2016 mwaka unaomalizika vibaya kwa mashabiki wa siasa za kiliberali.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Ukisema Big Government kwa mtu mwenye kushabikia sera za chama cha Republican atajua unamaanisha ukubwa na urasimu wa serikali, vitu ambavyo ni sifa kuu ya chama cha Democrat.

Sera za Republican zinaweka msisitizo katika udogo wa serikali, uwepo wa kodi ndogo ambazo haziathiri ukuaji wa sekta za kibiashara. Pia zinaweka msisitizo katika uondoaji wa urasimu wa kiserikali.

Republican ambacho ni chama kinachopewa sifa mbaya duniani kutokana na historia ya kina Ronald Reagan na George Bush wote wawili, kimekuwa ni chama ambacho ndani ya miaka minne ijayo kitaiongoza Ikulu pamoja na bunge la Marekani.

Inaonekana kuwa sera za kiliberali, sera zenye kutilia mkazo wa faida inayopatikana kuwa mali ya wengi, zimeshindwa kuwashawishi wapiga kurea wa Marekani ili wampe nafasi Mama Hillary Clinton.

Na sio Marekani tu, hata Ulaya na kwenye Waingereza wameona ni muda muafaka wa kila mtu afe kivyake, baada ya kuamua kujitoa kwenye umoja wa Ulaya. Ujerumani kwa Mama Angela Merkel na kwenye hakujatulia, vyama vyenye mrengo wa kulia vinamtupia lawama Mama huyu kwa sababu moyo wake wa huruma ndio umeifanya Ujerumani iwe kimbilio la wageni kutoka Afrika na mashariki ya kati.

Wageni ambao hawachelewi kuendesha lori kwa mwendo kasi wakielekea kwenye sehemu iliyokuwa imejaa watu wanaofanya manunuzi ya sikukuu ya krismasi. Jaribu kupiga picha mwendawazimu mmoja aingie kwa kasi pale mtaa wa Congo Kariakoo siku moja kabla ya krismasi mida ambayo watu wapo kwenye manunuzi ya sikukuu.

Sera za kiliberali zenye kutawaliwa na utu na upendo, zenye kuwajali wasiokuwa nacho, zinaonekana ni mzigo kwa mataifa ya Ulaya na Marekani.

Mwaka 2017 sio mwepesi sana kwa Afrika, na nchi zote ambazo zimelemazwa na uliberali. Ni mwaka wa kujitegemea kweli kweli, maana wazungu wameshaona kuwa uliberali unawazingua.

Na tuwe tayari kujifunga mkanda, Donald Trump anao muda wa kuifanya Marekani irudishe heshima kiuchumi duniani, muda wa kuibembeleza Afrika sidhani kama anao kwa sasa.
 
tapatalk_1457719968938-1.jpeg
 
Back
Top Bottom