2020 hiyo CCM ni kusuka ama kunyoa?

2020 hiyo CCM ni kusuka ama kunyoa?

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
7,564
Reaction score
9,043
Kesho kutwa Mungu jalia tunauanza mwaka 2020, ambapo CCM wana kazi moja kubwa kusuka ama kunyoa, wasiojua tafsida CCM wana kazi moja kuiokoa nchi au kuiangamiza.

Kila la heri wana JamiiForums kuelekea new year Mungu awabariki sana.
 
kama sheria na tume ya uchaguzi itabaki kama zamani hakuna jipya ccm inapeta kwa kishindo kikuuu
 
Hakuna jipya wembe ni ule ni ule, this time utakuwa butu zaidi
 
kama sheria na tume ya uchaguzi itabaki kama zamani hakuna jipya ccm inapeta kwa kishindo kikuuu
Mkuu naongelea uchaguzi wa ndani ya ccm uliojaa makundi , kundi la lowasa ,kikwete,kundi jipya la wasaka tonge nani ataibuka kidedea kati ya ccm kindakindaki na ccm wachumia tumbo ,wasaka vyeo bendera fuata Yaani vita kati ya vingunge na vikwete.
 
Viongozi wa upinzani wajue wasipotuongoza kudai tume huru ya uchaguzi, sisi wapiga kura wao hatuwezi kushiriki huu ushenzi unaoendelea hivi sasa. Hatutakuwa na muda wa kwenda kupanga mstari kupiga kura ambazo hatujui usalama wake.
 
hakuna jipya mkuu hizi porojo za chura tu ng'ombe hawezi acha kunywa maji ishu tume huru hapo nitakubali
 
Mkuu naongelea uchaguzi wa ndani ya ccm uliojaa makundi , kundi la lowasa ,kikwete,kundi jipya la wasaka tonge nani ataibuka kidedea kati ya ccm kindakindaki na ccm wachumia tumbo ,wasaka vyeo bendera fuata Yaani vita kati ya vingunge na vikwete.
ndani ya chama mimi sioni kama mtu ataamua kusimama na magufuli maana sheria yao ni ngumu kidogo hawa wengine watasubiri 2025
 
Back
Top Bottom