.

Hali hii ikiendelea namna hii, Ina maana Mapato ya TRA kwa mwaka 2020 yatapungua sana, mbaya zaidi hawa Mabeberu wa IMF na World Bank wanatuandama sana, wamefikia mahali sasa wanawatisha mpaka wawekezaji wapya kwamba Ati Tanzania siyo sehemu salama ya kuwekeza! Kwa maana hiyo tusitegemee wawekezaji wapya.

Korosho nayo ndiyo hivyo, inazidi kuozea maghalani.inatia uchungu. Raisi anajitahidi kutafuta japo Soko la mahindi Zimbabwe lakini kwa bahati mbaya sana tumeshachelewa, kwa sababu bei ya mahindi kwa sasa iko juu east Afrika kwa hiyo hatuwezi kuuza mahindi Zimbabwe kwa bei wanayoitaka. Mbaazi ndiyo kabisa hakuna mnunuzi. Yule mnunuzi aliyekuwa ananunua amegoma kwa sababu Serikali ilimdharau mpaka ikaamua kumpima mkojo, Na yeye akaamua kususa. Sasa wakulima wamebaki wanaduwaa hawajui la kufanya. Hakuna juhudi za kuwatafuta wanunuzi wapya.inauma sana!

Watanzania Tujiandae 2020 hali itakuwa mbaya kuwahi kutokea. Na bahati mbaya zaidi ni Mwaka wa uchaguzi, kwa hiyo Nchi itakuwa ktk hali ya uhitaji mkubwa wa pesa kwa ajili ya uchaguzi na pa kuzipata ni kwa hawa hawa wafanyabiashara wachache waliobaki wenye Roho Ngumu.au Wavumilivu.

Watanzania tutafanya Muujiza gani kuepuka hali hii? Hasa ukizingatia Zile mbwembwe za kwenye majukwaa kwamba 2020 tutakuwa na uchumi wa Kati kwa Sababu tulipata Gesi nyingi sana! Sasa iko wapi? Au imeibiwa? Kwanini Watanzania hawaambiwi ukweli na hii ni Nchi Yao ?!
 
Isije ikawa waliitamanii miti. Maana Kama mradi utakwenda kwa miaka 13 tena wakiwa wanakwenda ktk speed ya maxmum bila kukwama popote, naona kuna jambo limejificha ndani ya pazia
Inashangaza walivyokomalia mradi huu wakati njombe kuna mito mitatu ya maporomoko wanapiga stori tu nayo,Mbeya na Ruvuma,Njombe kuna makaa ya mawe wataimba ngonjera tu lakini huu imekua kama ule wimbo wa uchumi wa gas
Sasa mradi usipoisha ndani ya mda wa mkuu itakuaje?
 
Tatizo lako hasa wewe nini . Una uchungu na nchi . Au unataka kusema Mbowe ana uchungu na nchi kuliko JPM. Mbona wote hapa JFM mnaandika kama mna PHD ya majibu yote ya maisha.
Kama umeshaona uchumi utakufa so why write? Unataka kusema ndo una majibu au mtu wa kuinua uchumi huo 2020. Acha kuzunguka na weka jina la mgombea wako .
Jikite kwenye hoja zake acha hadithi zingine
 
Tatizo lako hasa wewe nini . Una uchungu na nchi . Au unataka kusema Mbowe ana uchungu na nchi kuliko JPM. Mbona wote hapa JFM mnaandika kama mna PHD ya majibu yote ya maisha.
Kama umeshaona uchumi utakufa so why write? Unataka kusema ndo una majibu au mtu wa kuinua uchumi huo 2020. Acha kuzunguka na weka jina la mgombea wako .
Kama nakuona ulivyo mind halo hahaaaa
 
Back
Top Bottom