2015 yako ilikuaje,lets share,2016 umejipangaje

2015 yako ilikuaje,lets share,2016 umejipangaje

Amekuwa mwema sana hadi najishangaa.

we will celebrate the good things HE has done to me shortly.

usimwambie mtu uje mwenyewe.

hahahahahahaha

Kweli kabisa.
Memis wewe pm
 
Mimi nime accomplish a big milestone Ila huu Mwaka umekuwa punctuated na changamoto za hapa na pale, Ila namshukuru Mungu kwa uzima haya mengine ni ya kuyapita.
Life goes on
 
As for me, inawezekana mwaka 2015 ukawa ndo mwaka ambao nimekutana na changamoto nyingi pengine tangu nizaliwe au nilipoanza kujitegemea kimaisha.
Yapo mengi ambayo nilipanga kuyafanya ndani ya mwaka 2015 ikiwemo kumuabudu Mungu ktk roho na kweli (mara kadhaa nimekuwa nikianguka dhambini), kuubadili mji waishio wazazi wangu, kufunga ndoa na mwanamke niliyeamini kuwa ni wa ndoto zangu and to start a familiy with her, kufanya saving itokanayo na kipato changi, kupunguza utumiaji wa pombe, kupata kiwanja n.k

Nasikitika kusema kuwa, mengi kati ya niliyoyapanga hayafanikiwa. Kwamba niliplan kuoa ifikapo Novemba 2015, mwanamke akanikimbia, kwenye ishu ya saving sijafanikiwa, kiwanja still mchakato unaendelea, kanisani mahudhurio yangu yamekuwa hafifu, pombe kuna nyakati nilikunywa kupita kawaida.
Angalau kidogo naweza sema nimebadili kwa kiasi mji waishio wazazi wangu na hali zao, ingawa sio kwa kiwango ninachotaka.

Aidha, mwaka 2015 umenifanya nitambue kiuhalisia ile kauli ya "Binadamu wabaya", coz baadhi ya watu niliowaamini, wao hawaja waaminifu kwangu. Wapo ambao walinikopa pesa ambapo hawajawa waaminifu kwenye kuzirejesha, takribani Tshs. 800,000/= nilizowakopa jamaa kwa nyakati tofauti hawajazirejeshwa.
Pia hata mwanamke niliyemuamini naye aliishia kuniumiza, I thank God nimesha-move on, but ni jambo ambalo lilikuwa changamoto in 2015, na kuwa ni mwaka ulionifanya nipitie kipindi kigumu cha kimahusiano ya kimapenzi, tofauti na nilivyotarajia.

Yapo ambayo nimejifunza kutokana na changamoto nilizopitia:-
1. Kuendelea kufanya kazi kwa bidii, na kufanya saving itokanayo na kipato halali.
2. Kuchagua marafiki kwa uangalifu, tena ambao watakuwa na mchango chanya ktk suala la maisha, sio wale wa kampani za pombe tu...
3. Kila kitu kinabadilika isipokuwa mabadiliko yenyewe, as unaweza kumuamini mtu kumbe hafai kuaminiwa.

My plans for 2016, yapo mengi ingawa ya muhimu ni pamoja na yafuatayo:-
1. Kumuabudu Mungu ktk roho na kweli tena kwa Kujisajili kanisani ninakoabudu (African Inland Church of Tanzania @AIC- T)
2. Kufanya kazi kwa bidii, sanjali na kuweka akiba itakayosaidia kufanikisha mipango yangu mbalimbali ya kimaendeleo.
3. Kujiendeleza kitaaluma kwa kusoma Masters degree.
4. Kuendelea kuwasaidia wazazi ikiwa ni pamoja na kubadili hali ya mji waishio, as suala la kuwasaidia financially nimekuwa nikilifanya kikamilifu on monthly basis, na kila nipatapo an extra income.
5. Kukamilisha mchakato wa kupata kiwanja ifikapo mwezi Aprili, 2016.
6. Kuwa na serious relationship, kwa kumpata binti ambaye baadaye atakuja kufanyika kuwa Mke. (Mungu anisaidie ktk hili) as biblia ninayoiamini inanifundisha kuwa Mke Mwema hutoka kwa Mungu. Rejea Mithali 19:24 "Nyumba na Mali ni urithi apatao mtu toka kwa wazee wake, lakini Mke mwenye busara hutoka kwa Mwenyezi Mungu".

Ee Mwenyezi Mungu nakushukuru kwa zawadi ya uzima na uhai uliyonipa mwaka 2015, nakuomba uendelee kuwa nami siku zote za maisha yangu, ukinilinda, kunisaidia sambamba na kunijaza roho Mtakatifu wako, atakayeniongoza kutenda Mema kwa jinsi inavyonipasa... Amen!!!
 
what a saddest story, my beloved lover since past 3yrs has gone to another man,...anyway I'm proud to breath upto a moment
 
Back
Top Bottom