2015 ipigie kura CCM

Hapo chini kwenye RED, Mkuu Mwiba umeniacha sina mbavu.

Yaani kwa lugha nyingine ni kwamba unamwambia mzee huyu hapo chini kwenye picha ya kwamba acha mwiba wa samaki (kupondewa nyumba yake na buldoza) ikamkwamie salama kooni kwa kuwa ni mchezo wake kwa kujichagulia wenyewe tu eti??


 
Tatizo sio serikali kuvunjia watu,ila serikali ilikuwa iwawahi hao wanaovamia au kujenga sehemu ambazo hazina kibali cha kujenga ,ingawa kuna zile zilizovinjwa kandokando ya bahari zilikuwa na vibali au watu walikuwa na vibali ,kama ni vya halali au haramu ,hio ni kazi ya serikali kujua.

Kuwawahi ni pale unapoona wanaanza kufyeka na kuchimba misingi au kusimamisha fito kwa zisizo hitajia msingi,unawasimamisha na ikibidi serikali kupitia vyombo vyake kuwapa kosa na kuwataka wavamizi hao kulipa kiasi fulani cha hela na kama haitoshi hata kuwashitaki ,lakini kuwawacha watu wajenge hadi wanahamia wanaoana wanazaa na kujukuu ,afu seikali inazuka na bomoabomoa ,eti wamevamia eneo ,hivi ilituchukua siku,miezi au miaka mingapi kuvaana na nduli Iddi AMini alipovamia nchi yetu ?

Serikali inavunja na kutothamini haki za binadamu ,inawafanya wananchi wake kama wanyama ,tena wale wanyama waharibifu wanaofaa kusakwa na kuuliwa ,maana kumvunjia mzee kama huyo kajumba chake ,umekusudia nini kama si kumuua ! Sisemi kama upinzani itakuwa kila mtu afanye atakavyo, hapana ila kuwepo na kuwawahi wavamizi hawa kabla hawajaanza kuzaana !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…