2016 US Election Results: Donald Trump has won the presidency

2016 US Election Results: Donald Trump has won the presidency

Marekani ni moja kati ya mataifa yenye uhimilivu wa katiba, sheria na sera (za kiuchumi, siasa na mahusiano ya kimataifa). Nchii ya Marekani haiongozwi na matamko au hisia za mtu alizo nazo au anazozisema kwenye majukwaa ya kisiasa ikiwamo kwenye kampeni. Hivyo basi, ni dhairi kwamba hakuna cha kuhofia zaidi ya uoga wako mwenyewe kama alivyosema Franklin Delano Roosevelt
MIXOLOGIST nakubaliana na wewe, nchi za wenzetu zina 'think tank' ambayo inasimamia usalama na ustawi wa kiuchumi, hivyo hata kama uropoke vipi, kauli zako haziwezi kubadili mambo.
 
Umofia kwenu Great Thinkers,

Trump alipata kusema akishinda kiti cha urais

  1. Waislam watapigwa BAN
  2. Latinos ni rapist
  3. Africa itawaliwe tena
  4. Atajenga ukuta kuzuia Mexicans
Kama kiongozi huyu angekuwa anatokea Africa akasema anafukuza wazungu wote kwa sababu walitunyonya sana na ni wezi, basi kwa huu ushindi wa Trump tungeshuhudia

'TRAVEL WARNINGS FOR U.S CITIZENS....' na blah blah kibao na kubezwa mshindi.

Swali je nchi za kiislam zimeshatoa Tahadhari ya raia wake wanaposafiri kuelekea U.S?
Obama alikua hamtaki Trump lakini, Trump kapita, hivi ni kwanini hakuja kujifunza namna ya kuendesha chaguzi
 
Yaani natamani hii tume ingekuwa inasimamia uchaguzi wa nchi zote duniani! Free and fair election. Yaani ndani ya saa tu, matokeo yanaanza kutiririka kama yalivyopatikana kwenye vituo. Siyo hapa kwetu kale kazee kapumbavvv eti kanatuambia mimi natangaza matokeo kadri ninavyoyapokea kutoka Lumumba, shenzy type kabisa!!
Kwani huku huwa tunafanya uchaguzi au kupoteza muda na fedha? mie nilishaapa sitajisumbua tena yaache yatawale.
 
Kwani huku huwa tunafanya uchaguzi au kupoteza muda na fedha? mie nilishaapa sitajisumbua tena yaache yatawale.
Mama kubwa, kama nakuona vile ulivyosusa!! Umenichekesha aiseeee, eti "yaache yatawale?"
 
Hayo maneno mengine sio kama yatafanyika ni kuchangamsha kampeni tu. Mfano kama yule jamaa aliesema million 50 kila kijiji mpaka leo hajawapa.


Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]
umenena vyema.
na kwenye kampeni yetu 2015 akatuaminisha kupatiwa katiba mpya ambayo sasa imeota mbawa kwi!kwi!kwi!
 
Huwezi kushinda urais Marekani bila kura za minorities eh?

😀😀😀😀😀😀😀😀

Kuna wanakijiji wengi sana walikuwa hawapigi kura katika chaguzi zilizopita aisee, mpaka watu wakajiaminisha kuwa bila minorities huwezi kuwa Rais Marekani. Unbelievable!
 
Nchi nyingi za Africa wanaong'ang'ania madarakani ni muda kutolewa kwa nguvu na kutawaliwa!
 
Milioni 50 ziko palepale hiyo ni ahadi ndani ya miaka mitano, acha mihemko kajenge chagadema inayojifia
 
Kuna wanakijiji wengi sana walikuwa hawapigi kura katika chaguzi zilizopita aisee, mpaka watu wakajiaminisha kuwa bila minorities huwezi kuwa Rais Marekani. Unbelievable!

Mimi nilijaribu ku reason na watu na kuwaambia kwamba kwa jinsi Marekani wanavyochagua rais [kwa EV], na ukiangalia demographics za majimbo mengi utaona kwamba Wazungu bado ni overwhelming majority wa states nyingi sana.

Nikabishiwa weee....nikasema basi bana. Nikajisemea tu mi mbeba maboksi nisiye hata na shahada ya chuo kikuu nitabishanaje na vichwa bana....nikasema sawa labda wako sahihi.

Now the silent majority have spoken.

Halafu, Trump wala hajafanya vibaya kwa minorities. Nadhani kapata asilimia kubwa ya Latinos kuliko hata Romney.
 
Zile pongezi wanazotoa kwenye mitandao, jamaa mwenyewe hata kuziona hazioni.

Zinaishia kujibiwa na secretary wa timu ya kampeni tu.

Pongezi za Rais kwa Rais huwa zinaenda kwenye official channels sio twitter na Fb
 
umenena vyema.
na kwenye kampeni yetu 2015 akatuaminisha kupatiwa katiba mpya ambayo sasa imeota mbawa kwi!kwi!kwi!
Wapi alikuahidi katiba mpya, unaota !?
Hayo maneno mengine sio kama yatafanyika ni kuchangamsha kampeni tu. Mfano kama yule jamaa aliesema million 50 kila kijiji mpaka leo hajawapa.


Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Baada ya Trump kutanganzwa rais mpya wa Marekani hali za waafrika wenzangu huko ni pressure tupu!

Na kwa unafki wa watu weusi nahishi hawata chelewa kujichekesha ili wahurumiwe.

Kweli wengine walijiona ni miungu watu kwa kuishi huko tena wakiwa ni watumishi kwenye kambi za vikongwe.

Nina Dada yangu wa tumbo moja alikwenda kufanya kazi huko akatelekeza mpaka wazazi mpaka kwenye misiba yao aligoma kurudi akidai asamehewe hawezi vumilia hali ya hewa ya huku.

Chaajabu Leo kaanza kuwasiliana na ndugu akieleza mashaka yakuendelea kuishi huko kufuatia ushindi wa Bwana Trump.

Asante Trump umeleta heshima nyumbani , timua wote huko warudi kukabiliana awamu ngumu ya kipindi hiki cha baba jesca.
 
Katika sera zake za mambo ya nje DONALD TRUMP amesema: baadhi ya nchi za Afrika zinazo tawaliwa kimabavu, na zilizo kidhiri ufisadi na vita, inapaswa wakoni wa kizungu warudi kuzitwa, na kuzitawala tena.
JE WEWE UNAONAJE NI NCHI GANI ZINAPASWA KUTAWALIWA TENA
 
Back
Top Bottom